Hawa hapa wazee walioshindwa kudumu kwenye mfumo wa siasa na sasa wanapelekwa mfumo unavyotaka

Beatrice Kamugisha

Senior Member
May 18, 2019
184
1,000
1. Edward Lowassa - alikuwa na nguvu CCM , akawa na nguvu upinzani huku akihesabika Kama shujaa wa mabadiliko. Hakudumu kwenye huo ushujaa akakubali kurudi CCM hadhi yake ikaporomoka na sasa anafanya watu wanayotaka siyo yeye anayotaka. Kisiasa hana Tena ushawishi, anazeeka akiwa amepotea kwenye ramani ya siasa.

2. Dkt. Wilbroad Slaa -
huyu aliupigania sana upinzani lakini chama chake kikasaliti maono yake, badala apigane akiwa ndani akapaniki na kukaa pembeni. Akiwa huko pembeni akaamua kujiunga CCM kupambana na upinzani lakini hakupata nafasi yakutimiza ndoto yake. Leo hii ni mteule kama Balozi na waliomteua ni ambao alikuwa anaamini wanavunja sheria, katiba na wanadhulumu watanzania. Hata Leo naamini anaona maovu kutoka kwa wale waliomteua lakini awezi Tena kuyasemea. Yupo kifungo Cha fikra na wale waliokuwa wanamuunga mkono wamepoteza imani naye.

3. Bernard Membe -
alisifika Kama Jasusi lakini kwa hali yake ya Sasa nachelea kuamini kwamba ni jasusi kweli. Alikosa urais 2015 akakasirika na baadaye akajiunga upinzani akitegemea atasimamishwa kama mgombea pekee mwenye nguvu wa upinzani. Hakutumia ujasusi wake kumwona Lisu, na Kama alimwona akutumia ujasusi huo kuona nguvu ya Lisu dhidi yake. Leo mambo yamebadilika, Hakuna kampeni Wala ushawishi, kwa umri wake amepotea kwenye ramani ya siasa za Tanzania kwa kutokujua Nini afanye kwa wakati gani.

4. James Mbatia -
Amesimamia kwa muda mrefu hoja ya mama Tanzania, Amesimamia elimu na kujipambanua kama mpinzani wa kweli. Mwaka huu wakamlaghai akawasaliti wapinzani wenzake na kujitengenezea NCCR yake akiamini anakwenda kuwa chama kikuu Cha upinzani Tanzania. Akapewa mashangingi akaanza kupambana na chadema Mbeya chini ya ulinzi wa Dola na akaelekea Mara kuvuna wanachama. Kwa wakati huo anayafanya hayo aliamini anakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani hivyo akawashawishi baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamfuate. Mara paap Lissu akaingia nchini akabadili upepo wa siasa nchini. Waliomwaid Mbatia wabunge wakajikuta wao wenyewe hawana uhakika wakushinda, wakaachana na mipango yote wakabaki kukipambania chama chake. Leo hii Mbatia na watu wake hata uwezo wakufany kampeni Jimbo moja hawana. Usaliti.mwisho amepotea kwenye ramani za siasa.

5. Fredrik Sumaye -
Huyu tayari amekwama, Leo nimemsikia anauliza Mbowe anamsaidiaje Lisu kwenye kampeni badala yakueleza anamsaidiaje Mwenyekiti wake wa chama kushinda urais. Kwisha.

6. Mrema, Cheyo, Shibuda, Mtatiro, Kafulila, Nassary, Machali, Mkumbo, Lipumba nk
. Walikua na maono wakawika ila walipokubali kuishi kwa kutamani wao tu ndo waonekana wanang'ara na kuwa kileleni kisiasa basi hakuna wanachosema chenye tija kwa Taifa bali wanatamka chenye tija kwa familia zao.

Mwenyenzi Mungu anapokutumia uwavushe watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine usiweke tamaa, kubali kuishi kwa njaa ila utimize lengo na dhamira ya nafsi yako. Bora ujipe Likizo ya Muda usome upepo ila usiruhusu kununuliwa
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,375
2,000
Hata Tundu Lissu ni mwepesi sana, sema hawamtaki tu, Tundu ndiyo mwepesi kuliko wote kwa maana ni attention seeking sana, hivyo kama wangemuhitaji wala usingemsikia tena huko kwenu akikimbizana na vumbi Tunduru au sijui Bahi, kwenye ile Uongozi wa tls tu tayari alishalainika kila siku alikuwa kwa wakubwa wa CCM kujitambulisha kupiga ma selfie na akina Ndugai na kurusha kwenye mitandao, muulize Maalimu Seif alipopewa ving'ora na CCM alikuwaje? Acheni kujidanganya, wote wako kimaslahi binafsi tu.
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
3,625
2,000
Sumaye hata Lowassa wangekubali kuwa neutral lakini yaliyowapata walikuwa hawana jinsi, kuporwa Kwa ardhi na mkwe kubambikiwa kesi kuliwafanya hawa wazee watembee macho chini. Aliezoea favour za CCM hauwezi upinzani.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,407
2,000
Hata Tundu Lisu ni mwepesi sana, sema hawamtaki tu, tundu ndiyo mwepesi klk wote kwa maana ni attention seeking sana, hivyo kama wangemuhitaji wala usingemsikia tena huko kwenu akikimbizana na vumbi Tunduru au sijui Bahi, kwenye ile Uongozi wa tls tu tayari alishalainika kila siku alikuwa kwa wakubwa wa CCM kujitambulisha kupiga ma selfie na akina Ndugai na kurusha kwenye mitandao, muulize Maalimu Seif alipopewa ving'ora na CCM alikuwaje? Acheni kujidanganya, wote wako kimaslahi binafsi tu, ...
Mwingine ni John Pombe Magufuli, anayekwenda kupotea na kusahaulika kuanzia masaa 72 yajayo.

Bahati mbaya kwake huyu ni kuwa, mwisho wake ni wa fedheha zaidi kuliko wote hao kwani uwezekano ni 100% kwa Magufuli kushindwa uchaguzi na kuishia jela kwa mauaji ya watu ya makusudi kabisa!

Wewe humjui Tundu Lissu. Huyu si mbabaishaji kama wewe na baba yenu mwongo mwongo Magufuli. Tundu Lissu hutembea katika maneno yake. Hajawahi ku - retreat wala ku - surrender.
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,375
2,000
Wewe humjui Tundu Lissu. Huyu si mbabaishaji kama wewe na baba yenu mwongo mwongo Magufuli. Tundu Lissu hutembea katika maneno yake. Hajawahi ku - retreat wala ku - surrender.

Acha kujidanganya, hakuna mtu mwepesi na corrupt kama tundu, CCM tu hawana shida naye na wala hawamuhitaji, lkn laiti wangemhuitaji wala usingemsikia, kwa kifupi siyo tishio kwa mustakabili wa CCM.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,407
2,000
Acha kujidanganya, hakuna mtu mwepesi na corrupt kama tundu, CCM tu hawana shida naye na wala hawamuhitaji, lkn laiti wangemhuitaji wala usingemsikia, kwa kifupi siyo tishio kwa mustakabili wa CCM, ...

Real? Real?

Hebu fanya hivi:

1. Onesha ufisadi wa Tundu Lissu nasi tutawaonesha wa baba yenu Magufuli..!

2. CCM haiwezi kumhitaji Tundu Lissu kama ambavyo kamwe haitakuja kutokea Tundu Lissu akaja kuihitaji CCM..!

3. Tundu Lissu ni tishio kubwa na hatari la uwepo wa CCM. Asingekuwa tishio, John Pombe Magufuli asingejaribu kutaka kumuua kijinga na kipumbavu vile..!!
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,375
2,000
Real? Real?

Hebu fanya hivi:

1. Onesha ufisadi wa Tundu Lissu nasi tutawaonesha wa baba yenu Magufuli..!

2. CCM haiwezi kumhitaji Tundu Lissu kama ambavyo kamwe haitakuja kutokea Tundu Lissu akaja kuihitaji CCM..!

3. Tundu Lissu ni tishio kubwa na hatari la uwepo wa CCM. Asingekuwa tishio, John Pombe Magufuli asingejaribu kutaka kumuua kijinga na kipumbavu vile..!!

tundu siyo tishio kwa CCM amini hilo, CCM siyo wajinga wanaijua hii nchi nje ndani, wanajua nani tishio na nani siyo, wana watu wao ndani na nje ya nchi wana wana Usalama kila mahali hivyo amini nakwambia wanajua nani ni tishio na yupi siyo, mfano mdogo tu mwaka 2015 Serikali hata ilinunua magari mapya ya washa washa mengi sana na askari wetu walikuwa wanafanya mazoezi mitaani kujipanga kwa maana walijua ni tishio, sasa leo hii umeshasikia Serikali hata ikipasha Jeshi letu moto? Hakuna, kila kitu shwari tu, wanajua kwamba jinsi ya kudili na watu kama tundu ni kumpa anachotaka, nacho ni attention, sasa attention kaipata baada ya Oktoba 28 utaona kitakachofwatia, hautamsikia tena labda kwenye Mitandao, ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom