Mwanza: Vivuko viwili vyasimamishwa

Mwanza: Vivuko viwili vyasimamishwa

Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoa Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu, ambapo Waziri amesisitiza kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

MV%20LINK.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021, na kueleza kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.
Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.
Kumbe bado tuna watu wenye akili na busara TZ. Huyu Waitara ni mmoja wao

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Maendeleo kwa nchi za dunia ya tatu ni dhana ya ndotoni. Kwa fikra hizi zinazoamua kuhusu mstakabari wa maisha ya wananchi kwa namna hii ni hakika pasi na shaka kwamba kuna ki-aina fulani cha laana.

Unafungia vivuko viwili ambavyo vimekuwa ni msaada kwa serikali, wananchi na nchi kwa miongo mingi tu just kirahisi tu hivyo simply una mamlaka ya kufanya hivyo.

Laiti nchi hii tungelikuwa na watoa Huduma ambao ni serious na reliable kama mwenye vyombo hivi japo wawili kila Wilaya ni hakika tungekuwa ni taifa la kutolea mfano kwa ubora na uhakika wa Huduma zetu.

Mungu atusaidie ili tuweze kuzitumia mbongo na akili alizotujalia, tuachane na matumizi ya akili za matope.
"NOT YET UHURU"
Wewe hujui kitu kuhusu uendeshaji wa hivyo vivuko. Huwezi ukaendesha kivuko bila service wala wafanyakazi wenye sifa. Likitokea la kutokea mtaanza kulaumu serikali. Pale kuna vivuko vya Kitano hakuna tatizo lolote.
 
Sarikali ingesaidiana na mmiliki kufuta suruhu ili watu wahudumiwe. Mbona sababu zenyewe ni za kawaida. We hujaona vyombo vinavyomilikiwa na serikali vinaua. Mv Bukoba!
Pia kivuko cha Nyakaliro-kome(kisiwani) ni kibovu na hatari zaid Tanzania lakini bado kinapga kazi sembuse kamanga ferry?
Mwita waitara ni mlevi tena wa pombe kali
 
Wewe hujui kitu kuhusu uendeshaji wa hivyo vivuko. Huwezi ukaendesha kivuko bila service wala wafanyakazi wenye sifa. Likitokea la kutokea mtaanza kulaumu serikali. Pale kuna vivuko vya Kitano hakuna tatizo lolote.
Pole.
Siku moja utatoka usingizini
 
Wewe hujui kitu kuhusu uendeshaji wa hivyo vivuko. Huwezi ukaendesha kivuko bila service wala wafanyakazi wenye sifa. Likitokea la kutokea mtaanza kulaumu serikali. Pale kuna vivuko vya Kitano hakuna tatizo lolote.
Unaonekana hujui chochote kabisa
 
Maendeleo kwa nchi za dunia ya tatu ni dhana ya ndotoni. Kwa fikra hizi zinazoamua kuhusu mstakabari wa maisha ya wananchi kwa namna hii ni hakika pasi na shaka kwamba kuna ki-aina fulani cha laana.

Unafungia vivuko viwili ambavyo vimekuwa ni msaada kwa serikali, wananchi na nchi kwa miongo mingi tu just kirahisi tu hivyo simply una mamlaka ya kufanya hivyo.

Laiti nchi hii tungelikuwa na watoa Huduma ambao ni serious na reliable kama mwenye vyombo hivi japo wawili kila Wilaya ni hakika tungekuwa ni taifa la kutolea mfano kwa ubora na uhakika wa Huduma zetu.

Mungu atusaidie ili tuweze kuzitumia mbongo na akili alizotujalia, tuachane na matumizi ya akili za matope.
"NOT YET UHURU"
Duuuh!!! Hawa ndio wa tz. Taratibu zikifuatwa wanalalamia,zisipofuatwa wanalalama!!! Ni bora mussolini angekuwa rais wa nchi yetu tungekaa wote mstari mmoja ulionyooka kama rula hakuna fyuu wala swiii!!
 
Sarikali ingesaidiana na mmiliki kufuta suruhu ili watu wahudumiwe. Mbona sababu zenyewe ni za kawaida. We hujaona vyombo vinavyomilikiwa na serikali vinaua. Mv Bukoba!
Hiyohiyo mv bukoba ndio ilitupa fundisho. Wakae watafute suluhu!?!?! Taratibu zinajulikana naamini mmiliki anazijua ila ni ukaidi tu!! Ndugu yangu vyombo vya usafiri wa majini vina standards za kufuata kimataifa na zetu,serikali haiwezi kuweka rehani maisha ya watu wake simply coz taratibu hazikufutwa. Alternative zipo nyehunge ferries na kigongo busisi
 
Duuuh!!! Hawa ndio wa tz. Taratibu zikifuatwa wanalalamia,zisipofuatwa wanalalama!!! Ni bora mussolini angekuwa rais wa nchi yetu tungekaa wote mstari mmoja ulionyooka kama rula hakuna fyuu wala swiii!!
Pole.
Hujui uliandikalo
 
Hiyohiyo mv bukoba ndio ilitupa fundisho. Wakae watafute suluhu!?!?! Taratibu zinajulikana naamini mmiliki anazijua ila ni ukaidi tu!! Ndugu yangu vyombo vya usafiri wa majini vina standards za kufuata kimataifa na zetu,serikali haiwezi kuweka rehani maisha ya watu wake simply coz taratibu hazikufutwa. Alternative zipo nyehunge ferries na kigongo busisi
Pole
 
"awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya

1. kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.

2.Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine,

3.pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma"

Mosi, Hizo ndo sababu za kusimamiahwa kama zilivyotajwa na mamlaka husika, naomba unisaidie kunionesha ubovu wa vyombo uko wapi huenda sijasoma vizuri.

Pili, umejiuliza hivi vyombo huwa vinahudumia watu wangapi, mizigo kiasi gani na magari mangapi kwa siku ili tujiulize mandala wake ni upi?

Kama ni kwa kutegemea chombo kimoja ama vingine vilivyopo siku zote unasemeaje capacity ya vyombo hivyo, je, vina uwezo wa kuhudumia abiria wake wa kila siku pamoja na jao walokuwa wanahudumiwa na vyombo hivi?

Huoni hii ndiyo inaweza kuwahatarisha wananchi zaidi kwa vile watalazimika kujazana kuliko uwezo wa vivuko hivyo husika.

Je? Unajua ni kiasi gani wananchi watahangaika wakati Sisi tupo kwenye viyoyozi na ma V8 mtaani huku tukiwa hatuna mpango nao?

Ndugu, najua unawajali Watanzania, ila jaribu kufungua macho zaidi uone kuna kitu hakipo sawa pahala.
Acha propaganda wewe mbona vya kule ziwa nyasa vimeondolewa majini!?! Maisha ya ndiyo first priority ya serikali yoyote duniani
 
Hii isue imekaa kifigisu figisu zaidi ya uhalisia wake, yaani waitara amekutana na kukaa na ‘uncle’ wake kitana wakaandika hukumu yao kwa kamanga ferry,
 
Pole.
Hujui uliandikalo
liseme tulielewe kama waziri kaomba rushwa thibitisha humu,cc tunafuata sababu zilizotolewa na ni za kisheria, sasa wewe kama una kitu unakijua kilicho chini ya zulia ungekieleza hapa na kama hakiwezi kuelezeka hapa usingeleta kabisa hoja yako hapa maana hili ni jamvi la udadisi
 
Karukwaa mtu hapo

Tupeleke dreamliner jaman ivushe wale........

Back
Top Bottom