KASHEBO
Member
- Dec 4, 2012
- 31
- 4
Basi wapendwa, namalizia ili sasa ujue kwanini kichwa cha habari kipo vile.
Baba yule akaniambia 'mimi sijali kwamba umekana humjui kimapenzi ila mimi nakuonya kama ulikuwa na mahusiano naye kuanzia leo achana naye na hata kama humjui usimsogelee maana mimi nishawekeza mali zangu nyingi na niko tayari kumfanya chochote ambaye ataonekana ndio tatizo la yeye kuachana na mimi na hili analijua mke wangu na mama yake na hata yeye analijua, naweza hata kumloga mtu huyo' basi baada ya kunitisha hivyo yule baba akasema mimi na wewe ni wanaume na hata kama hujapitia mambo kama haya ipo siku utakuwa mkubwa kama mimi alafu akasema kuanzia leo mimi nawewe ni marafiki ukipata nafasi njoo pale bwalo la jeshi ulizia jina langu ntakununulia hata kinywaji. Nikamkubalia baba yule na akaaga na kuondoka nikamsindikiza japo nilikuwa nimejawa na woga uliochanganyikana na hasira.
Niliporudi ndani nikamkuta mpenzi wangu eti anajiliza kwa kuwa alikuwa anasikia kila kitu na mimi kila kitu nilijua amesikia ndio maana nkawa namuuliza yule baba maswali ili atoe maelezo ya kina. Eti akasema nikweli huyu baba alikuwa mpenzi wa tangu zamani lakini tangu nilipokupata wewe nikaachana naye ila amekuwa king'ang'anizi akinitishia kunipiga wakati mwingine anakuja hadi nyumbani, kuna siku eti alikuja na bunduki kumtisha akimuacha anapiga risasi. Mimi nikasema kwanini hukuniambia ukweli akasema sikuta wewe ujue, akasema mambo mengi aliyoeleza sio ya kweli simu ambayo alimnunulia baada ya kuona anataka kuachana naye ilibamkubali tena na alimlazimisha kuichukua ndo akaniletea mimi.
Baada ya kuona haitumii yaani akikutana naye anakuwa hana simu hiyo akimuuliza anamwambia nimeiacha nyumbani akamwambia airudishe. Mimi nikawa mkali na kumwambia mimi na yeye basi, akalia sana na kunishi nimsamehe, alikuwa hajawahi kulala kwangu lakini siku hiyo alilala tena bila kwao kujua yuko wapi. Baada ya kunibembeleza kwa muda mrefu nikamsamehe labda kwa kuwa alinipa zawadi ya penzi la kubembelezwa.
Tuliendelea pamoja kwa muda tena wa miezi kama minne baada ya kumwambia kwa kuwa ameshanajua baba yule naishi hapa inabidi niame, akakubali kunipa kiasi cha tsh 180000 kama kodi ya miezi 6 nikapange kwingine. Kuna siku nilimua twende kutembelea maeneo ya jeshini huko kwasababu alishasema ameachana naye muda mrefu tena kuna siku tulikutana naye mjini hakujali (kumbe hakutuona) yeye akasema si umeona.
Wakati tumefika maeneo ya kwao tunatembea tumeshikana mikono, mimi ndo nilkuwa wa kwanza kumuona lakini kwa kuwa nilijua hakuna shida sikushtuka, alipo mwona akaniachia mkono ghafla, na yule askari alipotuona akaja kasi na kumshika yule mpenzi wangu na kuanza kumchapa vibao vikali, nilijaribu kumtetea kwa kumwambia mimi nimekutana naye pale tu wala si mpenzi wangu ila akaniambia kama hayakuhusu wewe ondoka.
Nilisikia mpenzi wangu akipiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio jamaa alizidi kupiga sana na kumzoa mitama barabarani huku yeye akijitetea kuwa mimi hanijui, ila yule baba alikuwa anamuuliza si ulisema tukutane leo mbona hukutokea? Kumbe ulikuwa na huyu kijana na nikimaliza wewe namwendea yeye, ila yule msichana akasema wala hakuna haja kuja kwangu maana mimi sijui kitu. Niliamua kuondoka katika eneo la tukio nikaelekea nyumbani huku nalia, nilikuwa natembea naongea peke yangu njiani nikijiuliza mimi sijawahi hata kumfinya mpenzi wangu leo anapigwa kama mbwa mbele yangu mimi siwezi hata kumsaidia, lakini roho nyingine inaniambia mwache akome ni umalaya wake na uongo wake alionao.
Nilipofika nyumbani nikalala lakini kutokana na hasira niliyokuwa nayo iliyochanganyikana na uchungu sijui nini kiliendelea hadi kesho nilipozindukia hospital na mpenzi wangu akiwa pembeni yangu. Nilianza tena kulia kwa nguvu nikisema atoke ndani na yeye akaanza kuniomba msamaha, baadae alikuja nesi na kumtaka aondoke. Nesi alilirudi kuniuliza ni nani maana yeye ndiye alikuleta jana usiku ukiwa umezimia tena analia na kujilaumu, alisema wewe ni mumewe ila amekukosea na sasa hajui umejudhuru nini, tulidhani umekunwa sumu lakini vipimo vikapinga, amelala hapa amekaa analia. Nikamwambia aende zake yeye ndo kasababisha niko hivi tena sita kumwona.
Jioni yake niliruhusiwa kwenda nyumbani, akaja kama kawaida yake nikasema mimi naona niende kujisalimisha kwa yule baba kuwa ananing'ang'ania, akaondoka kwenda kwao analia. Alirudi kesho yake akaniambia anipe faini kama mwanzo ili nimsamehe maana ile pesanaliyonipa mwazo niliila wala sikuama nkamwambia ilikuwa kama faini, akaniuliza nataka kiasi gani nikasema sitaki pesa maana kilichobaki ni kuuawa mimi hivyo hakuna kiasi kinachoweza kulipa maisha yangu. Ulikuwa ndio mwisho wa kuonana na yule dada hadi kipindi cha miezi miwili nilipokuwa naumwa akaja kuniona akasema ''ona sasa unaugua peke yako ndani wakati mimi nipo na nina kupenda nipe nafasi ya mwisho Jose mimi nilishaachana na yule baba kwanza nilikuwa simtaki ilanbaada ya kipigo kile nilimwambia mama akaenda kumshtaki kazini kwake na akaambiwa kunitibu na kuacha kunisumbua.
Kwa kuwa mimi pia nilikuwa nimemmisi niliona nitumie wakati huo kujifanya nimemkubalia maana alisema nitaje faini kipindi kile, nikamwambia nitakukubalia lakini kwa masharti, akasema sema chochote mimi nitafanya, nikasema unaweza kunipa laki mbili? Akasema ndiyo kama kweli utanisamehe nikasema sawa, yeye alikuwa anamiliki akaunti ya CRDB ambayo alifunguliwa na mama yake ili kuwekewa fedha ya mirathi ya baba yake alipokufa maana waligawana mafao ya baba yao japo mimi sikuwa najua sana kuhusu kiasi na matumizi ya pesa hiyo.
Pamoja na kwamba nilikubali na siku hiyo tukafanya lakini moyo ulishajenga chuki na kusema sasa nianze kutafuta mtu mwaminifu wa kuoa na sasa nilipanga nirudi nyumbani kabisa kijijini. Nikiwa nimeenda kwenye likizo nyumbani kwa bibi nilikutana na msichana mmoja ambaye eti na yeye alikuja kumsalia bibi maana aliwahi kukaa kwake akiwa mdogo, nikamuliza uliza maswali kama kawaida yetu wanaume akaniambia anaishi geita anafanya kazi ya ualimu ila kwao ni jirani tu na hapo kijijini kwetu akaniachia namba yake wote tukaondoka. Nikiwa nimesharudi mwanza nikampigia simu nikamuuliza kama anamchumba akasema ndio anaye na wanakaribia kuoana, kwa kuwa tunajua kwa baadhi ya wasichana hii huwa swaga nikamwambia mimi siitaji kukuchezea bali nahitaji ndoa na wewe akasema umechelewa.
Nikaamua kukausha maana bado nilikuwa bado na huyu wa mwanza japo kwa kishingo upande. Siku moja bibi alikuja kunitembelea mwanza, ilikiwa baada ya mimi kuugua kwa kipindi kirefu na kulazwa, alipokuja aliniuliza kwanini naishi peke yangu kwa nini nisioe mimi nikamwambia bado sijampata wa kumwoa, akaniuliza na jesca je? Nilishtuka na kushangaa sana maana jesca huyu ni yule niliyekutana naye kwake na sikuwahi kumwambia kwamba nilimwambia habari za ndoa na wala hakuona tunapeana namba za simu wala tunaongea maana mimi mambo yale nilifanya kwa siri kwa kumuogopa yeye.
Nikatabasamu nikamwambia huyo anaye wakwake kwanini umesema huyo? Akasema yeye yule binti amekaa naye kwa miaka miwili alipokuwa anasoma, anatabia nzuri sana na anaakili sana tena mtu wa nyumbani ambaye kabila moja, kwa sasa alisema anafanya kazi geita ya ualimu wa watoto wadogo kwakuwa alisoma chuo cha malezi sengerema. Akampasifa nyingi sana na akasema mimi kazi yangu ni kumwambia yeye mambo mengine atamaliza.
Akasema si vizuri kukaa peke yangu ndani ni bora nioe ili nipate msaidizi atayeniuguza hata nikizimia tena, maana safari hii nilikuwa nimezimia tena nikakutwa na rafiki yangu saa 2 baada ya kunipitia twende kazini akaona siamki, aliita gari la kazini baada ya kupata taarifa wakanipeleka hospitali, mara hii nilikuwa naumwa vidonda vya tumbo. Nikamwambia nitalifanyia kazi lakini akiwepo bado nikampigia simu yule dada nikajifanya namsalimia na bibi yetu pia anamsalimia yupo mwanza amekuja kuniona nilkuwa naumwa, nikampa bibi simu wakasalimiana.
Baada ya bibi kuondoka nikaamua kulifanyia kazi suala lake japo nilishapewa majibu awali, nilimpigia nikajifanya namkumbisha ombi langu, akaniuliza hivi sisi tunaweza kuoana sio kwamba tuna undugu? Mimi nikamwambia (huku nilijua dili limetiki) amuulize bibi kwa ushahidi, akasema atamuuliza. Baada siku yaani kesho yake nikampigia tena kumuuliza imekuwaje, kwa sauti ya bashasha akaniambia hakuna shida, basi tukaanza kuzungumzia habari za ndoa.
Wakati huo nikuwa bado ninaye huyu wa mwanza ila baada ya kumaliza chuo alienda naye sengerema kupiga tempo katika hospitali ya wilaya ndo akanipa wa kunogesha mipango na huyu wa geita. Ilifika hatua nikamwambia jesca unaonaje uje mwanza tuanze maisha mimi nitaenda kwenu kujitambulisha, alikuja na mimi nikapiga safari kwenda kujitambulisha kwao wakanipagia mahali na nikalipa na tukaanza process za ndoa.
Kama mwezi mmoja tangu aje yule wa Geita nikampigia simu na kumwambia Kuwa mimi sasa nimeachana naye na nitaka kuoa, alikasirika akasema nisidanganye yeye ndo mke wangu, niliamua pia kumwadithia jesca kuwa nilikuwa na mtu ila alinitendea mambo ambayo niliona hayaweza kutudumisha katika ndoa nimeachana naye na kuamua kumuoa yeye ila hakukubali vizuri hivyo anaweza kuja wakati wowote hapo nyumbani kwani alipazoea na anajua kila kitu ndani humo na hasa akijua nataka kuoa.
Kama nilijua siku akapiga simu anakuja kwake yaani kwangu nikamwambia kuna mtu na simuitaji aje nilishamwambia, sasa ikabidi nimpe taarifa huyu niliye naye akaenda kwa jirani na mimi nikafunga nyumba nikakaa nje. alipo kuja alikuja na Nanasi na samaki kama alivyozoea alipo kuwa akija kuniona akanikuta nje nikmwambia haruhusiwi kuingia ndani akasema yeye humo ni kwake. Majirani wakawa wengi wakitaka kuona nini kitaendelea pale maana jesca wanamjua na habari za ndoa na huyu wanamtambua maana alikuwa anakuja mara kwa mara pale nyumbani, hasa walitaka kujua huyu wa ndoa itakuwaje atakapojua ukweli huu. Niliamua kuondoka kumwacha pale mlangoni na funguo nikaondoka nazo.
Kumbe baada ya mimi kuondoka aliomba sijui nini alichotumia kwa jirani akavunja mlango na kuingia ndani, akavunja kila kitu kinachovunjika, akachana kila kitu kinacho chanika na akaamua kubeba vitu alivyohisi avichukue vikiwemo vyeti vyangu na barua za muhimu za kazi. Kuna akaniambia huku mambo si safi kwa simu nikama huyu msichana amebeba vitu vyako anaingiza kwenye gari, nikatoka mbio kufika ameshaondoka, kuangalia ndani ni kama pamepigwa radi, nikachukua teksi kianza kumfuatilia kwao. Kumbe aliita gari akabeba mikoba ya mke wangu na vitu vingi tu.
Nilipofika kwao hapakuwa na mtu ila yeye akajifungia chumbani kwa mama yake nikamwambia fungua unipe vitu vyangua akakataa. Nikavunja na mimi kitasa kama alivyovunja cha kwangu ila ukatoka mkono wa upande wangu ila yeye akabaki ndani, sebuleni kulikuwa na kabati la vyombo na mimi nikapasua kila kitu humo. Akapiga simu kwa majirani amevamiwa wakaja na mwenyekiti wakasema ni uvamizi wakataka wanikamate kama mwizi ila wengine wakasema ni ishu za mapenzi wakamwita mama yake, alipofika akaamuliwa atoke ndani huko chumbani aje tuyarudie.
Mimi nikaeleza kila kitu maana mama yake alijua kila kilichokuwa kinaendelea kati yetu pamoja na ule ugomvi na fumanizi zile mimi nikamwambia kwa kigezo kile mimi simwitaji tena. Mama yake akasema hata kama hayo hayamuhusu mimi nimemfanyia dharau sana kupasua vyombo vyake nivilipe, nikasema kama nalipa hivi na yeye akalipe vya kwangu. Baadae mama yake akamwamuru anipe kila kitu alichotoa kwangu na niondoke tukielewana yeye mama yake ataninunulia kila kilichovunjika.
Nikaondoka nikijua huo ndo mwisho kurudi nyumbani nikamkuta mke wangu tu bi amekaa ameshafanya usafi nikamsimulia kilichoendelea akanipa pole maana alikuwa anajua kila stori licha ya watu kudhani kuwa itakuwa skendo tena kwake tuliongea mengi ikawa siku ambayo alinieleza kwanini aliachana na aliyekuwa ameniambia kuwa ni mchumba wake.
Eti alimpenda sana lakini siku moja alimtenda sana tena kwenye kundi la watu alipomkuta na msichana mwingine akamwambia kuwa yeye hakuwa taipu yake ndio maana akamuulizia bibi kuhusu mimi niloshaoa ili anikubalie. Nikajua sababu ya bibi kujua siri ambazo mimi sikumwambia sasa tukawa tumekutana watu ambao tulitendwa huko tutokako sasa tumeoana tuna mwaka wa tatu katika ndoa na mungu katujalia watoto wawili mapacha.
Kilichonifanya kuandika stori hii kuwa mke wangu anaonekana alimpenda sana huyo aliyemtenda kiasi cha siku moja kuomba kwenda kwao ambako ndiko kwao na alaiyekuwa mchumba wake na ikadhibitika kuwa kuwa alienda kulala kwake siku moja maana yule jamaa hajaoa na alimfuata kwao na alikwenda na watoto nilipomwambia mimi nakuacha kwa hili ulilonitendea eti ananiambia ukweli ''samahani mume wangu nikwambie ukweli leo nimetoka kwa mchungaji ameniombea na ninashida kubwa sana tangu umenooa huwa namuwazia sana yule mpenzi wangu wa na kuna siku huwa naota anafanya mapenzi na mimi na huwa nakuta kama kweli nimefanya, ndio maana mara nyingi sitaki kufanya mapenzi na wewe na hata kama nikijilazimisha naumia kweli tena mchungaji amesema nikwambie ukweli na nikupeleke uombewe na wewe eti kuna roho haitaki ndoa yetu, mimi nilisikia nimemisi sana mpenzi huyo nikaamua kwenda nyumbani kwa kupanga safari ya uongo na nilipofika nyumbani niliona nachelewa kwenda kwake, alikuja akanipeleka kwake nikalala na tulifanya akaniambia eti na hawa watoto ni wakwake, wakati huo nilikuwa sijui nini kilikuwa kichwani maana nilikuwa kama sijitambui, ila sasa mme wangu unisamehe nimetubu na mchungaji amesema kila kitu kitaisha.
ADHABU HII NINAYOPATA LEO NI KWASABABU YA HISTORIA NYUMA? JE NINI NIFANYE? KILA SWALI UNALOJIULIZA SASA NA MIMI NAJIULIZA HILOHILO ILA MAJIBU SINA.