Mwendesha pikipiki achomwa moto bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwendesha pikipiki achomwa moto bure

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 24, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Mwendesha pikipiki achomwa moto bure


  Na Jovither Kaijage, Ukerewe

  MWENDESHA pikipiki mmoja ameuawa na wananchi katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza baada ya kugongwa na baiskeli, katika ajali iliyosababisha kifo cha mtu mmoja kati ya wawili waliokuwa wamepanda baiskeli hiyo.Mwendesha
  pikipiki aliyeuawa kikatili ni Eric Elius (34) mkazi wa Kijiji cha Buhima wakati aliyekufa katika ajali hiyo ni Martha Kanyago (20) Mkazi wa Kijiji cha Chankamba, Ukerewe na mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Igombe, Ilemela jijini Mwanza.

  Akithibitisha tukio hili Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Simon Sirro alisema limetokea juzi saa 12:00 jioni kati ya kijiji cha Igalla na Chankaba wilayani Ukerewe.

  Alisema mwendesha baiskeli aliyetambuliwa kwa jina la Muoja Mabagara, mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Igalla ambaye ametoroka, alishindwa kuimudu kutokana na mwendo kasi katika mteremko, hali iliyosababisha ayumbe na kugonga pikipiki.

  Katika ajali hiyo Martha aliyekuwa abiria wake, alipoteza maisha.

  Kamanda Sirro alifafanua kuwa baada ya ajali hiyo kutokea, kundi la watu lilijitokeza na kumpiga kwa fimbo na mawe mwendesha pikipiki huyo, kisha wakamfunga mikono na kumchoma moto pamoja na pikipiki yake.

  Kamanda huyo alisema tayari jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwapata waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kwa mtu wa kawaida kukubaliana na hoja baiskeli imeigonga pikipiki na kusababisha mauti kwa huyohuyo mwendesha baiskeli hata kama simulizi hiyo ni ya kweli...........................

  Waendesha pikipiki wote yabidi wawe na kofia maalumu kwa kazi hiyo na sheria hiyo itungwe kama haipo na isimamiwe kidete vinginevyo tutazidi kulia na khali hii ya kusikitisha......................
   
 3. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,050
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Ni kitu cha kawaida sana hiki, vipi useme haiwezekani?? Hata magari yanagongwa na baiskeli
   
Loading...