Mwasisi wa CHASO, Deogratius Kisandu ajiunga na CCM

Mwasisi wa CHASO, Deogratius Kisandu ajiunga na CCM

DSC00586.JPG


SABABU ZA KUJIUNGA NA NCCR-MAGEUZI
1. Ni Chama kikongwe, waasisi na waanzilishi wa mageuzi hapa nchini. Ni Chama kilichopitia migogoro na misukosuko mingi ambacho ninaamini kimekomaa.

2. Ni chuo kizuri cha wanasiasa,watu wengi wamepitia hapa, wakafundwa na baadaye wakatamaniwa hata vyama vingine. Mifano michache ni Dkt. Masumbuko Lamwai, Dkt. Festus Limbu, Steven Wasira (CCM) na Ndesamburo, John Mnyika, Joseph R. Selasini, Chiku Obwao, Suzana Kiwanga, Profesa Mwesigwa Baregu, Mabere Marando nk.
Ninaamini kwamba, kujiunga kwangu na Chama hiki nitajifunza mambo mengi.

3. NCCR-Mageuzi ni Chama na kipimo cha demokrasia kwa vitendo. Ni Chama ambacho hakina mtu mmoja tu kwa ajili ya nafasi ya za uongozi, yeyote ana nafasi ya kugombea nafasi anayotaka na mkutano mkuu wa Chama ndio uamue nani anafaa kuwa mgombea urais.
Mfano, Mwaka 1995 Chama kilimsimamisha ndugu A.L. Mrema kugombea urais. Mwaka 2000 Chama kilimsimamisha ndugu Edith S. Lucina kugombea urais. Mwaka 2005 Dkt. E.A. S. Mvungi aligombea urais na mwaka 2010 Chama kilimsimamisha ndugu Hashim S. Rungwe aligombea urais. Hii ni tofauti na baadhi ya vyama vingine.

4. Nilipotangaza kugombea urais kupitia CHADEMA, niliwekewa mizengwe, nikajengewa chuki. Nilitangaza kugombea urais, lakini sikutangaza kwa mwaka gani, kwani mwaka 2015 umri wangu wa kikatiba wa kugombea urais hauniruhusu, nilikusudia baada ya mwaka 2015, lakini kwa CHADEMA inaonekana wana wagombea wao wa Kaskazini kwa miaka hamsini ijayo.
Ninaamini ndani ya NCCR-Mageuzi, umri wangu ukifika, mkutano mkuu ndio utaamua na siyo kiongozi mmoja.
Baada ya kusema hayo, ninaomba sasa nikabidhiwe Kadi ya NCCR-Mageuzi.


----------------------------------04/01/2013
D. KISANDU
 
Mapema sana tulimshauri ajiunge na ccm akawa hatuelewi, tulimshauri hivyo kwasababu tangu mwanzo alionyesha tabia mienendo ya ccm, pls Nape Nnauye mpelekeni huyu kisandu kwenye matibabu ya majeraha aliyokua akilalamika enzi yupo nccr la siivyo atahamia ACT huyu

Mbona CCM wamemtupa na wamemuwekea vikwazo vya kimaisha huko mwanza.
 
Back
Top Bottom