Baada ya Serikali kushindwa ni muda sasa wa kurejesha Daladala za kusafirisha abiria Kariakoo-Kimara-Mbezi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,464
222,724
Kama ilivyoshindwa mambo mengi, kufikia hadi kuuza Bandari basi ni vema sasa kurejesha tena usafiri wa Daladala kama ilivyokuwa awali Kutoka Kariako hadi Mbezi kupitia Kimara.

Hii ni kwa sababu wakazi wa maeneo hayo wanayo haki ya kusafiri kutoka makwao na kwenda mjini.

Naona dalili ya Jambo baya kutokea muda wowote kwenye Stendi ya Mwendokasi Gerezani

Angalia hali hii, hawa wote wanazo tiketi mkononi, kitendo cha kuwauzia tiketi huku mabasi yakiwa hamna japo ni Wizi lakini pia kunasababisha manung'uniko yatakayokuja kuzaa maafa kwa ngumi kuvurumishwa kwenye stendi hiyo

Lakini kwanini tufike huko?

Screenshot_2024-05-23-15-22-36-1.png

PIA SOMA
- Daladala za Mbezi kupitia Manzese, Fire hadi Mnazi Mmoja zimeanza kazi rasmi
 
Niliandika humu Mama Samia kafeli sana,,yaaani wameshindwa kuwambia watu wa daladala wanununue magari makubwa wendeshe BRT?Kampuni mwanzoni lianza vizuri lakini sasa imekuwa ovyo sana na bahati mbaya hawasemi na waandishi wa habari Wala hawawaulizi wahusika wa serikali
 
Waandishi wa Habari wa Tanzania wameelekezwa kusifia serikali tu, vinginevyo hawatapewa matangazo
 
Back
Top Bottom