Mwelekeo wa cuf na chadema kisiasa tz

MKILINDI

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
549
549
Mgogoro ndani ya chama na kushuka kwa cuf katika chaguzi mbili bara na visiwaani na kupanda kwa chadema katika chaguzi zote,
inaweza ikawa ni mwelekeo mbaya kwa cuf na kufifisha matumaini yao kisiasa nchini tanzania, je pia inaweza kuwa ni nyota njema kwa chadema kujitanua hadi visiwani?
 
Ha ha ha tatizo lenu chadema hamjui adui wenu nani? naona mnahangaika na CUF kuliko CCM.

Hakuna ukweli hapo, CUF ndio wanahangaika na CDM kuliko CCM, pia CCM wanahangaika zaidi na CDM kuliko CUF.
Na nnajua kuwa wajua kuwa CUF na CCM wanaunda umoja ktk uwili.
 
Hakuna ukweli hapo, CUF ndio wanahangaika na CDM kuliko CCM, pia CCM wanahangaika zaidi na CDM kuliko CUF.
Na nnajua kuwa wajua kuwa CUF na CCM wanaunda umoja ktk uwili.

Kwanza kabisa hii thread na zingine nyingi ni uthibitsho mdogo wa jinsi chadema inavyohangaika na CUF

Uthibitisho mkubwa ni jinsi chadema wanavyoichafua CUF kwa mambo ya kikatiba (kushiriki serikalini huko zenj), kama vile chadema wengesusa ikiwa wangepata wabunge zenj ambayo si kweli..

Uthibitisho mkubwa mwingine ni jinsi chadema walivyofurhaia matokeo ya uzini, igunga etc.. kwa kushika na mbili..na siyo kuwashinda CCM..

Chadema wanaiogopa CUF kuliko hata CCM..
 
Fitina za Kuifisidi Jamhuri ya Zanzibar na
Watu Wake ! Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa –
Zanzibar. TUMEJIFUNGIA na WAZEE na tumekaa
tukanong’ona ! Kwanza Serikali ya
Tanganyika walituletea sakata la
Hamad Rashid, na watu wakalivamia.
Ikawa mwezi na nusu Wazanzibari
hatujadili tena kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae likaja suala
la kuongezwa kwa mipaka ya bahari
kuu la Tibaijuka na Shamhuna. Akina
Bilali, Samia Suluhu na wenziwao
tutajuwana nao BAADA ya kuiweka
mezani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Pia kwa makusudi, wamelizusha suala
la kufutwa kwa mitihani ya kidato cha
nne. Tunalopaswa kufanya ni
kuhakikisha Waziri wa Elimu wa
Zanzibar, anatoa ripoti juu ya kufutwa
kwa mitihani ya kidato cha nne, pamoja na kutueleza kwa kina mfumo wa
mzima wa elimu duni uliopo Zanzibar. Hivi sasa limezuka suala la uchaguzi
mdogo wa Uzini na Chadema
kuchukua nafasi ya pili baada ya
kuwanunua wapiga kura mamluki.
Tujue kwamba, Tanganyika iliyojificha
ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitosita na haitolala
mpaka tuifuate MILA yao ya kuijadili
Katiba ya Muungano KWANZA bila ya
kuirudisha Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar. Tukiyafuata waliyoyakusudia
na wanayoyapanga, tutakuwa tumetoka nje ya kuidai HAKI yetu ya
kimsingi ya kuirudisha Jamhuri ya Watu
wa Zanzibar. Hamad Rashid, Bilali,
kufutwa kwa mitihani na uchaguzi wa
Uzini, zote hizi ni mbinu, ujanja na fitina
za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar. Kamwe hatutaicheza ngoma
yao ! Zamani ilikuwa ni UHAINI kujadili
Muungano. Juzi tu, wajanja hawa hawa
kwa kutaka kuiendeleza falsafa hiyo ya
Unyerere, wamepitisha sheria Bungeni
ya kumchukulia hatua yo yote
atakaejadili lo lote ambalo liko nje ya hadudi rejea za rasimu ya Katiba. Kwa
mantiki hiyo, yo yote atakaetoa NGUVU
ya HOJA ya kuirudisha Jamhuri ya Watu
wa Zanzibar KWANZA na/au Muungano
wa Mkataba na kuukataa Muungano
wa Katiba wakati wa mchakato wa Katiba utakapokuja, atachukuliwa
hatua za kisheria kwa kufikishwa
Mahakamani, ili wengine waogope
kuendelea kuidai Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar, na badala yake iendelezwe
HOJA ya NGUVU na ya udikteta inayotakiwa ya kujadili Katiba
iliyosimama juu ya misingi ya KIKOLONI
inayopinga uwepo wa Jamhuri ya Watu
wa Zanzibar ambayo ndio mbia mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hizo zinazodaiwa kuwa ni hati za
Muungano baina ya Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar, zilijengwa juu ya taswira ya
Muungano baina ya Uingereza na
Ireland ya Kaskazini ya wakati ule, pale Ireland ya Kaskazini ilipokuwa ni
koloni la Uingereza. Kudhihirisha njama za wajanja hawa,
juzi tarehe 12 Februari 2012,
Halmashauri Kuu ya CCM kwa
makusudi, imeifanyia marekebisho
Katiba ya CCM yenye lengo la
kuwaangusha na kuwadhibiti - MASHUJAA wa MARIDHIANO yetu yaliyo
HALALI Kikatiba, na badala yake,
kuwabeba VIBARAKA ambao
wameonesha wako tayari kuiuza
Zanzibar na Wazanzibari kwa UTASHI
wa UBINAFSI unaoongozwa na uroho na ulafi wa madaraka. WAZANZIBARI po pote tulipo duniani
TUMESHAAMKA na KUSIMAMA KIDETE
kwa kuelewa kuwa, yote haya ni
katika mbinu chafu, hadaa, ghilba na
fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU
la kuipigania na kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tusikubali, na kwa
hakika HATUTAKUBALI kuondolewa
kwenye njia na lengo letu hilo HALALI
la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar yenye hadhi yake kitaifa na
kimataifa; maana sisi wananchi wa Zanzibar, tuna mamlaka na haki ya
Kikatiba katika kuendesha nchi yetu
kama Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo
la 2010, inavyoeleza kwenye Sura ya
Pili: (a) “Mamlaka ya kuendesha nchi ni
ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana
na Katiba utatoka kwa wananchi
wenyewe”. Jamhuri ya Watu wa Zanzibar KWANZA!
 
Back
Top Bottom