Mwanza: Rais Magufuli atinga uwanjani ghafla kwenye mechi kati ya Buhongwa vs Nyamwaga

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,498
54,923
Akiwa na Ulinzi mkali na wa hali ya juu kabisa, leo jioni rais Magufuli aliamua kwenda kuangalia mpira wa Miguu uliokiwa unaendelea jinini mwanza.

Rais Magufuli akiwapungia mkono washabiki waliohudhuria mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga katika uwanja wa Nyamagana leo.
67db5e252f453f0ec67b980ec9637238.jpg
81ba8b8204293b10ed6d5f5205b826d6.jpg
59145e03c3fc7c11b40445a22ad9c22c.jpg

Rais Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa FC mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana kuangalia mpira.
303b448d33b06cd5f51bb5767c66c347.jpg

Rais Rais Magufuli akiangalia mpira pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela katika uwanja wa Nyamagana.

Rais Magufuli akinunua karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
753de3f0a1b1dc8223667823cc7ba781.jpg

eda5f4227dac65395ad63348072b698c.jpg

Rais Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi ya Buhongwa na Nyamwaga FC.
Mwanza
 
Kwa mara yangu ya kwanza niliona bunduki zikiwa hadharani katika msafara wa Raisi wakati wa mazishi ya Marehemu Abeid Amani Karume.

Leo naona naona mtu aliyeshiba akiwa ametangulia mbele ya Rais na kidole kwenye trigger,nimeogopa!!!

Kama Taifa tupo katika hali ambayo si ya kawaida na viashiria hivi ni lazima vichunguzwe kwa makini. Kuna mahali tumekosea na kama hatutajisahihisha tutafika mahali ambapo hatukutegemea.
 
Hivi alilipia kiingilio na watu wake? Na kwanini amekaa sehemu ya Timu badala ya Jukwani? Je, alikuwa anasubiriwa uwanjani kuwa geni rasmi? kama siyo alikagua timu wakati gani? je, baada ya kuingia uwanjani Mpira kweli uliangaliwa ama Mkulu ndo aliyeangaliwa (na mashabiki)?
 
Nimeangalia sana ulinzi huu, inaonyesha wazi ni dhaifu usio na mbinu ya kumlinda rais hata kama wanawaangalia washabiki.

Haiwezekani rais anazungukwa na kundi kubwa la walinzi kiasi kwamba hata wao wenyewe hawawezi kuona vizuri walio nje ya mita tano kutoka kwenye mzingo.

Ulinzi wa ajabu sana huu
 
Back
Top Bottom