Mwekezaji wafunga wananchi 15 wa kijiji cha Uleling'ombe wilayani Kilosa


M

Mlyafinono

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
177
Likes
0
Points
0
Age
42
M

Mlyafinono

Senior Member
Joined Apr 6, 2012
177 0 0
Mwekezaji wa kampuni moja inayochimba dhahabu katika kijiji cha Uleling'ombe wilayani Kilosa anadaiwa kuwafunga jela wanachi 15 wa kijiji hicho kwa madai kuwa wamemuibia madini yake.Hata hivyo pamoja na kuwafunga jela wananchi hao inadaiwa hakuna ushahidi ambao unaonyesha wananchi kuhusika na wizi huo.

Mwekezaji huyo amekuwa akilalamikiwa na wananchi wa kijiji hicho kwamba aliwaahidi kuwajengea barabara lakini hadi sasa miaka mitano imepita mwekezaji huyo hajatekeleza ahadi yake. Kutokana na hali hiyo walikusudia kufanya maandamano ya kumpinga mwekezaji huyo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini kijijini hapo.Inadaiwa mwekezaji huyo amewakamata viongozi wa serikali kiasi kwamba hawawezi kuwatetea wananchi
 

Forum statistics

Threads 1,275,228
Members 490,947
Posts 30,536,206