Mwanzo wa Safari

Liganga

Senior Member
Jul 4, 2007
165
125
Mwanzo wa safari.
===================

Tumeshajua wapi tulipotoka na historia imeandikwa vema,

mimi na wewe tukiwa tumeshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuikamilisha hadi hapa ilipofikia.


Tumeshajua vema wapi tumekwama, tathmini zimefanyika na majalada kuhusu nini chanzo au kikwazo yamejaa tele.

Kwa kiwango kikubwa ni mimi na wewe ndo tumeshikilia usukani wa chombo hiki, kuendelea kuwa hapa ni uthibitisho wa

kulidhika kwetu.Kuamka ni vema,lakin itakua haina maana iwapo utaamka wakati jirani zako wote walishaamka mapema,

wakaokota kuni zote kule msituni, wakateka maji pale kisimani na kuelekea shambani kuzalisha.


Tumeshajua na kutambua wapi twatakakwenda. Wale wote waikwamishao safari yetu wanafahamika kuanzia wanapoishi,

wanapofanyia kazi zao, mbinu na uwezo wao, mianya na nafasi zao. Hakika kila alfajir jua uamka ili mimi na wewe

tupate nafasi nyingine kutekeleza malengo yetu na si yale yaliyotushinda jana. Ufananishapo safari yetu na mapambano,

utatambua yakuwa ushindi wake hauitaji bunduki wala mizinga,bali akili na maarifa mikononi mwa weredi.


Kwa utangulizi huu, naomba sasa tuamke na tuianze safari. Uongozi imara na wenye kuheshimu miiko, miongozo na sheria

ni muhimu ili kuakikisha chombo chetu akipotezi mwendo na mwelekeo.Ni vema kila mmoja wetu atambue malengo ya hii safari,

maana asiyetambua aendako, hakika hatojua iwapo amefika.


MALENGO
=========
1.) Kuhakikisha heshima na mapenzi kwa nyumba yetu inarejeshwa na kuhimizwa.

2.) Kuhakikisha tunalinda shamba letu dhidi ya kwerekwere, viwavi, ngedere,nzige na nguruwe. Maana hawa huvuna wasichopanda

na kutusababishia njaa, shida na maafa.

3.) Kuwawezesha na kuboresha uwezo wa wakazi wa nyumba yetu ili waweze kuvuna na kupanda shamba letu kwa mbinu za kisasa,

kwa ari na hamasa kubwa.Tukisisitiza ushindani wa haki baina ya wakazi wetu.

4.) Kuwachukulia hatua kali wale wote wasio waaminifu nyumbani, wanaodokoa mboga na kutegea kazi.

5.) Kuwa mfano wa kuigwa na majirani zetu na kamwe wasitubeze. Ili litawezekana tukifanikiwa kuhakikisha wananunua chakula,

maziwa, nyama na ngozi toka kwetu,wanakodisha punda na majahazi yetu kwa usafirishaji.



Mwisho
=========
Usisubiri 2010 ili kufanya maamuzi.

Wakati ni huu, mimi na wewe kufungua ukurasa mpya(mwanzo wa safari).

Chombo kianze kamata kasi sasa na 2010 itakua ni kupanga gia kuukwea mlima kitonga.

Fikisha ujumbe huu kwa wakazi wenzio wote.
 
Safari == mabadiliko

Huu ndo uwe mwanzo wa haya mabadiliko. Muda ndo jambo lamsingi leo hii tukiamua tunaweza.

"Uhuru na mawazo mbadala ya watu leo hii, ujenga msingi na elimu kwa kizazi kijacho"
 
Back
Top Bottom