Kila mmoja anayajua maneno aliyoongea Shibuda ndani ya kikao cha CCM. Angekuwa Chadema damu asingeongea vile. Swali ni je, Chadema imfanyeje? Mimi napendekeza, Chama kimvumilie tu. Wengine watabisha ila Shibuda ana nguvu sana kwa Wasukuma na CCM wanalijua hilo. Kuondoka kwake litakuwa pigo kubwa. Namshauri Mbowe ajaribu kumpa nafasi fulani kwenye chama tuone ata perfom vipi. Huyu bwana ni shetani muhimu. Kama anataka urais apewe nafasi agombee wanachama wenyewe wataamua. Siasa ni ujanja pia. Kwa mfano Republican hawakumfukuza Powel kwa kumpigia kampeni Obama kwa kampeni zote mbili. Chadema tujifunze kuwavumilia watu controversial kama Shibuda, so long as hafanyi maamuzi ya Ki ccm ndani ya chama aachwe tu, tena akaribishwe hata kwenye M4C. Maoni yangu tu!