Mwenendo wa Bunge wakera wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenendo wa Bunge wakera wananchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Feedback, Jun 21, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, amesema ameanza kupokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa wananchi wakieleza kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo. Akitoa matangazo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Spika Makinda, aliwataka wabunge wabadilike ili kuheshimu kanuni na taratibu za Bunge kwa lengo la kurejesha hadhi ya chombo hicho muhimu kwa mustakabali wa Taifa.

  “Wananchi wananitumia meseji nyingi sana, kwamba Bunge halina heshima tena mbele ya jamii kutokana na vitendo vinavyofanywa na wabunge wawapo bungeni. Wanasema walikuwa wanapenda sana kusikiliza na kufuatilia matangazo ya vipindi vya Bunge kupitia redio na televisheni, lakini sasa hawana hamu kabisa na hawatuangalii,” alisema Spika Makinda.

  Alisema vitendo vya utovu wa nidhamu kwa wabunge wengi na kutoheshimu kanuni za Bunge kwa kuomba miongozo na taratibu bila kuzingatia mpangilio mzuri, kwa kiasi kikubwa ndiko kulikowafanya wananchi kutopenda kufuatilia vikao hivyo.

  “Nawaombeni wabunge wote tubadilike, ili turejeshe imani na hamu ya wananchi kutuangalia na kuona tunawawakilisha vipi ndani ya Bunge na namna Serikali inavyoeleza utekelezaji wa kero zinazowakabili wananchi,” alisema.

  HabariLeo.
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  hapo ccm imekula kwao walizani bunge ni sehemu ya kufanya ushabiki wa chama na miongozo yao hisiyo na maana
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Angetilia mkazo wa kuanza kubadilika yeye kiongozi mbele kabla ya anaowaongoza.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ujumbe huo humwambia kuwa anaendesha bunge vibaya, lakini yeye anadhani kama alivyotangaza
   
Loading...