MWANZA: Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanajamvi.

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa jijini Mwanza wakati wakijaribu kuwatoroka askari polisi pindi wakiwapeleka mahali ambapo wenzao walikuwa wamejificha ili waweze kufanya uvamizi, huku jeshi la polisi mkoani humo pia likifanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shortgun ikiwa na risasi tatu, ambayo inadaiwa kuporwa kwenye kampuni ya ulinzi ya ulinzi wa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: ITV
====

Tazama mjadala wa habari hii ukisomwa kwenye JamiiLeo..

Kwanini wauawe badala ya kuwajeruhi ili kuwakamata? polisi hawaruhusiwi kuua mtu yeyote yule. Hao waliowaua hao watu ndio majambazi washtakiwe mara moja maana hata mauaji ya wafanyabiashara wa madini walidanganya ni majambazi wakawaua kumbe ni wafanyabiashara na ilikuja kubainika baada ya kufanya uhunguzi. Hivi hukumu ya Bagenyi imeshatekelezwa?
 
Safi sana...

Kanda ya Ziwa kwa sasa imechafuka sana, kila kona ujambazi unafanyika mchana mchana.

Musoma huko nasikia watu wameanza mchezo wa kufunga mtaa tena mchana kweupe na wanavyoiba ni visimu vya wa akina mama, juzi kati mtu kaingiliwa na majambazi wanataka awape elfu 90 mtaji wake wa kuuza samaki, wanajua mpaka kauza samaki wapi na mtaji wake ni shilingi ngapi.
 
Habari wanajamvi.

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa jijini Mwanza wakati wakijaribu kuwatoroka askari polisi pindi wakiwapeleka mahali ambapo wenzao walikuwa wamejificha ili waweze kufanya uvamizi, huku jeshi la polisi mkoani humo pia likifanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shortgun ikiwa na risasi tatu, ambayo inadaiwa kuporwa kwenye kampuni ya ulinzi ya ulinzi wa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: ITV
Nini Maana halisi ya "kunyang'anya silaha harakaharaka?"
 
Wakiwapeleka mahakamani wengine wanatoka mbinu waliyopewa na mkuu wa kaya wewe unamuona jambazi ana silaha unamchelewesha wa nini akikuwahi si ataleta madhara mlaze mapema
 
Kwanini wauawe badala ya kuwajeruhi ili kuwakamata? polisi hawaruhusiwi kuua mtu yeyote yule. Hao waliowaua hao watu ndio majambazi washtakiwe mara moja maana hata mauaji ya wafanyabiashara wa madini walidanganya ni majambazi wakawaua kumbe ni wafanyabiashara na ilikuja kubainika baada ya kufanya uhunguzi. Hivi hukumu ya Bagenyi imeshatekelezwa?
Wewe kama si jambazi basini familia ya jambazi.
 
Kwanini wauawe badala ya kuwajeruhi ili kuwakamata? polisi hawaruhusiwi kuua mtu yeyote yule. Hao waliowaua hao watu ndio majambazi washtakiwe mara moja maana hata mauaji ya wafanyabiashara wa madini walidanganya ni majambazi wakawaua kumbe ni wafanyabiashara na ilikuja kubainika baada ya kufanya uhunguzi. Hivi hukumu ya Bagenyi imeshatekelezwa?
Acha kutetea majambazi basi,last week ijumaa majambazi wamumuua kijana wa duka la jumla mchana wa saa tisa makondeko dar,nawachukia mno majambazi,kama wanaua watu kwa nini wao wasiuliwe?,au wao kuuliwa wana kinga?
 
Chuki zako sio sababu ya kufanya sheria zipinde, kuna taratibu za kutoa hukumu ya kifo kwa wauaji. Sasa hao wanaosemwa ni majambazi huko mwanza waliua mtu?
 
Kama ushawahi kukoswakoswa na risasi zaidi ya moja huwezi ku shuti kwa kujeruhi...
 
Chuki zako sio sababu ya kufanya sheria zipinde, kuna taratibu za kutoa hukumu ya kifo kwa wauaji. Sasa hao wanaosemwa ni majambazi huko mwanza waliua mtu?

Nachukia mijambazi, badala ya kufanya kazi ya halali kwa nguvu zao wenyewe wafanikiwe wanaishia kuibia watu na kuua watu wasio na hatia.

Ningekuwa me IGP au Mkuu Kaya ningetoa order kabisa ukikamata jambazi piga risasi kabisa hiki kizazi cha miharamia kipotee kabisa.

Ningefanya kama Rais wa Philipines anavyofanya tokomeza kabisa kizazi cha watumia na wauza unga.

Na hapa majambazi yote tokomeza kabisa, mpaka mtu akifikiria kuiba ajihisi kujikojolea kabisa kwa woga. Ukicheka cheka nao kwa sheria za ajabu watazidi kuleta madhara,, dawa ni kutokomeza kabisa..
 
Mbona husemi yale majambazi yaliyochota pesa na kubeba kwenye masandarusi nayo yauawe?
 
Back
Top Bottom