Mwelekeo wa TZ yetu

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Wakuu hebu tuweke mwelekeo wa nchi yetu mpaka ifikapo mwaka 2015 jk atapoachia nchi tutakua kwenye hali gani kiuchumi na kisiasa?

Nawakilisha
 
Mukuu wangu,
Inji yetu inaeleke kuzuri sana,
Kwa kasi hii ya kupewa "maisha bora" itapelekea Wananji yote kujivua magamba.

Tatizo la umeme "litakuwa ni historia"...usinielewe vibaya hapa, mimi nakariri tu maneno ya wakulu wetu...mizungu inasema, history repeats itself!
Natumai umeelewa vizuri sasa,muelekeo wa nchi yetu, nchi tajiri ya rasilimali na mali ghafi lakini ina umasikini wa kutisha.

Tusisahau kuna katiba mpya inakuja...lakini hakutakuwa na kipya katika katiba hiyo...hali hii itapelekea mipasho kuzidi bungeni na wananchi watazidi kulalamika.... in the meantime, jeshi letu linastock upya yale maghala ya mabomu, na polisi wetu watapata risasi zaidi ili waendelee na kazi yao ya "kulinda" maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani.

Vyama vya upinzani badala ya kuungana au kushirikiana, vitaendeleza vita vya panzi, wataendelea kugawa kura za upinzani na hivyo kuwazawadia "wenye magamba" ushindi ili waendelee kutekeleza kazi waliyotumwa na wananchi; kutembeza bakuli na kuwaletea "maisha bora" na vibajaji kwa wagonjwa, mashangingi kwa wabunge na mawaziri.

Uchumi tumeshaambiwa kuwa unapaa, Lowasa alisema hivyo, na hapa pia wanasema hivyo https://www.jamiiforums.com/interna...take-a-knock-tanzania-still-looking-good.html

kwa hiyo, muelekeo wa nchi yetu kama unavaa miwani nyeusi au kama unatumia darubini utaona kuwa muelekeo ni mzuri.

Keep the hope....wenzetu wanachukua "vijisenti" vyao mapema.
 
kama matatizo ya ufisadi hayatashughulikiwa kwa dhati, kukatika umeme kusikokoma, utawala bora (haki itendeke katika maamuzi kv uchaguzi, usalama wa raia..) kama havitashughulikiwa kwa dhati; na wananchi wasipofanya kazi kwa bidii zaidi tutarudia maisha ya karne ya 18 ifikapo 2015. tuache ubabaishaiji tushughulkie mambo makubwa ya kuleta maendeleo km kilimo cha kisasa na miradi ya kuzalisha umeme wa kutosha badala ya kukodisha mitambo ili kupata 10-100%
 
Wala msitie shaka, nchi inakwenda vyema. Maisha bora yanaendelea kuratibiwa, miradi mikubwa ya umeme wa kulisha nchi yote inaendelea kwa speed ya mwanga mpaka tutauza nchi jirani. Kwa sasa tunatengeneza pesa kwanza tukishamaliza kuuza rasilimani zote tutakuwa na pesa nyingi hivyo elimu, afya vitakuwa bure na itabaki historia kwa watanzania. Kumbukeni sisi ni ndugu hivyo muungano utadumu kwa miaka alfu ijayo haya matatizo madogo ya muungano 2016 yatakuwa hadithi, msijali tuendelee "KUMUOMBA MUNGU" ashuke atutatulie matatizo yaliyo ndani ya uwezo wetu, tuendelee kuomba kwa bidii hata machozi ya damu yatoke maana ndiyo sadaka ifaayo...
 
Back
Top Bottom