Mwendokasi kituo cha Gerezani waheshimuni wateja wenu wanaokwenda Mbezi

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!

Leo kwa mara ya kwanza nimepanda mwendokasi mchana yaani majira kama ya saa 8 na nilichokiona palee Gerezani kinatia huzuni kwa kweli jinsi abiria waendao Mbezi wanavyoteseka na jua kali la mchana kwenye foleni wakati stand ni kubwa.

Hivi kweli watumishi wa stand hawajaliona tatizo au wanangoja mpaka watu waanze kupigia kelele,kama hauna wazazi nyumbani unaweza usione tatizo.

Masikikini nimekuta mzee na koti lake la mbunge wamemuweka kwenye foleni anangoja gari kapanga mstari,hapa ishu sio mzee ishu ni kwamba stand ya Gerezani ni kubwa sana wanashindwaje kufanya layout nzuri ili wale wanaopanda mabasi ya kwenda Mbezi mchana wa jua wasisimame mstari juani??

Jambo lingine kumekuwa na shida sana baada ya yule dada aliyekuwa anatangaza vituo kukaukiwa na sauti
vituo havitangazwi watu wanalalamika sana kupitishwa vituo kama ni mgeni wa jiji wale unaweza zunguka vituoni panda shuka kama kichaaa ,hivi hili hawalioni wakuu au sababu wao hawatumii huu usafiri?

Nashauri hawa wakurugenzi wangekuwa wanatenga muda wao hata kwa mwezi mara moja kusafiri na hizi Mwendokasi kusoma changamoto zinazowakabili wateja wao kuliko kuweka namba tu wakingoja watu tuwapgie tuwaambie kero zetu .
 
Tatizo mradi wa uma na hauna mshindani

Ni kosa kubwa kuita mwendo Kasi wakati mchakato mzima wa kupata gari na safari yenyewe unaweza kuzidi saa nzima na karaha za kutosha.

Kwakua viongozi wetu ambao ni zao la wanasiasa Hawa Nia ya dhati kusaidia wananchi basi tuvumilie kudumisha amani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom