Mwaweza kuninukuu.. You can quote me! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaweza kuninukuu.. You can quote me!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 6, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  • Kiongozi anayetewala kwa vitisho, ameishiwa maono

  • Mtu akikutisha maana yake ameshindwa kukushawishi

  • Wakianza kuzungumzia umwagikaji damu, wanajiandaaa kuimwaga

  • Ukiona watu wanapiga kelele, usidhani wote wanashangilia; wengine wanalia!

  • Ukiona watu wazima wanachekacheka mbele ya bosi, ujue wanajikomba!

  • Haki haitolewi bila gharama

  • Shawishi upewe haki yako, ukikataliwa lazimisha kwani hauna cha kupoteza isipokuwa haki yako!

  • Historia ya watawala duniani ni kuwaridhisha matajiri, hadi maskini watakapoamka kutaka kubadilisha historia na watawala!

  • Usiwasukumize maskini hadi wakakosa pa kusimamia; wakianza kukusukumiza utakosa pa kuhamia!

  • Mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?

  • CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!

  • Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!

  • Hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!

  • Sehemu moja ya ushiriki wa wananchi katika demokrasia ni katika kuwahoji, kuwapinga na kuwakosoa viongozi wao; pasipo kuwaomba msamaha kwanza!

  • Wafanyakazi wakisalimu amri watawala watawapangia mishahara kwa amri!

  • Mtawala akizungumza sana na kwa kirefu tena kwa jazba na manjonjo akimaliza wewe kataa! itabidi akushawishi vinginevyo atarudia tena!

  Zote na M.M.
   
 2. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  imetulia mkuu hii
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  1. Mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kubadilishwa na wanufaikaji wake wakuu! Yaani, uwaambie fisi wabadili utaratibu wa kula mifupa?

  2. CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuombewa au kungojewa; itaondolewa kwa kusababishwa!

  3. Hakuna haki ya kuipenda serikali; katika demokrasia kuichukia serikali ndio msingi wa kuipigia kura ya kuiondoa! Hivyo, chuki dhidi ya serikali siyo uhaini ni sehemu ya demokrasia!

  4. Katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua ubovu; na wana haki ya kuishi na matokeo ya uchaguzi wao huo hadi watakapoamka na kuchagua vyema!

  nimezipenda kweli hizi...hasa ya nne. Imefikia wakati watu waka-link ya nne na ya kwanza.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,975
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda haya maneno.Nitajadili baadaye ngoja niende ofisini kwanza.
   
 5. MARIJANI

  MARIJANI Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  no haya ni maono!!!!!!!!! Mkuuu m.m
   
 6. T

  Tristan Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,232
  Likes Received: 1,545
  Trophy Points: 280
  Mkuu MM mimi nadhani wakati wakati umefika tukaitumia ile ripoti ya mhadhiri wa Mzumbe kuisambaza kwenye vyombo vya habari na haswa wewe huwa unaandikia Mwanahalisi. Tunaweza kuondoa jina la yule msomi lakini maoni na uchambuzi ukabaki kama ulivyo maana gazeti linafika sehemu kubwa na litasomwa na wengi ili waelewe kuwa kinachodiwa kinawezekana ila ni ubishi na jeuri ya serekali iliyo madarakani. Haiwezekani raisi wa nchi ahutubie taifa kwa hotuba iliyojaa uwongo pasi vigezo.
  Mungu ibariki Tanzania na wabariki wafanyakazi wake.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,039
  Trophy Points: 280
  Swadakta
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,975
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa sijakupata vizuri.Nieleweshe tafadhali.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  haki haitolewi kama hisani; inadaiwa na ikikataliwa inalazimishwa!
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe Mzee wewe! Hii nimeipenda!
   
 12. J

  Jobo JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Well said, mbona usiseme tu kuwa Watanzania wanapaswa kukataa alichosema Kikwete?
   
 13. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama signature yangu vilee..! ki mantiki zinashabihiana.!
   
 14. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji, me and my alter ego like your way of thinking. We wish there were many of us
   
 15. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maisha bora aahidi yeye, tukikumbushia, anasema hataki kura zetu, na vitisho kibao! Duh! Labda tutafika
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,988
  Likes Received: 12,496
  Trophy Points: 280
  MM, CCM itaondolewa kwa kusababishwa?!, si mpaka hao wasababishaji wawepo!.
  Pomoja na haki hiyo ya kuchagua ubovu, kama waliitumia haki hiyo kuchagua ubovu wakiamini ndio ubora, na hata walipogundua kuwa kumbe walidanganywa na kuchagua ubovu, na wameuthibitisha ubovu wenyewe, kama wataendelea kuchagua ubovu, ili hali wanajua wazi ni ubovu, wananchi hao ndio wenye matatizo, na hawataamka kamwe na kuchagua vyema, wataendelea kuchagua ubovu mpaka mwisho wa maisha yao...

  "Ubovu huu (CCM), Utatawala Milele!"-

  Pasco.
   
Loading...