Mwarabu kumilikishwa Loliondo

Mwarabu kumilikishwa Loliondo

Hata ikiwa uongo watu watahisi kweli, tatizo mnaharibu sana kuliko kujenga ndugu zangu.

Tatizo letu watanzania ni kutokuwa makini kwa kila jambo, tumekuwa ni watu wa kubabaisha babaisha mno hata mahali palipo na usahihi wa hoja, Tabia hii tunayoiendekeza itaendele kututafuna kwa karne nyingi zijazo isipokuwa tumejifunga mkanda kuondoa udhaifu wa watawala. NASEMA hivi kwa sababu hatutakiwa kuwasaidia wamasai wa Loliondo tu kuna wamakonde pia wa Mtwara ambao wanapangiwa kudhulumiwa gesi bila majadiliano; Munapokaa kimya kwa hili na kuangalia mahali fulani hatutafika kokote. Namkumbuka mwanajamii fulani aliandika humu kuwa "walipokuwa wanawapiga wagiriki sisi tulikaa kimya kwa sababu sisi siyo wagiriki. Wakawaendea wasomali kuwapiga tukakaa kimya kwa sababu sisi siyo wasomali, SASA wamekuja kutupiga sisi, lo hayupo hata wa kutusaidia kwa sababu wagiriki na wasomali wote ambao wangetusaidia wamekwisha uawa wote"
 
mmarekani anaitwa mmarekani
mcanada anaitwa mcanada
muUAE anaitwa mwarabu
warabu mbona wanatoka nchi nyingi tu, moja wapo ni Tanzania, sasa hao wote ndio wamiliki? Acheni ubaguzi bana

Hakuna Waarabu Tanzania: Kila moja wetu ni mtanzania, na Loliondo tunazungumzia waarabu wageni sio watanzania.
 
mnataka wazungu na wadenmark pekee ndio waje wawekeze??? pili hii habari ni ya kizushi tu

ashakumu si matusi,acha kuwaza kwa masaburi mkuu,show the sense of patriotism and humanity a little bit,your stomch must not speak more than your brain bungeni
 
Last edited by a moderator:
NI kweli mwarabu alimilikishwa Loliondo na kutokana na juhudi za wabunge kama kina Philp Marmo na mwandishi Stan Katabaro walizuia akaendelea kuwinda kimya kimya huku akifanya kila kitu kama Dubai. Leo Serikali hasa IKULU inammilikisha Mwarabu eneo la Loliondo. Wanafanya hesabu ili kutumia vipengele vya sheria ya ardhi ya kuhaulisha ardhi ya vijiji na kuwa ya hifadhi. Wanadai ni kwa madhumuni ya hifadhi huku mwarabu inasemekana amewinda takriban wanyama 50,000 hadi sasa, amejenga chanzo kikuu cha maji ameweka mtambo wake wa mawasiliano. Halafu leo IKULU inataka kuwaondoa Wamasai. Kwa sababu Serikali haitambui tena sheria isipokua zile za kujinufaisha, TUWAUNGE MKONO wamasai wa Loliondo. WOTE KWA UMOJA WETU TUSIKUBALI

Wanyama elfu hamsini!!?! That adds up to around wanyama elfu mbili mia tano kwa msimu. U are a genius! I envy you!
 
anaepanda juu LAZIMA ashuke chini akishuka ni mitama kwenda mbele, itakuja siku hopefully sooner rather than later tutapata serikali makini alafu utumbo wote wa namna hii utaanikwa wazi. kwani nani anaenforce mkataba kati ya mwarabu wa loliondo na taifa letu zaidi ya serikali yenyewe, ni ngumu kuimagine lakini angalia hii situation kama vile wanakodi nchi kwa muda kidg. hofu yangu iko na hali ya wanyama pori uko, jamaa anaweza komoa piga shaba kila kitu
 
Sasa tunao waandishi wengi wa habari za kiuchunguzi,mitandao kama JF,na walau kidogo nafasi ya kusema tofauti na enzi za Stan Katabalo!

Kwanini hili swala tunalijadili kwa wepesi sana? Hivi kweli Stan Katabalo alipigana bila woga leo tuna puuza damu yake kwa faida ya vizazi vyetu?

Mimi nadhani waandishi wetu kama wana nia njema waanzishe Operation chukua Loliondo kwa faida ya Taifa hili na kuenzi juhudi binafsi za Stan Katabalo!
 
Sasa tunao waandishi wengi wa habari za kiuchunguzi,mitandao kama JF,na walau kidogo nafasi ya kusema tofauti na enzi za Stan Katabalo!

Kwanini hili swala tunalijadili kwa wepesi sana? Hivi kweli Stan Katabalo alipigana bila woga leo tuna puuza damu yake kwa faida ya vizazi vyetu?

Mimi nadhani waandishi wetu kama wana nia njema waanzishe Operation chukua Loliondo kwa faida ya Taifa hili na kuenzi juhudi binafsi za Stan Katabalo!
Mkuu waliopo ni wachache sana na kibaya wengi wao wananunulika.

Inabidi sisi wenye nchi tusimame imara kutakaa haya madhila yanayotuzonga kila kukicha.

Habari zinatufikia kila kukicha kuhusu upuuzi tunaofanyiwa na wanaoendesha serikali. Lazima tuchukue hatua baada ya kuelewa
 
Back
Top Bottom