JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,270
BENKI YA DUNIA imeitabiria mema nchi yetu ya Tanzania. Imepongeza hatua za Rais Magufuli katika Ukusanyaji Kodi na vita dhidi ya Rushwa. Hata hivyo imeitaka serikali kuwekeza nguvu nyingi zaidi kwenye rasilimali watu na Miundombinu. Pia imeishauri serikali kuzitumia sekta binafsi kushirikiana katika kukuza uchumi kwa njia salama.
Je, kwa mwendo huu wa sasa, Tanzania itatoboa?!
Ukiwa kama mwananchi wa kawaida, ni hatua zipi zaidi unatamani zichukuliwe kwa haraka na serikali ili kuboresha maisha na kupunguza hali ya umaskini?
Maoni yako ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu. Nchi ya Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe.
===================
Hatua za kukwamua uchumi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk John Magufuli zimeanza kuzaa matunda ikiwemo ongezeko la makusanyo ya mapato ya kila mwezi. Taarifa ya Benki ya dunia inaeleza.
Benki ya Dunia katika ripoti yake ya nane iliyotolewa tarehe 20 Mei 2016 kuhusu uchumi wa Tanzania imetaja hatua hizo kuwa ni pamoja na udhibiti wa matumizi ya fedha na rushwa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mkazi wa benki hiyo nchini Tanzania Bella Bird amesema mafanikio hayo yatakuwa endelevu iwapo serikali itawekeza zaidi kwenye miundombinu na rasilimali watu kama njia ya kuweka mazingira bora ili sekta binafsi ichanue zaidi na kufungua ajira.
Amesema hatua hiyo siyo tu itapunguza umaskini kwa mujibu wa malengo ya maendeleo endelevu, bali pia itaendana na vipaumbele vya serikali ya sasa na azma yake ya kufanikisha dira ya 2025.
Ripoti inagusia pia ubia kati ya serikali na sekta binafsi, PPP ikisema ni hatua njema lakini mipango madhubuti inatakiwa ili kuondokana na tabia ya utendaji kazi kwa mazoea katika ubunifu na utekelezaji wa PPP (Public Private Partnership).
Katika hatua nyingine, Benki ya Dunia inasifu juhudi za Rais John Magufuli katika ukusanyaji wa kodi, kupambana na ufisadi na kuondoa uzembe, inasema katika ripoti hiyo kuwa ili ukuaji huo wa uchumi uendane na ustawi wa jamii, Serikali inatakiwa kufanya mambo ya msingi ambayo yatasaidia kuimarisha ubia baina yake na sekta binafsi (PPP) kugharamia miradi mikubwa ya miundombinu na huduma kwa jamii.
Ripoti hiyo inayoitwa “The Road Less Travelled: Unleashing Public Private Partnership in Tanzania” ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alisema Serikali inakubaliana na ripoti hiyo na mapendekezo yaliyomo na kwamba inaandaa mazingira mazuri ya kuhakikisha sekta binafsi inashirikishwa kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kuinua hali ya maisha ya watu.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa Tanzania bado inasuasua katika maendeleo ya miundombinu na huduma za kijamii kutokana na kukosekana kwa fedha za kutosha, hivyo PPP itasaidia kupunguza mwanya wa kibajeti kugharamia masuala hayo.
Benki ya Dunia imesema kuwa Tanzania ina mifumo na uzoefu wa PPP lakini kuna mengi yanatakiwa kufanyika ikiwamo kutekeleza mambo takribani sita ambayo yataimarisha ushirika huo yakiwemo;
1. Kuchagua kwa makini aina ya miradi ya kushirikiana kwa mujibu wa mahitaji ya utekelezaji kifedha na ambayo yana mvuto kwa sekta binafsi..
2. Kuanzisha mfumo imara wa kitaasisi na kiudhibiti utakaosaidia kuimarisha utekelezaji wa miradi ya PPP..
3. Serikali kujiimarisha katika njia zitakazosaidia kuimarisha taasisi za kusimamia ubia na sekta binafsi ikiwamo kuanzisha kituo maalumu cha PPP kinachotakiwa kiendeshwe na mtendaji mkuu mwenye uzoefu na kadhalika.
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda alisema Serikali inajitahidi kuongeza mapato kupitia kodi na matokeo ya awali mwaka huu yanaonyesha hali ni nzuri.
SOMA RIPOTI NZIMA KWENYE PDF FILE (ATTACHED)