Mwanzo wa mwisho wa Zitto na ACT yake

Mwanzo wa mwisho wa Zitto na ACT yake

Mkuu mimi nilikuwa mwanachama hai wa CCM lakini tangia upendeleo wa vyeti ujitokeze wazi wazi wakati kuna ndugu zangu ilibidi waache kazi kwa kukosa vyeti, wengine wamebakiza miaka mine tu wasaafu. Nimemfuata Wema Sepetu CHADEMA.
Zidi kumfata tu hadi uingie naye shimoni.
 
SAFI.
SIJUI WALITAKA AKATAE! MBONA MBATIA ALITEULIWA NA STILL ALIKUWA UKAWA.
TUACHE SIASA ZA UKILITIMBA.
Kitila pika kazi.
Kikwete hakuwahi kusema hatoshirikiana na upinzani wala Mbatia hakuwahi kusema watu wa aina yake wasiteuliwe na Rais ndiyo maana hatukuzungumzia unafki
 
Kikwete hakuwahi kusema hatoshirikiana na upinzani wala Mbatia hakuwahi kusema watu wa aina yake wasiteuliwe na Rais ndiyo maana hatukuzungumzia unafki
Ila aliwahi sema Mh.Lowassa ni fisadi?
 
Binafsi kama mchoma mahindi ambae sina elimu tena mnyonge, nisie kua na sauti wala athari juu ya kitu chochote, mpaka kufikia jana nilikua sio mwanachama wa chama chochote.

Lakini kulingana na hali ya kisiasa nchini hasa ubabe wa serikali ya awamu ya tano pamoja na adhalimu wa wazi wa kukumbatia uovu uliochupa mipaka wa mkuu wa mkoa wa DSM

Nilijikuta napinga utawala wa CCM pamoja na CCM yenyewe, kiasi cha kuamua kutafuta chama ili niweze kuonyesha upinzani wangu dhidi ya chama tawala.

Nia pamoja na azma yangu mpaka kufikia juzi ilikua ni kujiunga na ACT-Wazalendo, ili niwe mwanachama hai hii ni kutokana na mambo yafuatayo

1. Nilikua namkubali sana Zitto Kabwe
2. Nilikua naukubali sana upambanaji wa Kitila
3. Sera za ACT zilikua zinakaribiana kidogo na mafundisho ya imani yangu

Lakini kuanzia sasa sina tena imani na Zitto kabwe wala Kitila, licha ya kuwa wameonyesha kua wao ni wanafiki kiasi gani bali pia hawafai hata kwa urafiki wa kawaida kwa maana hiyo chama cha ACT ni chama cha kinafiki

Kwa muono wangu kwa sasa Zitto hana tofauti na Lipumba, na endepo lingetokea hili kabla ya mkutano wao wa azimio la arusha basi angejikuta anahutubia CCM wenzie tu.

Hakika zito kwa sasa watanzania wa mlengo wa upinzani tumeshakustukia, na hiyo inaonyesha ni jinsi gani nyinyi watu wa kigoma mlivyo, tulili liona hilo kwa Dr. Aman Kaburu, na sasa wewe umetudihirishia kua wapinzani hasa wa Kigoma mkoje.

Kuanzia leo sintokua na imani tena na wapinzani hasa wa kutoka Kigoma, pia kaka Zitto tegemea watu wengi wata ku-unfollow kwenye page zako zote kwa sababu umetuangusha wengi tulio kua tunalukubali kwa mlengo wa upinzani.

Amini ukipenda hili ndio anguko lako kisiasa kama alivyoanguka Mrema, na huu ndio mwanzo wa mwisho wako, hakuna atakae kuelewa tena. Asante kwa machache ya kinafiki uliyoyasimamia nakutakia utimishi mwema kwa CCM chini ya kimvuli cha ACT


Mnyanyembe wa Mboka
Umemsahau Machali.
 
Si kweli na wewe unapotosha tu Kama hayo magazeti.Kilichopo ni kua elimu imefanikiwa Ila siyo kwa asilimia Mia lkn imefanikiwa,Kuna changamoto za upungufu wa fedha na walimu kutokana na kwamba kumekua na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaohudhuria shule,hata wale waliokua wameacha Sasa wamerejea shuleni na walimu ni walewale kidadi kwahiyo kuna changamoto hiyo,lkn kusema elimu bure iko ICU humtendei yeyote haki kwakua huo ni uongo.Serikali iliyopo inafanya kitu ambacho kimeshindikana kufanyika kwa miaka 30 na zilizoitangulia.

Ulichoandika hapa ni uongo uliokithiri kwa miaka mingi kwa CCM kuwahadaa WATANZANIA. Huna ushahidi wowote wa kufanikiwa kwa elimu hapa nchini. Huoneshi kuwa elimu imefanikiwa kwa asilimia ngapi, badala yake unakuja na hadidu za rejea
 
Ulichoandika hapa ni uongo uliokithiri kwa miaka mingi kwa CCM kuwahadaa WATANZANIA. Huna ushahidi wowote wa kufanikiwa kwa elimu hapa nchini. Huoneshi kuwa elimu imefanikiwa kwa asilimia ngapi, badala yake unakuja na hadidu za rejea
Ukweli utajulikana tu,Ila kusema elimu bure iko ICU huo ni uongo wa kiwango cha lami.
 
Back
Top Bottom