Mwanzo mwisho wa maisha ya Franco Luambo Makiadi

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,210
85,321
Franco ambaye alizaliwa Tarehe 6 Julai, 1938, katika Kijiji cha Sona Bata Magharibi ya Kongo, atakumbukwa na watanzania wakati alipofanya onyesho kweye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 1973.

Baba yake Joseph Emogo alikuwa mfanyakazi wa Shirika la reli wakati mama yake alikuwa mama wa nyumbani akioka mikate na kuuza Sokoni wakati akiwa bado mdogo wazazi wake walihamia katika Jiji la Kinshasa.

Franco alipofikisha umri wa miaka Saba alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na akiwavutia wateja pembeni mwa mama yake wakati akiuza mikate.

Kipaji chake kiligunduliwa na mpiga gita Paul Ebengo Dewayon ambaye alijitolea kumfunza Franco jinsi ya kupiga vyema Ala hiyo.

Mwaka 1950, wakati huo akiwa na umri wa miaka 12, alitengeneza jina akiwa katika bendi ya Watam ya Ebengo Dewayon ambaye alikuwa kiongozi wa bendi hiyo.

Alizikonga nyoyo za wapenzi kwa uwezo wakemkubwa wa kupiga gita ambalo lilikuwa kubwa kuliko yeye.Miaka mitatu baadaye Franco alirekodi wimbo wake wa kwanza uliokuwa na jina la Bolingo na Ngai na Beatrice.(mpenzi wangu Beatrice) baada ya kukubalika kuwa mmoja wa wana bendi ya Loningisa Studio, kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane alitoa nadhiri kwamba ataishi na Franco katika maisha yake yote yaliyosalia.

Chini ya Henri Bowane Franco akawa mpiga gita la solo ambapo alikuwa kipiga staili ya Sebene na akaanza kutunga na kuimba yeye mwenyewe kwa staili za rumba na za kiafrika na hata za kilatini.

Mwaka 1955 pamoja na kwamba alikuwa akipewa kazi nyingi katika Studio hapo Franco aliunda bendi akiwa na Jean Serge Essous iliyokuwa ikipigia katika Baa ya Ok.

Huko Kinshasa.
Mwaka uliofuatia bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Ok Jazz na baadaye ikaitwa T.P.Ok. Jazz kuenzi sehemu ilipoanzia bendi hiyo yaani katika Bar yenye jila la OK (OK. Bar)

Katika kipindi cha mwaka mmoja bendi yake ya T.P.Ok Jazz ikagundulika kwamba inataka kumpiku Vicky Longomba ambaye alikuwa katika bendi ya Grand Kale ya African Jazz ambayo ndiyo ilikuwa bendi kubwa nchini Kongo.

Franco alishadai kwamba bendi yake ya Ok.Jazz ilitoa zaidi ya album 150 katika kipindi cha miaka 30.
Mwaka 1958 Franco alifungwa kwa kosa la ajali ya barabarani.

Purukushani za kisiasa katika nchi yake ya Kongo Franco alilazimika kuhamia Ubelgiji kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake.
Baada ya nchi kutulia ikiwa chini ya uongozi wa rais Mobutu Seseseko Kuku Ng’endu Wazabanga ambaye alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire, Franco alirudi nchini mwake na kafanya tamasha kambambe la Festival Ok. Jazz f African Arts lililofanyika Kinshasa mwaka 1966.

Ok Jazz iliisaidia sana Serikali ya Mobutu katika mambo ya kisiasa kupitia nyimbo zake zilizokuwa na mafunzo mengi.Franco hakuona soni katika kusifia mazuri wala kuonya mabaya pamoja na kwamba aliwekwa lupango mara nyingi alipokiuka taratibu za nchi.

Mwaka 1970 Franco alipata pigo kubwa kwa kufiwa na mdogo wake Bavon Marie Marie amabaye kifo chake kilitokana na ajali ya gari alipokuwa akiendesha kwa hasira baada ya kukorofishana na kaka yake Franco juu ya mwanamke ambaye pia alikufa katika ajali hiyo.

Mwaka 1980 Serikali ya Kongo (Zaire) ilimtunuka hadhi ya kuwa Babu wa muziki wa Kongo kama heshima kwa juhudi zake za kufufua uchumi amabo ulikuwa ukiyumba nchini humo.

Wakati wa maisha yake aliwahi kuongeza uzito ghafla na kufikia paundi 300 ambazo ni sawa na kilo 136. Franco alifyatua wimbo mkali mwaka 1985, uliotikisa nchi wa Mario. Lakini mwaka 1987 fununu zikaanza kuzagaa kwamba Franco yu mgonjwa.

Wimbo aliotengeneza mwaka huo kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Attention na SIDA’(Jihadhari kwa Ukimwi / AIDS)
Franco alifariki tarehe 12, Oktoba 1989 akiwa katika hospitali mojawapo huko Ubelgiji na mwili wake ulisafirishwa kupelekwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire zamani) ambako jeneza lake lilipitishwa mitaani kuagwa na wananchi likisindikizwa na ulinzi mkali wa Polisi na baadaye serikali ikatangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa.

Wakati wa siku hizo za maombolezo radio ya taifa hilo ilikuwa ikipiga nyimbo za Franco hadi tarehe 17, Oktoba 1989 alipozikwa kwa heshima zote za kitaifa.

Naomba kuwasilisha...


images-2.jpeg
 
Shukrani sana mkuu kwa historia tamu kabisa.

Huyu jamaa acha kabisa, nilikuwa na album zake ya nyimbo kama 100 hivi, bahati mbaya nikalifuta
Ni moja ya watu kwa kweli walikuwa vichwa.
Mkuu, binafsi naeeza nikasema enzi zile Lwambo ndie alikua gwiji la muziki wa Zaire, akifuatiwa na Sam Mangwana
 
Katika kipindi cha mwaka mmoja bendi yake ya T.P.Ok Jazz ikagundulika kwamba inataka kumpiku Vicky Longomba ambaye alikuwa katika bendi ya Grand Kale ya African Jazz ambayo ndiyo ilikuwa bendi kubwa nchini Kongo.
Mkuu hapa kuna utata kidogo. Vicky Longomba (Baba wa Awilo) ifahamike ni mmoja kati ya watu sita wanaosemekana walianzisha bendi ya OK Jazz (June 6, 1956) akiwa pamoja na kijana Franco (akiwa na umri wa miaka 18). Vicky (mwimbaji) akiandamana na Brazzos (mpiga besi gitaa) alishirikiana na African Jazz 1960 walipokwenda Ubeligiji kutumbuiza waliokuwa wanadai uhuru wa KONGO. Mwaka 1961 alianzisha bendi ya Negro Success na alirejea OK Jazz 1962 akiongozana na Brazzos ambako alikuwa Co-President wa OK Jazz hadi 1971 alipotoka OK Jazz na Kuanzisha Orchestre Lovy du Zaire bahati mbaya afya yake ilizorota na baada ya miaka mitatu akaacha kupiga muziki. Alipotoka OK Jazz ikabadili jina na kuwa TP OK Jazz. Swala la Franco kumpiku Vicky kwa ujumla halipo. Ni Vicky ambae alimuongoza Franco kwenye mambo ya utawala kwani alikuwa na experience na mambo hayo na alikuwa mkubwa kwa Franco. Tukumbuke Franco hakuwa na elimu kubwa ya shule hivyo Vicky na Grand Kalle walikuwa watu wake wa karibu (kaka zake).
 
Mwaka 1980 Serikali ya Kongo (Zaire) ilimtunuka hadhi ya kuwa Babu wa muziki wa Kongo kama heshima kwa juhudi zake za kufufua uchumi amabo ulikuwa ukiyumba nchini humo.
Kwa kiingereza alitunukiwa hadhi ya Grand Master (Fr. Grand Maitre) pamoja na Kalle Jeff (Joseph) (Mwanzishi wa African Jazz bendi ya kwanza ya kisasa Congo na The African Jazz School of music) na baada ya hapo Franco (mwanzilishi wa OK Jazz School of Music) akajulikana kama Grand Maitre Franco..... na kale Grand Kalle ambae Franco na Tabu Ley walimbatiza jina la Baba wa Mziki wa Kisasa wa DRC. Na hadhi hiyo ni wanamuziki wawili tu DRC walio wahi kuipata. Hivyo Neno Babu hapo lina maana hiyo ya Grand Master of Congolese Music.
 
Alifariki kwa ugonjwa gani?
Franco alifariki wakati akitibiwa katika hospitali moja jijini Brussels, Ubelgiji, tena alifariki mbele ya dada yake Marie Louise, mkewe Annie baadhi ya wanawe na baadhi ya wanamuziki wa bendi yake.


Fununu zilianza kuenea mapema 1987 kwamba nguli huyo alikuwa anaumwa sasa zikachukua sura mpya baada ya watu kuanza kuvumisha kwamba huenda maradhi ya Ukimwi ndiyo yaliyokuwa yamekatisha uhai wake.

Hii ilitokana na sababu mbili: kwanza, mwaka huohuo 1987 zilipovuma habari hizo kwamba jamaa anaumwa baadaye akaanza kutoonekana mara kwa mara jukwaani. Lakini pili ni baada ya kutoa albam yake – ya mwisho akiwa hai – yaAttention na SIDA (Jihadhari na Ukimwi)
 
@Masiya,Mkuu, tukitaka kupata kufahamu nini kikitokea kwenye Bendi ya TP OK Jazz ni lazima pia tukumbuke bendi ilivyokua na historia ndefu kuanzia miaka ya 1950. Na kati ya mwaka 1950 na 1960 wanamuziki walioanza bendi wakati huo na kujulikana kama OK Jazz walikua Vicky Longomba, Jean Serge Essous, François Luambo Makiadi, De La Lune, Augustin Moniania Roitelet, La Monta LiBerlin, Saturnin Pandi, Nicolas Bosuma Bakili Dessoinand na muimbaji Philippe Lando Rossignol.

Walianza kupiga muziki wao mahali palipojulikana kama Longisa Studios mjini Kinshasa wakiwa wasanii huru wa kujitegemea kabla ya kuunda bendi hii mwaka 1956. Jina OK Jazz lilitokana na klabu cha pombe walipokua wakichezea muziki wao, OKBar. Bendi hii mpya ilikua ikitumbuiza mara kwa mara kwenye Studio ya mjini na mwishoni mwa wiki wakicheza kwenye harusi.

Mwaka 1957,muimbaji kiongozi Philippe Lando Rossignol akaondoka kwenye bendi hiyo na badala yake Edo Nganga kutoka Congo Brazaville akawa muimbaji kiongozi. Baadaye mwaka huo Isaac Musekiwa kutoka Zimbabwe mcheza Saxophone akajiunga na bendi ambayo uongozi wake wakati huo ulikua kati ya Vicky Longomba, Essous na Franco.

Bendi hii ilivunjika baada ya Vicky Longomba na Jean Essous kujiondoa na kumuacha Franco peke yake. Hapa aliamua kuleta waimbaji wapya na kuimarisha bendi. Baadaye Vicky Longomba alipoamua kurudi pamoja na halaiki ya waimbaji wazuri wengi, akiwemo Verckys Kiamungana Mateta na kuanza kukabiliana na Bendi maarufu kipindi hicho ya African Jazz ya Joseph Kabasele, Franco akijivunia miamba ya wanamuziki na kuvutia wanachama wengi Bendi ikapewa jina TP OK Jazz TP ikimaanisha Tout Pouissas.
 
Kwa kiingereza alitunukiwa hadhi ya Grand Master (Fr. Grand Maitre) pamoja na Kalle Jeff (Joseph) (Mwanzishi wa African Jazz bendi ya kwanza ya kisasa Congo na The African Jazz School of music) na baada ya hapo Franco (mwanzilishi wa OK Jazz School of Music) akajulikana kama Grand Maitre Franco..... na kale Grand Kalle ambae Franco na Tabu Ley walimbatiza jina la Baba wa Mziki wa Kisasa wa DRC. Na hadhi hiyo ni wanamuziki wawili tu DRC walio wahi kuipata. Hivyo Neno Babu hapo lina maana hiyo ya Grand Master of Congolese Music.
Mkuu, asante sana kwa kutulisha madini adhimu....
 
Back
Top Bottom