Mwasapila awatoa hofu wagonjwa wa Ukimwi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwasapila awatoa hofu wagonjwa wa Ukimwi.

Discussion in 'JF Doctor' started by Monasha, Apr 24, 2011.

 1. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 80
  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, amewatoa hofu wagonjwa wa Ukimwi ambao wamepata tiba yake na baada ya kupimwa wameendelee kukutwa na virusi vya ugonjwa huo.

  Akizungumza kabla ya kuanza kutoa tiba jana nyumbani kwake Samunge, Mchungaji Mwasapila alisema mgonjwa wa Ukimwi mara baada ya kupata kikombe, virusi vya HIV vitaendelea kupukutika taratibu na havitazaliana tena.

  "Napenda kuwaondoa hofu wenye Ukimwi kwamba ukitumia kikombe, utaona mabadiliko ya afya yako baada ya siku saba tu, lakini unaweza kupima na kujikuta bado unavirusi, usiwe na hofu vitapukutika na mwisho vitakwisha vyote mwilini," alisema Mwasapila.

  Mwasapila alisema mabadiliko ya afya kwa wenye virusi vya Ukimwi yatakuwa kati ya siku saba na 21 na kama mgonjwa na anahofu, anaweza kuendelea kutumia dawa zake za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs), ila alisisitiza kuwa dawa yake inatosha kuponya.

  Je wewe mwanajamiii unasemaje kwa hili la Babu. Ataweza kuponya UKIWMI au ni porojo tu??
  Naomba pia kama una mtu uliyemwona kapona kabisa basi usisite kutueleza ukweli wanajamii wenzako.
  Mi si mwamini babu.
   
 2. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ewe mwenye HIV uliyekunywa kikombe cha babu, ni bora ukaendelea na dawa zako ARV, na baadaye ujikute umepona kuliko kuacha ARV, na ujikute hujapona.

  Babu haaminiki maana ameanza kujitetea, kuwa inaweza fikia siku 21.

  Haya let us wait and see kama sio alama ya mpinga Kristo 666 inapigwa mihuri!!!!


   
 3. GABLLE

  GABLLE Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uponyaji wa babu ni kwa imani ndugu zangu. Usitegemee kupona kama huna imani!!!!!:A S-heart-2:
   
Loading...