Mwanza tupo karibu na ziwa ila tunanunua maji ya kusomba.

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,307
2,000
Tofauti na maeneo ya katikati ya jiji la Mwanza, hivi karibuni tumekumbwa na janga la maji. Yani tuna mabomba ya maji lakini maji hakuna. Sasa tunanunua maji ya kusomba kutoka ziwani. Dumu 500 hadi 1000. Sababu haieleweki. Wengine tumeenda mpaka kwenye ofisi za idara husika za maji kuuliza ni kwanini. Wao wanadai kuwa gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa wanashindwa kuwasha mashine muda wote. Kwahiyo maji maeneo ya mbali na mji hayafikiwi na maji sababu ya baadhi ya mashine kuzimwa.

Viongozi husika tunaomba muangalie swala hili. Tukikosa maji tukaendelea kutumia haya maji ya ziwani si muda mrefu tutaanza kuugua kichocho na kipindupindu.
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,056
2,000
Jamaaenu anafahamu hilo? Muda si mrefu atalitolea tamko na mtapata maji ya kutosha!!!!...

Lakini pia ningependa hiyo mitambo ya maji iharibike kabisa..ili muisome namba vizuri.....mnajiona sana na huyo mtu wenu.....
 

ding'ano

Senior Member
Feb 24, 2013
182
500
Jamaaenu anafahamu hilo? Muda si mrefu atalitolea tamko na mtapata maji ya kutosha!!!!...

Lakini pia ningependa hiyo mitambo ya maji iharibike kabisa..ili muisome namba vizuri.....mnajiona sana na huyo mtu wenu.....
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,307
2,000
Jamaaenu anafahamu hilo? Muda si mrefu atalitolea tamko na mtapata maji ya kutosha!!!!...

Lakini pia ningependa hiyo mitambo ya maji iharibike kabisa..ili muisome namba vizuri.....mnajiona sana na huyo mtu wenu.....
Dah. Kuwa na huruma jamaa
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,707
2,000
Nachoshangaa nini sasa kwa nchi
Hii mbona mororo tu kwa ujumla tanzania haikutakiwa kuwa na uhaba wa huduma ya maji kila kona maji wananchi hawana maji
 

KIOO

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
6,144
2,000
Akili zenu zinafanana basi itakuwa, nlifkiri gharama za kiwanja cha bird zimeelekezwa kiwanjani baada ya kutatua mahitaji muhimu kwa jamii.

Kumbe hata maji ni tabu halaf mapesa chungu nzima anaenda kujenga kiwanja cha bird, vizuri sana ni bora mkae hivyo hivyo.

Blood Full.
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,043
2,000
Kuna Wilaya moja nilienda kwenye kituo cha Afya eti hakuna Maji na miundo mbinu ya Maji IPO kabisa. Ukiangalia kama mita 800 hivi unaona Maji ya Ziwani Yale pale lakini kituo cha Afya hakina Maji!! Nilishangaa sana
 

Dindira

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,926
2,000
Matatizo ya maji peleka kwa mbunge wako. Hapa lete matatizo pasua kichwa. Kutoa maji ziwani kuyaleta mjini hakuhitaji genius afike hapo Mza. Ni suala la uamuzi tu.
 

Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,163
2,000
unasema mwanza, nenda ukerewe kisiwa kimezungukwa na maji uone watu wake wanavyopata shida ya maji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom