Mwekezaji wa shirika la UDA kukamatwa na kufilisiwa!

Pamoja na kwamba kuna dosari hapa na pale ktk kutoa UDA lakini swali ni kwamba angepewa mzungu kama ambavyo wamepewa sehemu nyingi tu, mngelelamika wafungwe??? migodi mbona mmenywea? walinzi wenye dhamana ya mali/UDA ndo wakamatwe wajibu mashitaka sio mtu aliyekuja mchana kweupe; kama waliona tapeli wangekataa asinunue, kama waliomba rushwa sisi wtz ndo tuwaajibishe; unakumbuka walimpa barua wakisema aweke fedha hizo kwenye akaunti xxxx ambazo ni yao; sasa yeye kama mnunuzi kazi yake ilikuwa kulipa na kupata UDA, alilipa kama alivyoelekezwa na mliowapa dhamana na alipewa UDA. Story over.
Haloo wacha kuleta ugoro wako hapa. Ati nini?? Story over?? Watu wanaiba mchana halafu unasema ati story over? Wewe pamoja na wao lazima tuwapeleke jela tu. Nasema tena mtaenda jena hakuna cha story over hapa!!!! Kuna timu inafanya kazi mchana na usiku,,, hata muwe mnakungiwa kifua na rais au mwanae LAZIMA MUENDE JELA TU!!! Zama hizi ni zama nyingine kabisa.... jitayarishe na kama ni ndugu yako mtayarishe....
 
Hii nayo ni kazi iliyofanyika awamu yetu hii ya wachapakazi hodari,lol!
 
Hili la mtikila nalo neno linahitaji kuzingatia maslahi ya umma..... kumbe mzee bado yupo ...nilidhani RIP
 
Pamoja na kwamba kuna dosari hapa na pale ktk kutoa UDA lakini swali ni kwamba angepewa mzungu kama ambavyo wamepewa sehemu nyingi tu, mngelelamika wafungwe??? migodi mbona mmenywea? walinzi wenye dhamana ya mali/UDA ndo wakamatwe wajibu mashitaka sio mtu aliyekuja mchana kweupe; kama waliona tapeli wangekataa asinunue, kama waliomba rushwa sisi wtz ndo tuwaajibishe; unakumbuka walimpa barua wakisema aweke fedha hizo kwenye akaunti xxxx ambazo ni yao; sasa yeye kama mnunuzi kazi yake ilikuwa kulipa na kupata UDA, alilipa kama alivyoelekezwa na mliowapa dhamana na alipewa UDA. Story over.
.

Huo ni utetezi ambao haukubariki mbele ya chombo chochote cha sheria... mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanavunja sheria ya nchi.... mvunja kanuni na mvunjishwaji kanuni wote wana makosa kwa kupeleka fedha kwenye akaunti ya mtu binafsi.
 
Unashangaa nini hujui wasukuma ni zaidi ya 25% ya watanzania wote; ulitaka wingi huo usionekane kwenye nafasi za serikali??? unajua 68% ya wasomi wote wanatoka kanda ya ziwa??? acha ukabila wewe ongea tu kama hoja ina mashiko utanungwa mkono lakini ukabila na udini hatutaki.

sensa hii ni ya mwaka gani? naona wamekukuna upele unaibuka na sensa bandia............kutoa takwimu ambazo hujatuambia chanzo chake nalo ni kosa la udanganyifu.
 
Haloo wacha kuleta ugoro wako hapa. Ati nini?? Story over?? Watu wanaiba mchana halafu unasema ati story over? Wewe pamoja na wao lazima tuwapeleke jela tu. Nasema tena mtaenda jena hakuna cha story over hapa!!!! Kuna timu inafanya kazi mchana na usiku,,, hata muwe mnakungiwa kifua na rais au mwanae LAZIMA MUENDE JELA TU!!! Zama hizi ni zama nyingine kabisa.... jitayarishe na kama ni ndugu yako mtayarishe....

Unaweza ukamgombania kila mtu vile hujui nini kinaanza kama yai na kuku, lakini ukweli wa mambo na ktk dunia ya structured approach, mwenye makosa makubwa ni yule ulompa dhamana akaichezea, akakusaliti, ni kama kwenye ndoa usigombane na mtu anayemla mkeo, gombana na mkeo maana ndo mwenye dhamana. Tukihakikisha kuwa tunaowapa dhamana wanawajibika 100% au 99% tu, tatzo linalojirudia rudia tutakuwa limekwisha kwa asilimia hizo hizo.

Sasa Robert inawezakana alijua kuwa hawa watu wanahujumu nchi lakini yeye haikuwa kazi yake, na pengine asingejua undani wa ama kweli au si kweli; utawala wa kuheshimiana yeye akafanya kazi yake kwa maelekezo ya viongozi halali wa UDA; kama waliwaibia wananchi, kamati za checks and balance ndo sehemu yake haswa. So i give robert the benefit of doubt, which also does not mean hana makosa hata kidogo.

TUMELEGEA SANA KWA WATU TUNAOWATUMA WATUTUMIKIE, wanalipwa fedha hawafanyi kazi yao; Jamaa ambao wanajaribu kuexploit huo udhaifu wetu, tunawachukia sana, NAKWAMBIA ni hulka ya binadamu wote kuexploit loopholes, wala sio ya robert. Kama hukuexploit UDA, haina maana hujaexploit popote, hata kusomea fani ambayo ni demanding ni kiexploit loopholes ili uje ufaidi. hata kufungua duka ni kuexploit loopholes, hata kuoa na kuolewa ni hivyo hivyo kuexploit loopholes. So it is human nature, we can not blame robert mpaka ithibitishwe dhamana ipi tuliyompa kuhusu kulinda maslahi ya UDA ambayo ameikiuka.

Watu wanaexploit loopholes za kodi, kweli wanakwepa kodi lakini mbona hawafungwi??? serikali inachofanya ni kuziba hizo loopholes pale inapoziona kuwepo; mfano ni kufuta mpango wa fedha ya nyumba kutolipiwa kodi, na hivyo fedha yote inakatwa kodi. Maana wabongo mshahara 120,000/- kodi ya nyumba 600,000/- vile tu ilikuwa haikatwi kodi. So serikali ziba loopholes kama zipo, waliopewa dhamana kama walifanya vivyo isivyo PELEKA MAHAKAMANI.
 
sensa hii ni ya mwaka gani? naona wamekukuna upele unaibuka na sensa bandia............kutoa takwimu ambazo hujatuambia chanzo chake nalo ni kosa la udanganyifu.

Kwenye hesabu hoja huwa ni kuprove; unaweza ukaomba tuprove au kama uko fit kichwani ukatoa counterprooof. So omba kimoja kifanyike acha kulalama; Harafu one thing has to be clear, simtetei mtu hapa, leo hata kesho hakuna. NACHOJARIBU KUKIINGIZA KICHWANI MWA MTANZANIA NI KWAMBA Hawa tunaowapa dhamana TUWAFUNDISHE ADABU KWANZA kabla ya kupanua wigo.
 
Tangu uhuru Tanzania haijawahi kufanya sensa ya udini,,,,,,, Nyerere alikataa hili kuwekwa kwenye sensa ni nani alihesabu watanzania kwa dini zao bila tunaohesabiwa kujua??????????? ni udaku kutumia takwimu za mtu yoyote.
 
Kama una uchungu wa dhati na nchi hii habari hii haitakuwa ndefu kusoma. Imeletwa kwenu na mchungaji Christopher Mtikila kupitia gazeti la uhuru.

Tumefurahishwa na taarifa za kizalendo kutoka ndani ya TAKUKURU kwamba thamani ya shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) ambalo ni mali ya wananchi siyo shilingi bilioni 11 tu kama ilivyokisiwa awali, bali ni zaidi ya shilingi bilioni 20.

Kwani shirika la UDA siyo tu lina karakana ya uhandisi ambayo ni moja ya kubwa kuliko zote katika Afrika Mashariki, ikiwa na mashine za kila aina na mitambo ya kila huduma, tulivyopewa na Wajerumani ambao dunia inawaheshimu kwa ubingwa wao katika uhandisi, bali pia shirika lina mali nyingi sana zisizohamishika.

Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya katiba ya nchi, inayomuwajibisha kila raia kulinda mali asilia ya taifa letu, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na kututaka sisi sote tutunze vizuri mali yote ya mamalaka ya nchi na ya pamoja kama shirika letu la UDA, na kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa letu kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya nchi yao, tunatoa tamko kwamba:

1. Wahusika wote katika serikali yetu yaani Waziri wa Fedha, Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa tawala za Mikoa na serikali za Mitaa wanapaswa kufikishwa Mahakamani mara moja kwa uharibifu na ubadhirifu wa mali za mabilioni ya fedha za shirika letu la UDA.....saa ya ukombozi ni sasa.

2. shirika la thamani ya zaidi shilingi bilioni 22 kuuziwa Robert Kisena kwa shilingi bilioni moja tu na robo, bila kutangaza tenda ya wazi kama inavyopasa kisheria na kupata mwekezaji wa kweli mwenye zaidi ya hizo bilioni 22, lakini huyo Robet kisena akalipa shilingi milioni 285 tu na kukabidhiwa mali ya wananchi ya shilingi bilioni 22 ni Ufisadi kichaa! Mauzo yabadilishwe mara moja, na Robert Kisena pamoja na hao watumishi wa umma waliokula naye dili hii wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria ndani ya siku saba! Uharamia huu ndio unaopaswa kumalizwa kwa risasi hadharani! tutahakikisha kuwa sheria ya adhabu hii inatungwa upesi sana, ...saa ya ukombozi ni sasa.

3. Shirika la UDA ni usafiri wa wananchi katika jiji la Dar es salaam, hivyo mwekezaji anayetakiwa ni wa kuliboresha kwa ajili ya huduma hiyo, siyo wa kuliua! Robert Kisena ameharibu na kukongoloa kabisa mitambo na mashine zote za UDA za mabilioni ya fedha mashine nyingine zimekatwa na kuuzwa kama chuma chakavu 'scrap'! Karakana ya UDA yeye (kisena) anazipangisha kama maghala ya kuweka mtama wa kampuni ya pombe, na uwanja wa mabasi yeye anakodisha wenye makontena kama bandari kavu! kuharibu mitambo na mashine za umma za mabilioni ya fedha kama mwendawazimu ni kosa kubwa sana la jinai, ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kufikishwa mbele ya sheria kwa uharibifu kuu wa kutisha.

4. Mali zote za Robert Kisena anazomiliki kwa jina lake au kwa majina ya kibiashara zikamatwe kwa amri ya Mahakama tayari kwa kuuzwa, ili kurejesha mashine na mitambo ya UDA alizoharibu, pamoja na mali zingine alizofuja. Ikiwa mali zake zimekopewa mapesa katika mabenki, wanaomdai watakatiwa sehemu yao baada ya kulipia mali za UDA.

5. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameshangaza ulimwengu kwa kuwafikisha mahakamani akina Iddi simba kwa kupokea rushwa ya kisena, lakini yeye mtoaji wa hiyo rushwa amemwacha, kinyume kabisa cha sheria! Robert Kisena anayo hatia ya wazi kabisa ya utoaji wa rushwa ya shilingi 320 iliyo dhahiri hata kwa kipofu! Ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kuunganishwa na wenzake aliowapa hiyo rushwa.

6. Robert Kisena apigwe marufuku kuonekana UDA kwa sababu hana mpango kabisa wa kuboresha shirika letu la usafiri., kwani hata mabasi yaliyotolewa na benki ya CRDB kusaidia kusafirisha wanafunzi jijini ameshindwa kuyaendesha kwa ajili ya watoto wetu, mpaka benki imelazimika kuyavuta kutoka kurasini wiki hii.

7. Tunataka ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Fedha za serikali iwekwe wazi bungeni haraka, na wabunge wa Dar es salaam wahakikishe kwamba yaliyoagizwa na Mkaguzi Mkuu huyo yanatekelezwa kwa ajili ya ya maslahi ya taifa letu.

Kuhusu uvumi uliozagaa kwamba Robert Kisena eti analindwa na Rais Kikwete katika uharibifu na ubadhirifu huu wa kutisha, tunasema kwamba yaweza kuwa hila tu ya hawa waporaji ya kujificha katika jina la KIKWETE! Nchi yetu haingozwi na majina ya watu bali na katiba na sheria. Hawa ni wabaya wa Kikwete, wanaotaka kumharibia maisha yake baada ya kuondoka madarakani yawe machungu.

Hivyo, kama alivyowaondoa mara moja Mawaziri waporaji wa nchi yetu kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Umma, ambo ni lazima awafikishe mbele ya sheria, Kikwete analazimika pia kuwatupa kizimbani mara moja vigogo wote walioimemena UDA yetu pamoja na Robert Kisena... saa ya ukombozi ni sasa!

Kama tulivyotamkwa katika kipengere 1 - 7 hapo juu yataonekana kuchelewa kutekelezwa na kuendelea kuwaudhi wanannchi, DP kwa nguvu ya Ibara ya 27 ya katiba ya nchi itachukua hatua kali. saa ya ukombozi ni sasa!

MCHUNGAJI C. MTIKILA
MWENYEKITI DP
2 JUNI, 2012

SOURCE: GAZETI LA UHURU 5 JUNI, 2012 UKURASA WA TATU.
wapi sasa hi
 
Duh, ukisikia time will tell ndio hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Robert Kisena aliweka fedha za rushwa kwenye akaunti binafsi ya Iddi Simba anapaswa kusimama kizimbani na wenzie kisha mahakama itaamua ni nani kati yao hahusiki na kashfa ya UDA.

kashfa ya UDA yuko pia prof Athuman Kapuya ambaye pia ana hisa kwenye kiwanda cha malampaka Tabora cha kuchambua pamba kisha wawili hao wakaelekeza nguvu yao kununua UDA
Je IDD SIMBA , RIDHIWANI NA MASABURI WATATAJWA ? Hili jambo tumelipigia kelele muda mrefu sana ila tulipuuzwa , hatutaki ashughulikiwe Kisena pekee
 
Hawa ndo nataka wachomolewe wazi kweupee! Tutajua hata ulanguzi wao wa vyeo vilivyokuwa vinauzwa.
 
Kama una uchungu wa dhati na nchi hii habari hii haitakuwa ndefu kusoma. Imeletwa kwenu na mchungaji Christopher Mtikila kupitia gazeti la uhuru.

Tumefurahishwa na taarifa za kizalendo kutoka ndani ya TAKUKURU kwamba thamani ya shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) ambalo ni mali ya wananchi siyo shilingi bilioni 11 tu kama ilivyokisiwa awali, bali ni zaidi ya shilingi bilioni 20.

Kwani shirika la UDA siyo tu lina karakana ya uhandisi ambayo ni moja ya kubwa kuliko zote katika Afrika Mashariki, ikiwa na mashine za kila aina na mitambo ya kila huduma, tulivyopewa na Wajerumani ambao dunia inawaheshimu kwa ubingwa wao katika uhandisi, bali pia shirika lina mali nyingi sana zisizohamishika.

Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya katiba ya nchi, inayomuwajibisha kila raia kulinda mali asilia ya taifa letu, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na kututaka sisi sote tutunze vizuri mali yote ya mamalaka ya nchi na ya pamoja kama shirika letu la UDA, na kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa letu kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya nchi yao, tunatoa tamko kwamba:

1. Wahusika wote katika serikali yetu yaani Waziri wa Fedha, Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa tawala za Mikoa na serikali za Mitaa wanapaswa kufikishwa Mahakamani mara moja kwa uharibifu na ubadhirifu wa mali za mabilioni ya fedha za shirika letu la UDA.....saa ya ukombozi ni sasa.

2. shirika la thamani ya zaidi shilingi bilioni 22 kuuziwa Robert Kisena kwa shilingi bilioni moja tu na robo, bila kutangaza tenda ya wazi kama inavyopasa kisheria na kupata mwekezaji wa kweli mwenye zaidi ya hizo bilioni 22, lakini huyo Robet kisena akalipa shilingi milioni 285 tu na kukabidhiwa mali ya wananchi ya shilingi bilioni 22 ni Ufisadi kichaa! Mauzo yabadilishwe mara moja, na Robert Kisena pamoja na hao watumishi wa umma waliokula naye dili hii wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria ndani ya siku saba! Uharamia huu ndio unaopaswa kumalizwa kwa risasi hadharani! tutahakikisha kuwa sheria ya adhabu hii inatungwa upesi sana, ...saa ya ukombozi ni sasa.

3. Shirika la UDA ni usafiri wa wananchi katika jiji la Dar es salaam, hivyo mwekezaji anayetakiwa ni wa kuliboresha kwa ajili ya huduma hiyo, siyo wa kuliua! Robert Kisena ameharibu na kukongoloa kabisa mitambo na mashine zote za UDA za mabilioni ya fedha mashine nyingine zimekatwa na kuuzwa kama chuma chakavu 'scrap'! Karakana ya UDA yeye (kisena) anazipangisha kama maghala ya kuweka mtama wa kampuni ya pombe, na uwanja wa mabasi yeye anakodisha wenye makontena kama bandari kavu! kuharibu mitambo na mashine za umma za mabilioni ya fedha kama mwendawazimu ni kosa kubwa sana la jinai, ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kufikishwa mbele ya sheria kwa uharibifu kuu wa kutisha.

4. Mali zote za Robert Kisena anazomiliki kwa jina lake au kwa majina ya kibiashara zikamatwe kwa amri ya Mahakama tayari kwa kuuzwa, ili kurejesha mashine na mitambo ya UDA alizoharibu, pamoja na mali zingine alizofuja. Ikiwa mali zake zimekopewa mapesa katika mabenki, wanaomdai watakatiwa sehemu yao baada ya kulipia mali za UDA.

5. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameshangaza ulimwengu kwa kuwafikisha mahakamani akina Iddi simba kwa kupokea rushwa ya kisena, lakini yeye mtoaji wa hiyo rushwa amemwacha, kinyume kabisa cha sheria! Robert Kisena anayo hatia ya wazi kabisa ya utoaji wa rushwa ya shilingi 320 iliyo dhahiri hata kwa kipofu! Ni lazima Robert Kisena akamatwe mara moja na kuunganishwa na wenzake aliowapa hiyo rushwa.

6. Robert Kisena apigwe marufuku kuonekana UDA kwa sababu hana mpango kabisa wa kuboresha shirika letu la usafiri., kwani hata mabasi yaliyotolewa na benki ya CRDB kusaidia kusafirisha wanafunzi jijini ameshindwa kuyaendesha kwa ajili ya watoto wetu, mpaka benki imelazimika kuyavuta kutoka kurasini wiki hii.

7. Tunataka ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Fedha za serikali iwekwe wazi bungeni haraka, na wabunge wa Dar es salaam wahakikishe kwamba yaliyoagizwa na Mkaguzi Mkuu huyo yanatekelezwa kwa ajili ya ya maslahi ya taifa letu.

Kuhusu uvumi uliozagaa kwamba Robert Kisena eti analindwa na Rais Kikwete katika uharibifu na ubadhirifu huu wa kutisha, tunasema kwamba yaweza kuwa hila tu ya hawa waporaji ya kujificha katika jina la KIKWETE! Nchi yetu haingozwi na majina ya watu bali na katiba na sheria. Hawa ni wabaya wa Kikwete, wanaotaka kumharibia maisha yake baada ya kuondoka madarakani yawe machungu.

Hivyo, kama alivyowaondoa mara moja Mawaziri waporaji wa nchi yetu kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Umma, ambo ni lazima awafikishe mbele ya sheria, Kikwete analazimika pia kuwatupa kizimbani mara moja vigogo wote walioimemena UDA yetu pamoja na Robert Kisena... saa ya ukombozi ni sasa!

Kama tulivyotamkwa katika kipengere 1 - 7 hapo juu yataonekana kuchelewa kutekelezwa na kuendelea kuwaudhi wanannchi, DP kwa nguvu ya Ibara ya 27 ya katiba ya nchi itachukua hatua kali. saa ya ukombozi ni sasa!

MCHUNGAJI C. MTIKILA
MWENYEKITI DP

2 JUNI, 2012

SOURCE: GAZETI LA UHURU 5 JUNI, 2012 UKURASA WA TATU.
KABURI LIMEFUKULIWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom