mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
Naguswa kutoa angalizo juu ya tahadhari inayopaswa kuchukuliwa na Serikari ama wenye mamlaka sawia.Mji wa Dar es salaam umekuwa ukikua kwa kasi sana kutokana na wakazi wapya kuongezeka sababu ya vivutio mbalimbali vya kimwili,kiroho na kimazingira.
Maeneo ya pugu ni moja kati ya vitongoji vikongwe ktk jiji la Dar hasa kwa kuhusishwa na utumishi wa awali wa shujaa wa taifa Hayati Mwl. J.K Nyerere {Mungu amrehemu aliko} akiwa mwalimu katika sekondari ya Pugu.Lakini kwa sasa kuwa sehemu ya makazi ya viongozi waandamizi wastaafu akiwemo Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda na wengine.
Katika mpaka wa eneo la pugu na msitu wa kisarawe kuna makazi ya mwekezaji mwindaji {mwenye asili ya mataifa ya magharibi} na mfanyabiashara wa wanyama pori maarufu kama mzungu.Mzungu huyu anawinda,anahifadhi,anavuna na kuwasafirisha nje ya nchi wanyama hai aina mbalimbali kama simba,duma,chui,nyani,sokwe,nyoka,chatu,n.k
Inasemekana ana vibali vyote vya kufanya biashara husika {japo si ya kuvuka mipaka isiostahiri} lakini Katika mengi yenye mapungufu ni uhifadhi duni wa wanyama hatari husika kwa kiwango cha kuweza kucholopoka na kusababisha tafrani kwa wakazi wa maeneo yalio karibu.Lakini pia amekuwa akipitiliza kwa kuingia katika maeneo ya jeshi ..
Ni wito wangu kwa taasisi zinazohusika {Wizara ya Maliasiri na Utalii,JWTZ,n.k} kuchukua tahadhali mahsusi na hatua stahiki za kuzuia matatizo,maafa ama uharibifu.Pia leseni hizi zifanyiwe mapitio na ikibidi zifutwe ikiwa tija yake kwa taifa ni ya kutia shaka.