Mwaweza kuninukuu.. You can quote me!

Mwaweza kuninukuu.. You can quote me!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,095
Reaction score
43,305
  • Kiongozi anayetewala kwa vitisho, ameishiwa maono

  • Mtu akikutisha maana yake ameshindwa kukushawishi

  • Wakianza kuzungumzia umwagikaji damu, wanajiandaaa kuimwaga

  • Ukiona watu wanapiga kelele, usidhani wote wanashangilia; wengine wanalia!

  • Ukiona watu wazima wanachekacheka mbele ya bosi, ujue wanajikomba!

  • Haki haitolewi bila gharama

  • Shawishi upewe haki yako, ukikataliwa lazimisha kwani hauna cha kupoteza isipokuwa haki yako!

  • Historia ya watawala duniani ni kuwaridhisha matajiri, hadi maskini watakapoamka kutaka kubadilisha historia na watawala!

  • Usiwasukumize maskini hadi wakakosa pa kusimamia; wakianza kukusukumiza utakosa pa kuhamia!

  • Mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?

  • CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!

  • Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!

  • Hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!

  • Sehemu moja ya ushiriki wa wananchi katika demokrasia ni katika kuwahoji, kuwapinga na kuwakosoa viongozi wao; pasipo kuwaomba msamaha kwanza!

  • Wafanyakazi wakisalimu amri watawala watawapangia mishahara kwa amri!

  • Mtawala akizungumza sana na kwa kirefu tena kwa jazba na manjonjo akimaliza wewe kataa! itabidi akushawishi vinginevyo atarudia tena!

Zote na M.M.
 
1. Mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?

2. CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!

3. Hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!

4. Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!

nimezipenda kweli hizi...hasa ya nne. Imefikia wakati watu waka-link ya nne na ya kwanza.
 
Nimeipenda haya maneno.Nitajadili baadaye ngoja niende ofisini kwanza.
 
  • kiongozi anayetewala kwa vitisho, ameishiwa maono
  • mtu akikutisha maana yake ameshindwa kukushawishi
  • wakianza kuzungumzia umwagikaji damu, wanajiandaaa kuimwaga!
  • ukiona watu wanapiga kelele, usidhani wote wanashangilia; wengine wanalia!
  • ukiona watu wazima wanachekacheka mbele ya bosi, ujue wanajikomba!
  • haki haitolewi bila gharama
  • shawishi upewe haki yako, ukikataliwa lazimisha kwani hauna cha kupoteza isipokuwa haki yako!
  • historia ya watawala duniani ni kuwaridhisha matajiri, hadi maskini watakapoamka kutaka kubadilisha historia na watawala!
  • usiwasukumize maskini hadi wakakosa pa kusimamia; wakianza kukusukumiza utakosa pa kuhamia!
  • mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?
  • ccm haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!
  • katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!
  • hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!
  • sehemu moja ya ushiriki wa wananchi katika demokrasia ni katika kuwahoji, kuwapinga na kuwakosoa viongozi wao; pasipo kuwaomba msamaha kwanza!
  • wafanyakazi wakisalimu amri watawala watawapangia mishahara kwa amri!
  • mtawala akizungumza sana na kwa kirefu tena kwa jazba na manjonjo akimaliza wewe kataa! Itabidi akushawishi vinginevyo atarudia tena!

zote na m.m.

no haya ni maono!!!!!!!!! Mkuuu m.m
 
Mkuu MM mimi nadhani wakati wakati umefika tukaitumia ile ripoti ya mhadhiri wa Mzumbe kuisambaza kwenye vyombo vya habari na haswa wewe huwa unaandikia Mwanahalisi. Tunaweza kuondoa jina la yule msomi lakini maoni na uchambuzi ukabaki kama ulivyo maana gazeti linafika sehemu kubwa na litasomwa na wengi ili waelewe kuwa kinachodiwa kinawezekana ila ni ubishi na jeuri ya serekali iliyo madarakani. Haiwezekani raisi wa nchi ahutubie taifa kwa hotuba iliyojaa uwongo pasi vigezo.
Mungu ibariki Tanzania na wabariki wafanyakazi wake.
 
  • Kiongozi anayetewala kwa vitisho, ameishiwa maono
  • Mtu akikutisha maana yake ameshindwa kukushawishi
  • Wakianza kuzungumzia umwagikaji damu, wanajiandaaa kuimwaga!
  • Ukiona watu wanapiga kelele, usidhani wote wanashangilia; wengine wanalia!
  • Ukiona watu wazima wanachekacheka mbele ya bosi, ujue wanajikomba!
  • Haki haitolewi bila gharama
  • Shawishi upewe haki yako, ukikataliwa lazimisha kwani hauna cha kupoteza isipokuwa haki yako!
  • Historia ya watawala duniani ni kuwaridhisha matajiri, hadi maskini watakapoamka kutaka kubadilisha historia na watawala!
  • Usiwasukumize maskini hadi wakakosa pa kusimamia; wakianza kukusukumiza utakosa pa kuhamia!
  • Mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?
  • CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!
  • Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!
  • Hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!
  • Sehemu moja ya ushiriki wa wananchi katika demokrasia ni katika kuwahoji, kuwapinga na kuwakosoa viongozi wao; pasipo kuwaomba msamaha kwanza!
  • Wafanyakazi wakisalimu amri watawala watawapangia mishahara kwa amri!
  • Mtawala akizungumza sana na kwa kirefu tena kwa jazba na manjonjo akimaliza wewe kataa! itabidi akushawishi vinginevyo atarudia tena!

Zote na M.M.

Mkuu hapa sijakupata vizuri.Nieleweshe tafadhali.
 
Well said, mbona usiseme tu kuwa Watanzania wanapaswa kukataa alichosema Kikwete?
 
Mwanakijiji, me and my alter ego like your way of thinking. We wish there were many of us
 
Maisha bora aahidi yeye, tukikumbushia, anasema hataki kura zetu, na vitisho kibao! Duh! Labda tutafika
 
  • CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!
  • Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!
Zote na M.M.

MM, CCM itaondolewa kwa kusababishwa?!, si mpaka hao wasababishaji wawepo!.
Pomoja na haki hiyo ya kuchagua ubovu, kama waliitumia haki hiyo kuchagua ubovu wakiamini ndio ubora, na hata walipogundua kuwa kumbe walidanganywa na kuchagua ubovu, na wameuthibitisha ubovu wenyewe, kama wataendelea kuchagua ubovu, ili hali wanajua wazi ni ubovu, wananchi hao ndio wenye matatizo, na hawataamka kamwe na kuchagua vyema, wataendelea kuchagua ubovu mpaka mwisho wa maisha yao...

"Ubovu huu (CCM), Utatawala Milele!"-

Pasco.
 
Back
Top Bottom