This is very wrong information: "Dala Dala" does not mean "Dollar" DALA DALA lilitokana na nauli iliyokuwa inatozwa miaka ile ikiwa na shilingi 5 ya pembe tatu, watanzania walikuwa wakiita jina dala. Baada ya mfumo wa mabasi madogo kuanza nauli ikiwa ni dala, yaani shilingi 5. wapige debe wakawa wanaita wateja kwa kuwaambia nauli ni dala tu, yaani kariakoo ni dala tu, dala dala post, dala dala kariakoo na nk. kumbuka kipindi kile kulikuwa na mabasi ya ikarus ambayo nauli ilkuwa ni zaidi ya sh. 5. Baada ya hapo mabasi madogo yakaitwa dala dala kwa sababu nauli yake ilikuwa ni dala. ikumbukwe kuwa baadae magari aina ya chai maharage yalikuja. nayo yakaitwa CHAI MAHGARAGE, mpaka sana ufafiri km huu popote unapotumika unaitwa chai maharage, hata kule zanzibar miaka miwili iliyopita yalikuwa yakiitwa chai maharage.
Waandishi wavivu waache kupotosha umma.