Mwekezaji wa shirika la UDA kukamatwa na kufilisiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwekezaji wa shirika la UDA kukamatwa na kufilisiwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jun 7, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kama una uchungu wa dhati na nchi hii habari hii haitakuwa ndefu kusoma. Imeletwa kwenu na mchungaji Christopher Mtikila kupitia gazeti la uhuru.


  Tumefurahishwa na taarifa za kizalendo kutoka ndani ya TAKUKURU kwamba thamani ya shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) ambalo ni mali ya wananchi siyo shilingi bilioni 11 tu kama ilivyokisiwa awali, bali ni zaidi ya shilingi bilioni 20.

  Kwani shirika la UDA siyo tu lina karakana ya uhandisi ambayo ni moja ya kubwa kuliko zote katika Afrika Mashariki, ikiwa na mashine za kila aina na mitambo ya kila huduma, tulivyopewa na Wajerumani ambao dunia inawaheshimu kwa ubingwa wao katika uhandisi, bali pia shirika lina mali nyingi sana zisizohamishika.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya katiba ya nchi, inayomuwajibisha kila raia kulinda mali asilia ya taifa letu, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na kututaka sisi sote tutunze vizuri mali yote ya mamalaka ya nchi na ya pamoja kama shirika letu la UDA, na kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa letu kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya nchi yao, tunatoa tamko kwamba:

  1. Wahusika wote katika serikali yetu yaani Waziri wa Fedha, Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa tawala za Mikoa na serikali za Mitaa wanapaswa kufikishwa Mahakamani mara moja kwa uharibifu na ubadhirifu wa mali za mabilioni ya fedha za shirika letu la UDA.....saa ya ukombozi ni sasa.

  2. shirika la thamani ya zaidi shilingi bilioni 22 kuuziwa Robert Kisena kwa shilingi bilioni moja tu na robo, bila kutangaza tenda ya wazi kama inavyopasa kisheria na kupata mwekezaji wa kweli mwenye zaidi ya hizo bilioni 22, lakini huyo Robet kisena akalipa shilingi milioni 285 tu na kukabidhiwa mali ya wananchi ya shilingi bilioni 22 ni Ufisadi kichaa! Mauzo yabadilishwe mara moja, na Robert Kisena pamoja na hao watumishi wa umma waliokula naye dili hii wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria ndani ya siku saba! Uharamia huu ndio unaopaswa kumalizwa kwa risasi hadharani! tutahakikisha kuwa sheria ya adhabu hii inatungwa upesi sana, ...saa ya ukombozi ni sasa.

  3. Shirika la UDA ni usafiri wa wananchi katika jiji la Dar es salaam, hivyo mwekezaji anayetakiwa ni wa kuliboresha kwa ajili ya huduma hiyo, siyo wa kuliua! Robert Kisena ameharibu na kukongoloa kabisa mitambo na mashine zote za UDA za mabilioni ya fedha mashine nyingine zimekatwa na kuuzwa kama chuma chakavu 'scrap'! Karakana ya UDA yeye (kisena) anazipangisha kama maghala ya kuweka mtama wa kampuni ya pombe, na uwanja wa mabasi yeye anakodisha wenye makontena kama bandari kavu! kuharibu mitambo na mashine za umma za mabilioni ya fedha kama mwendawazimu ni kosa kubwa sana la jinai, ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kufikishwa mbele ya sheria kwa uharibifu kuu wa kutisha.

  4. Mali zote za Robert Kisena anazomiliki kwa jina lake au kwa majina ya kibiashara zikamatwe kwa amri ya Mahakama tayari kwa kuuzwa, ili kurejesha mashine na mitambo ya UDA alizoharibu, pamoja na mali zingine alizofuja. Ikiwa mali zake zimekopewa mapesa katika mabenki, wanaomdai watakatiwa sehemu yao baada ya kulipia mali za UDA.

  5. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameshangaza ulimwengu kwa kuwafikisha mahakamani akina Iddi simba kwa kupokea rushwa ya kisena, lakini yeye mtoaji wa hiyo rushwa amemwacha, kinyume kabisa cha sheria! Robert Kisena anayo hatia ya wazi kabisa ya utoaji wa rushwa ya shilingi 320 iliyo dhahiri hata kwa kipofu! Ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kuunganishwa na wenzake aliowapa hiyo rushwa.

  6. Robert Kisena apigwe marufuku kuonekana UDA kwa sababu hana mpango kabisa wa kuboresha shirika letu la usafiri., kwani hata mabasi yaliyotolewa na benki ya CRDB kusaidia kusafirisha wanafunzi jijini ameshindwa kuyaendesha kwa ajili ya watoto wetu, mpaka benki imelazimika kuyavuta kutoka kurasini wiki hii.

  7. Tunataka ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Fedha za serikali iwekwe wazi bungeni haraka, na wabunge wa Dar es salaam wahakikishe kwamba yaliyoagizwa na Mkaguzi Mkuu huyo yanatekelezwa kwa ajili ya ya maslahi ya taifa letu.

  Kuhusu uvumi uliozagaa kwamba Robert Kisena eti analindwa na Rais Kikwete katika uharibifu na ubadhirifu huu wa kutisha, tunasema kwamba yaweza kuwa hila tu ya hawa waporaji ya kujificha katika jina la KIKWETE! Nchi yetu haingozwi na majina ya watu bali na katiba na sheria. Hawa ni wabaya wa Kikwete, wanaotaka kumharibia maisha yake baada ya kuondoka madarakani yawe machungu.

  Hivyo, kama alivyowaondoa mara moja Mawaziri waporaji wa nchi yetu kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Umma, ambo ni lazima awafikishe mbele ya sheria, Kikwete analazimika pia kuwatupa kizimbani mara moja vigogo wote walioimemena UDA yetu pamoja na Robert Kisena... saa ya ukombozi ni sasa!

  Kama tulivyotamkwa katika kipengere 1 - 7 hapo juu yataonekana kuchelewa kutekelezwa na kuendelea kuwaudhi wanannchi, DP kwa nguvu ya Ibara ya 27 ya katiba ya nchi itachukua hatua kali. saa ya ukombozi ni sasa!


  MCHUNGAJI C. MTIKILA
  MWENYEKITI DP

  2 JUNI, 2012


  SOURCE: GAZETI LA UHURU 5 JUNI, 2012 UKURASA WA TATU.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wengi tunashangaa kwa nini kesi ya UDA haijamgusa Robert Kisena! Inaonekana huu ni mbuyu ambao kama hautakatwa wananchi wengi wataumia kwa kisingizio cha uwekezaji. Hii habari kwamba ununuzi wa UDA unawagusa wakubwa na dagaa watatolewa kafara unaonekana unataka kutimia.

  Hakika sikutegemea Kisena kuachwa kwenye kesi ya Iddi Simba na wenzake.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sakata la UDA lina Ridhwan ndani yake akishirikiana na kisena watanzania litawasumbua sana kulimaliza. Kisena ni rafiki wa karibu sana wa Ridhwan ana kashfa nyingi lakini system haitamgusa kwa sababu ya mkono wa Ridhwan ambaye wameingia kwenye biashara ya pamoja na kisena kununua UDA.

  Kisena ndiye yule jamaa aliyegombea ubunge Maswa na John Shibuda mwaka 2010 na baadaye akampiga polisi - OCD wa maswa hadi kofia ikadondoka chini na kumchania nguo za polisi ( aliipiga Jamhuri) lakini jambo la ajabu hakuna mashitaka dhidi yake hadi leo ingawa OCD alihamishiwa shinyanga mjini.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwekezaji, Robert Kisena amebadili matumizi ya UDA ikiwemo karakana ya kurasini iliyovunjwa lakini bado haguswi!!!!!!!!!!

  Mtikila anapaswa kufahamu kuwa hata kama Kisena atapigwa marufuku kukanyaga UDA bado wafanyakazi wake ndio wanaoongoza UDA kwa sasa hivyo anaoweza kuongoza kwa 'romote control' baada ya kuwatimia viongozi wa UDA iliyokuwa ya Umma.

  Kisena analindwa pia na Meya wa dar es salaam, Didas Masaburi ambaye mara kadhaa ameingia kwenye mgogoro na baraza la madiwani wa Dar es saam wakiongozwa na John Mnyika na wabunge wa Dar es salaam wakiongozwa na Abbas Mtemvu.
   
 5. papason

  papason JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hao akina riz 1, Kisena,ngeleja etc hamsini yao inakuja yaani baada ya uchaguzi wa 2015 tu niku wanyonga hadharani tena kwa mawee!
   
 6. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Robert Kisena kakopa bilioni 5 benki ya TIB kwa kutumia hati za UDA fedha za kilimo kwanza kwa kisingizio cha biashara zake za pamba. baadhi ya Maghala ya UDA kurasini yanawekwa Pamba. Hakuna mwekezaji hapo ni utapeli wa mchana kweupe.

  Wabunge wa dar es salaam watumie bunge linaloanza tarehe 12 Juni, 2012 kudai ripoti ya CAG kuna madudu kibao nchi itatikisika kwa nini kisena bado yuko mtaani.

  Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hosea ni msukuma, DPP Fereshi ni msukuma na Kisena ni msukuma na chenge ni msukumua wote wa shinyanga tunategemea nini hapo, kubebana. Hakuna kinachoshangaza Kisena kuachwa huru.
   
 7. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tusubiri tuone maana haya mambo ya Watanzania, yanaumiza kichwa sana.
   
 8. m

  mabhuimerafulu Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umeanza vizuri ukamaliza vibaya. HIVI MWANA JF HUWEZI KUJITAHIDI UKAKWEPA KULALAMIKIA UKABILA?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ukabila ukihusishwa na mtiririko unaoeleweka wa tuhuma unaweza kuleta hoja ya msingi.



  Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hosea ni msukuma,

  DPP Fereshi ni msukuma

  na Kisena ni msukuma - UDA

  na chenge ni msukumua - LADA

  wote wa shinyanga tunategemea nini hapo, kubebana. Hakuna kinachoshangaza Kisena kuachwa huru.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Robert Kisena aliweka fedha za rushwa kwenye akaunti binafsi ya Iddi Simba anapaswa kusimama kizimbani na wenzie kisha mahakama itaamua ni nani kati yao hahusiki na kashfa ya UDA.

  kashfa ya UDA yuko pia prof Athuman Kapuya ambaye pia ana hisa kwenye kiwanda cha malampaka Tabora cha kuchambua pamba kisha wawili hao wakaelekeza nguvu yao kununua UDA
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Suala la UDA lisipopata tiba ya kudumu na hasa kuirudhisha kwa umma kuna siku Dar es salaam patachimbika na patakuwa hapataoshi,

  majiji yote maarufu duniani kama London, New york na Tokyo yana usafiri wa umma ni sera gani hii ya kuwanyima wananchi usafiri wa umma kwa kisingizio cha uwekezaji???????????

  kashfa kama hizi za kujitakia ndizo zinawapa nguvu wapinzani pasipo sababu za msingi. Kisena ana kadi ya CCM na aligombea ubunge maswa kwa kadi ya chama hicho lakini amegeuka kuwanyang'anya wanannchi usafiri wao wa umma
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  It was very clear from the beggining kwamba jamaa walikuwa wanataka hizo karakana kama viwanja wafanye dry port za kuwekea makontena. No wonder Manji naye alikuwa ndani na akalalamika sana kwamba mchakato haukuwa wazi. Kweli juana na watu uvae viatu, ufisadi huu ulifanyika careless sana!
   
 13. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kitakacho fuata ni kuwaomba Boko Haram waanze kudeal na hawa viongozi wetu,kwa kuwa naona sauti zetu hazisikiki tena.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo. Alhajis Simba na Alhaj J. Kapuya ameingia ndani tena?
   
 15. G

  Galaticos Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kweli Tanzania shamba la bibi...watu wanajichumia tuuuu watakavyo.....
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mtikila usije pokea rushwa ya kisena ukanyamaza kama ulivyosainishwa na rostam!
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145

  Kwanini ni Mwekezaji wa UDA tu ndie wa kukamatwa na kufilisiwa? Hana GODFATHER'S? Hana

  Big CCM - Cult Backers?, what i can say is... it is strange... Something is cooking!!!

  * Or he might have make his Account as a Scapegoat, they moved out all what they need and all the praise to CCM and it's government for the Job well done...

  -- Try Idd Simba, Yusuf Manji, Chenge, Ngeleja, and other 3 brutus... wataifishe hao tutajua CCM
  Sasa hakuna Mchezo na kura zitarudi...


   
 18. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Unashangaa nini hujui wasukuma ni zaidi ya 25% ya watanzania wote; ulitaka wingi huo usionekane kwenye nafasi za serikali??? unajua 68% ya wasomi wote wanatoka kanda ya ziwa??? acha ukabila wewe ongea tu kama hoja ina mashiko utanungwa mkono lakini ukabila na udini hatutaki.
   
 19. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pamoja na kwamba kuna dosari hapa na pale ktk kutoa UDA lakini swali ni kwamba angepewa mzungu kama ambavyo wamepewa sehemu nyingi tu, mngelelamika wafungwe??? migodi mbona mmenywea? walinzi wenye dhamana ya mali/UDA ndo wakamatwe wajibu mashitaka sio mtu aliyekuja mchana kweupe; kama waliona tapeli wangekataa asinunue, kama waliomba rushwa sisi wtz ndo tuwaajibishe; unakumbuka walimpa barua wakisema aweke fedha hizo kwenye akaunti xxxx ambazo ni yao; sasa yeye kama mnunuzi kazi yake ilikuwa kulipa na kupata UDA, alilipa kama alivyoelekezwa na mliowapa dhamana na alipewa UDA. Story over.
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kisena hakamatwi hadi Ridhiwan aridhie.
   
Loading...