Mwanza: Wizi wa Watoto wachanga Wakithiri

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Akizungumza ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, alisema kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu, matukio manne ya wizi wa watoto yamejitokeza.

Kamanda Mutafungwa alieleza mbinu zinazotumika na wanawake hao kuiba watoto ni pamoja na kujenga urafiki na wazazi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ya kuabudia.

"Mbinu zinazotumika kuiba watoto ni akina mama walio na niovu kuweka urafiki wa karibu na mama wazazi,kisha kuaminiwa na kuachiwa watoto ndipo wanapata mwanya wa kutoroka na watoto hao,"alisema Mutafungwa.

Alisema mnamo Oktoba 16 mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi katika kata ya Kisesa wilayani Magu,mwanamke aliyejulikana kwa jina la Happiness Amosi(22) mkazi wa wa kijiji cha Kinyambwiga wilayani Bunda alimwiibia Neema Baraka (28)mtoto wa miezi mitatu wakati wakiwa Kanisani na kumpelekea hawalaya ambaye alimdanganya alikuwa na ujauzito wake.

"Matukio mengine matatu ni Oktoba 12 mtoto mwenye miezi sita aliibiwa na kijana asiyefamika kwa sura huko maeneo ya mtaa wa Uhuru kata ya miromgo, Oktoba 30 majira ya saa mtoto mwenye umri wa miezi sita aliibiwa huko Igombe wilayani Ilemela na Oktoba 13 majira ya saa tano asubuhi mtoto mwenye umri wa miezi nane aliibiwa katika mtaa wa Isela,vitendo hivyo vimetokea vyote mwaka huu,"alisema Mutafungwa.

Aidha Mutafungwa alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na kutambua jukumu lao la maingi la kuwalea na kwalinda watoto wao, kuacha uzembe wa kumwamini kila mtu, suala hilo limekua likichangia kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wanaotafuta watoto kwa muda mrefu kupata njia ya kuiba watoto.

Naye Tabiza Sospeter aliomba jamii kuhakikisha wanaondoa unyanyapaa kwa wanawake ambao hawakujaliwa kupata mtoto,ili kukomesha tatizo la wizi wa watoto ambalo watuhumuwa wakubwa wamekuwa ni akina mama waliyo na matatizo ya uzazi.

Aidha Tabiza aliomba serikali kuchukua hatua kali kwa mtu yoyote atakayebainika kufanya kitendo cha kikatili cha kuiba mtoto ambaye asiye wake.

Chanzo: Nipashe
 
Kama wanataka watoto, wawe wanatoa matangazo mbona watoto wapo wengi tu mitaani! watapata bila kukwiba
 
Watoto hao ni WA mchongo,bint anajifanya ana mimba halafu anavizia ikifika miezi Tisa ya kujifungua anaiba mtoto kana kwamba amejifungua yeye
 
Akizungumza ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, alisema kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu, matukio manne ya wizi wa watoto yamejitokeza.

Kamanda Mutafungwa alieleza mbinu zinazotumika na wanawake hao kuiba watoto ni pamoja na kujenga urafiki na wazazi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ya kuabudia.

"Mbinu zinazotumika kuiba watoto ni akina mama walio na niovu kuweka urafiki wa karibu na mama wazazi,kisha kuaminiwa na kuachiwa watoto ndipo wanapata mwanya wa kutoroka na watoto hao,"alisema Mutafungwa.

Alisema mnamo Oktoba 16 mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi katika kata ya Kisesa wilayani Magu,mwanamke aliyejulikana kwa jina la Happiness Amosi(22) mkazi wa wa kijiji cha Kinyambwiga wilayani Bunda alimwiibia Neema Baraka (28)mtoto wa miezi mitatu wakati wakiwa Kanisani na kumpelekea hawalaya ambaye alimdanganya alikuwa na ujauzito wake.

"Matukio mengine matatu ni Oktoba 12 mtoto mwenye miezi sita aliibiwa na kijana asiyefamika kwa sura huko maeneo ya mtaa wa Uhuru kata ya miromgo, Oktoba 30 majira ya saa mtoto mwenye umri wa miezi sita aliibiwa huko Igombe wilayani Ilemela na Oktoba 13 majira ya saa tano asubuhi mtoto mwenye umri wa miezi nane aliibiwa katika mtaa wa Isela,vitendo hivyo vimetokea vyote mwaka huu,"alisema Mutafungwa.

Aidha Mutafungwa alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na kutambua jukumu lao la maingi la kuwalea na kwalinda watoto wao, kuacha uzembe wa kumwamini kila mtu, suala hilo limekua likichangia kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wanaotafuta watoto kwa muda mrefu kupata njia ya kuiba watoto.

Naye Tabiza Sospeter aliomba jamii kuhakikisha wanaondoa unyanyapaa kwa wanawake ambao hawakujaliwa kupata mtoto,ili kukomesha tatizo la wizi wa watoto ambalo watuhumuwa wakubwa wamekuwa ni akina mama waliyo na matatizo ya uzazi.

Aidha Tabiza aliomba serikali kuchukua hatua kali kwa mtu yoyote atakayebainika kufanya kitendo cha kikatili cha kuiba mtoto ambaye asiye wake.

Chanzo: Nipashe
Mwanza kunakitu hakiko sawa juu ya watoto, naimani Mwanza ndio Mkoa/mji wenye watoto wengi wa mtaani
 
Back
Top Bottom