Mwelekeo wa chama cha ACT Wazalendo katika mwaka 2018

Mwelekeo wa chama cha ACT Wazalendo katika mwaka 2018

Chama chetu kina demokrasia pana sana
I believe your words Honourable but democracy has to be seen within the party. And not telling us here Sir. It is just an advice. That will be your game card.
 
Keep It up mheshimiwa watu wamechoka na siasa za uchochezi na vurugu. Kwa wapinzani wa kweli wanaoangalia mbadala wa CCM, ACT wanaitazama kwa umakini. Na hii ni turufu yako. Ila nakuomba uangalie sana uhuru wa mawazo mbadala ndani ya chama chako. Usije kuwa kama chama ulichotoka .
umesahau ana hulka ya fikra kinzani na huziamini na aliitwa mchochezi,/msaliti. Nadhani ushauri wako aausoma, ila kuwa submissivsijui
 
Wanikamate kunishtaki mahakamani basi. Mbona ni jambo rahisi sana
hahahaha watakukamata vipi wakati kila wakijaribu wanakutana na ziwa tanganyika?
 
Mwelekeo wa Chama cha ACT Wazalendo Katika mwaka 2018

1. Kupigania Haki za Wafanyakazi kupitia Vyama vya Wafanyakazi na haki za raia kupitia vyama vya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara wadogo kwa kujenga ushirikiano wa kipambano na Jumuiya hizo za Wananchi.

2. Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi nchini kwa kufanya vikao vya Mara kwa Mara na Viongozi wa Vyama vingine na kufanya shughuli za pamoja.

3. Kuendelea kusemea Haki za Kijamii kama Elimu na Afya na kuongeza juhudi za kupigania Haki ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi wote hasa Wakulima kwa kushawishi kuanzisha Fao la Bei katika mfumo wa Hifadhi ya Jamii nchini na Bima ya Afya kwa kila Mtanzania.

4. Kuendelea kushawishi Sera za Uchumi zinazomkomboa mwananchi wa kawaida kwa kukosoa Sera zinazodidimiza Maendeleo ya Uchumi na kupendekeza Sera mbadala.

5. Kujikita Katika Uimarishaji wa Chama kwenye ngazi zote na kufanya Mkutano Mkuu wa Chama Mwezi Agosti Jijini Mbeya sambamba na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia 2018.

Imetolewa na

Kamati Kuu ya Chama Cha ACT Wazalendo
Januari, 2018
Hivi ile kamati iliyoundwa na spika ndugai kuchunza makampuni ya mafuta na gesi walifikia wapi. Maana walitakiwa kutoa report dec au jan
 
umesahau ana hulka ya fikra kinzani na huziamini na aliitwa mchochezi,/msaliti. Nadhani ushauri wako aausoma, ila kuwa submissivsijui
Nashukuru mkuu. Mimi nimetoa maoni yangu kama mtanzania anayependa upinzani imara na si huu uhuni tuluonao sasa
 
Mh. Zitto una uwezo mzuri wa kujenga hoja, kuchambua pia una nyoto ya kiuongozi, inasikitisha sana kuona hadi mwanasiasa wa aina yako unafanya siasa za propaganda na kupotosha. Kila nikikumbuka upotoshaji wa ndege ya Dreamliner, upotoshaji wa tozo za miamala ya kutuma fedha kwenye simu na kadhalika nazidi kukushangaa tu. Stuka mapema, huko unapoenda si sahihi na si level yako, heshima yako ni kubwa sana usikubali kuishusha kwa umaarufu wa muda mfupi.
 
Alipotosha kitu gani kwenye ndege ya dreamliner?
 
Kweli siasa zimepoteza mvuto...Zitto zamani akileta uzi huku ndani ya saa moja page 20 zimefika...leo siku mbili hata page 2 haziishi...siasa bongo ximekufa
Tatizo ni mada.Huu siyo muda wa kuimarisha chama!Ni muda wa kudai haki za msingi za kikatiba, nadhani anapima upepo tu ili aweze kuona kama kuna opportunity ya kupata wanachama... keshapima na kuona!
 
1. Kupigania Haki za Wafanyakazi kupitia Vyama vya Wafanyakazi na haki za raia kupitia vyama vya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara wadogo kwa kujenga ushirikiano wa kipambano na Jumuiya hizo za Wananchi.
Mkuu Zitto Tunashukuru kwa Jitihada zako za kutetea wafanyakazi kipindi cha muswada wa mabadiliko ya mifuko ya hifadhi za jamii.

Kwakuwa Upo Jikoni ,Je fao lipi kwa sasa amao linatolewa? Je ni Fao la kutokuwa na ajira au Fao la kujitoa? Je nikipunguzwa kazi kwa sasa nitapewa fao la kutokuwa na ajira? Kama sio je nitapewa fao la kujitoa?
 
Ni kule kujikita ktk mambo ya akina Kijo Bisimba na kuacha kuangalia mahitaji halisi ya Mtanzania wa kawaida ila ktk machapisho ya chama yanakuwa yako mazuri sana
Unajua sometime hawa waheshimiwa hutingwa. Mkumbushe mahitaji ili akatusemee bungeni.
 
Mwelekeo wa Chama cha ACT Wazalendo Katika mwaka 2018

1. Kupigania Haki za Wafanyakazi kupitia Vyama vya Wafanyakazi na haki za raia kupitia vyama vya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara wadogo kwa kujenga ushirikiano wa kipambano na Jumuiya hizo za Wananchi.

2. Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi nchini kwa kufanya vikao vya Mara kwa Mara na Viongozi wa Vyama vingine na kufanya shughuli za pamoja.

3. Kuendelea kusemea Haki za Kijamii kama Elimu na Afya na kuongeza juhudi za kupigania Haki ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi wote hasa Wakulima kwa kushawishi kuanzisha Fao la Bei katika mfumo wa Hifadhi ya Jamii nchini na Bima ya Afya kwa kila Mtanzania.

4. Kuendelea kushawishi Sera za Uchumi zinazomkomboa mwananchi wa kawaida kwa kukosoa Sera zinazodidimiza Maendeleo ya Uchumi na kupendekeza Sera mbadala.

5. Kujikita Katika Uimarishaji wa Chama kwenye ngazi zote na kufanya Mkutano Mkuu wa Chama Mwezi Agosti Jijini Mbeya sambamba na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia 2018.

Imetolewa na

Kamati Kuu ya Chama Cha ACT Wazalendo
Januari, 2018

Asante ndg. Zitto, hayo maswala yote matano uliyoanisha ni muhimu sana. Lakini, naomba nichangie kidogo hapo kwenye la pili (2) ambalo lingefaa kutanguliwa na la kwanza (1) ambalo litakuwa na dhumuni la kudai katiba mpya au angalau tume huru ya uchaguzi.

Zaidi, vyama vya upinzani inabidi vishirikiane kudai uhuru wa kufanya shughuli zake za kisiasa kwa mujibu wa katiba bila kuogopa vitisho. Nasema bila kuogopa vitisho, kwasababu hata katiba ya sasa imetoa uhuru wa vyama vya siasa (sio CCM tu) kufanya shughuli zake. Lakini, anatokea mtu aliye apa kwa katiba hiyohiyo na kupiga marufuku "wapinzani" wasifanye siasa bila kuwa challenged kwa vitendo (kwa mfano, maandamano na njia nyingine zitakazo fikisha ujumbe sawasawa). Maandiko ya mitandaoni peke yake hayatoshi.

Hii ina maana hata tukipata katiba mpya yenye haki nyingine lukuki, lakini kama hatutokuwa tayari kuziheshimu na kuzipigania haki hizo, basi tutaendelea kunyanyasika tu. Rais yeyeto atakaye patikana huko mbele ya safari anaweza amua kuikanyaga katiba akijua kwamba Watanzania ni waoga.

Tunahitaji vyama vya upinzani/vyama vya siasa vitakavyokuwa tayari kuamsha ujasiri wa Watanzania.
 
Zitto njoo utusaidie kigoma halmashauri kwani mkurugenzi amezuia walimu tusijiunge na chama halali cha walimu 'Chakamwata' bila sababu
 
Mh. ZITO, katika mazingira ya namna hii ya kisiasa, you will achieve nothing! Nadhani vyama vya upinzania mjikite kumaliza gross human rights violations currently taking place in all fields in Tanzania. Short of that, hayo uliyoyaainisha hutaweza kuyafanya. Kama na mikutano ya ndani wanazuia, how do you move forward!

Human right violations!
 
Hiki Chama kinapokea ruzuku kutoka ccm
Huyu muhun wa kuitwa Zito a nasubiria 2020 ale mpunga wa ccm ahaha
 
Ni akina Zitto wametuzalishia kundi la vijana wanaofanya siasa zenye mlengo wa kuchumia matumbo yao kwa "kukopi" njaa na tamaa za watangulizi wao kwa jina la Upinzani.
Nakumbuka huyu mheshimiwa alivyozira uteuzi wa kamati ya bunge isiyokuwa na "ulaji"! Wapinzani wa Tanzania ni wa aina yake kwenye sayari hii!
 
Back
Top Bottom