Mwelekeo wa TZ yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwelekeo wa TZ yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shine, Sep 14, 2011.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wakuu hebu tuweke mwelekeo wa nchi yetu mpaka ifikapo mwaka 2015 jk atapoachia nchi tutakua kwenye hali gani kiuchumi na kisiasa?

  Nawakilisha
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tutakuwa dhoofu mbaya! nchi haina utawala wa sheria, sijawahi ona kwa kweli
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mukuu wangu,
  Inji yetu inaeleke kuzuri sana,
  Kwa kasi hii ya kupewa "maisha bora" itapelekea Wananji yote kujivua magamba.

  Tatizo la umeme "litakuwa ni historia"...usinielewe vibaya hapa, mimi nakariri tu maneno ya wakulu wetu...mizungu inasema, history repeats itself!
  Natumai umeelewa vizuri sasa,muelekeo wa nchi yetu, nchi tajiri ya rasilimali na mali ghafi lakini ina umasikini wa kutisha.

  Tusisahau kuna katiba mpya inakuja...lakini hakutakuwa na kipya katika katiba hiyo...hali hii itapelekea mipasho kuzidi bungeni na wananchi watazidi kulalamika.... in the meantime, jeshi letu linastock upya yale maghala ya mabomu, na polisi wetu watapata risasi zaidi ili waendelee na kazi yao ya "kulinda" maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani.

  Vyama vya upinzani badala ya kuungana au kushirikiana, vitaendeleza vita vya panzi, wataendelea kugawa kura za upinzani na hivyo kuwazawadia "wenye magamba" ushindi ili waendelee kutekeleza kazi waliyotumwa na wananchi; kutembeza bakuli na kuwaletea "maisha bora" na vibajaji kwa wagonjwa, mashangingi kwa wabunge na mawaziri.

  Uchumi tumeshaambiwa kuwa unapaa, Lowasa alisema hivyo, na hapa pia wanasema hivyo https://www.jamiiforums.com/international-forum/172576-eac-economies-take-a-knock-tanzania-still-looking-good.html

  kwa hiyo, muelekeo wa nchi yetu kama unavaa miwani nyeusi au kama unatumia darubini utaona kuwa muelekeo ni mzuri.

  Keep the hope....wenzetu wanachukua "vijisenti" vyao mapema.
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  daah mkuu sitaki ku imagin mana ka hadi ssa tu tupo exhausted sijui itakuaje
   
 5. reuby

  reuby Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama matatizo ya ufisadi hayatashughulikiwa kwa dhati, kukatika umeme kusikokoma, utawala bora (haki itendeke katika maamuzi kv uchaguzi, usalama wa raia..) kama havitashughulikiwa kwa dhati; na wananchi wasipofanya kazi kwa bidii zaidi tutarudia maisha ya karne ya 18 ifikapo 2015. tuache ubabaishaiji tushughulkie mambo makubwa ya kuleta maendeleo km kilimo cha kisasa na miradi ya kuzalisha umeme wa kutosha badala ya kukodisha mitambo ili kupata 10-100%
   
 6. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wala msitie shaka, nchi inakwenda vyema. Maisha bora yanaendelea kuratibiwa, miradi mikubwa ya umeme wa kulisha nchi yote inaendelea kwa speed ya mwanga mpaka tutauza nchi jirani. Kwa sasa tunatengeneza pesa kwanza tukishamaliza kuuza rasilimani zote tutakuwa na pesa nyingi hivyo elimu, afya vitakuwa bure na itabaki historia kwa watanzania. Kumbukeni sisi ni ndugu hivyo muungano utadumu kwa miaka alfu ijayo haya matatizo madogo ya muungano 2016 yatakuwa hadithi, msijali tuendelee "KUMUOMBA MUNGU" ashuke atutatulie matatizo yaliyo ndani ya uwezo wetu, tuendelee kuomba kwa bidii hata machozi ya damu yatoke maana ndiyo sadaka ifaayo...
   
Loading...