Alistahili kutimuliwa kazi miaka mingi iliyopita lakini unamjua DHAIFU mpaka Bunge la CCM limshinikize ndio afukuze kazi watu. Kazi ilishamshinda huyu siku nyingi sana na kuendelea kuwepo kwake ndio kumelichafua kabisa jeshi hilo na sasa kuonekana ni genge la wahuni, watesaji, wezi, majambazi na wauaji pia halina heshima hata kidogo katika kila kona ya nchi yetu. Kwa kifupi amechangia mno jeshi hilo kupoteza heshima yake nchini.
BAK,
Sidhani kama umemaanisha ambacho umekiandika hapo!
Katika ma-IGP walio tenda kazi nzuri kwenye nyanja ya usalama wa raia na mali zao ni huyu IGP ndiye anae ibuka kidedea.
Huwezi kupima tu Tanzania ya leo katika mambo ya kiuhalifu na ile ya enzi za Mkapa na Mwinyi?
Leo hii ujambazi na unyang'anyi ni kama hadithi vile, matukio ya aina hii ni ya kutafuta na tochi, unadhani hali hii imetokana na nini?
Hayo matukio uliyo eleza ni kweli yametokea wakati wake, ila yakupaswa uelewe kuwa uhalifu unazidi kukua, huwezi kufananisha mbinu za uhalifu za mwaka 1947 na za leo, hivyo jitihada ni kubwa za kupambana na matukio ya aina hiyo ndio maana hutokea mara chache chache.
Propaganda ambazo hazina ukweli wowote ndio kazi zenu nyie. Kama huoni wala husikii jinsi jeshi la polisi lilivyopoteza heshima yake hata ashuke Mungu kukwambia hivyo huwezi kumuamini. Mie nimemaliza.
BAK,
Si sahihi kuhukumu binadamu mwenzako kwa kutazama mabaya au madhaifu yake tu, huu si uungwana. Ni vyema pia tukatazama na mazuri yake ili tuweze kutoa hitimisho lililo sahihi.
Binafsi sidhani kama yupo mwanaadamu alie mwema na mkamilifu, ni ukweli usio pingika hata hao unao wakubali wana mapungufu yao, sasa iweje iwe ngumu kwako kukubali kuwa IGP Mwema nae anayo mazuri yake pia na hata mabaya?
BAK,
Si sahihi kuhukumu binadamu mwenzako kwa kutazama mabaya au madhaifu yake tu, huu si uungwana. Ni vyema pia tukatazama na mazuri yake ili tuweze kutoa hitimisho lililo sahihi.
Binafsi sidhani kama yupo mwanaadamu alie mwema na mkamilifu, ni ukweli usio pingika hata hao unao wakubali wana mapungufu yao, sasa iweje iwe ngumu kwako kukubali kuwa IGP Mwema nae anayo mazuri yake pia na hata mabaya?
BAK,
Sidhani kama umemaanisha ambacho umekiandika hapo!
Katika ma-IGP walio tenda kazi nzuri kwenye nyanja ya usalama wa raia na mali zao ni huyu IGP ndiye anae ibuka kidedea.
Huwezi kupima tu Tanzania ya leo katika mambo ya kiuhalifu na ile ya enzi za Mkapa na Mwinyi?
Leo hii ujambazi na unyang'anyi ni kama hadithi vile, matukio ya aina hii ni ya kutafuta na tochi, unadhani hali hii imetokana na nini?
Hayo matukio uliyo eleza ni kweli yametokea wakati wake, ila yakupaswa uelewe kuwa uhalifu unazidi kukua, huwezi kufananisha mbinu za uhalifu za mwaka 1947 na za leo, hivyo jitihada ni kubwa za kupambana na matukio ya aina hiyo ndio maana hutokea mara chache chache.
lol! Msema ukweli siku zote ni mpenzi wa Mungu. Na hakuna mahali nilipoandika kwamba kuna Mwanadamu asiye na mapungufu, lakini kama utendaji wa kiongozi katika chombo/taasisi ya Serikali ni mbovu basi hakuna sababu yoyote ya kumung'unya na kumremba ili kuonyesha kwamba alifanya kazi nzuri. Jeshi la polisi limeoza sasa hivi haliaminiki tena inabidi kufumuliwa lote ili kulijenga upya lakini DHAIFU hana ubavu huo. Na katika miaka hii miwili kati ya sasa na 2015 jeshi hili ndio litazidi kujichafua kwa kiwango cha kutisha.