Mwanza ni jiji kubwa kuliko Arusha ila kumejaa omba omba kila mtaa

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Kwanza niseme kabisa, kulinganisha jiji la Mwanza na Arusha ni matumizi mabaya ya akili. Arusha ni kamji kadogo Sana kwa Mwanza, Arusha inaingia mara mbili kwa Mwanza.

Tatizo ni kwamba hawa ndugu zetu wenyeji wa Mwanza, tukiwaambia wasizae Sana kama nyumbu hawatuelewi, mwisho wake jiji zima limejaa omba omba kila mtaa.

Yaani inafikia hatua omba omba wanapita nyumba kwa nyumba, ofisi kwa ofisi kuomba msaada.

Omba omba hawa, walio wengi ni watoto wadogo, hii maana yake ni kwamba wametelekezwa na familia zao au wamezikimbia familia zao kutokana na hali ngumu ya maisha.

Zaeni kwa mpangilio, msifyatue hovyo hovyo, yaani mji mzima umejaa omba omba kila kona hadi mtu unaona kero, ata ukisema utoe msaada, utatoa kwa wangapi kwa siku?

Nawasihi tena wenyeji wa Mwanza, hacheni kufyatua hovyo hovyo na kutelekeza watoto wadogo.
Mwanza-erial-2.jpg
 
Ukiona omba omba sehemu jua wanapata wasingekuwa wanapata wasingeendelea kuomba na waombaji wengi Mwanza wametoka mikoa mingine Arusha ikiwemo.Sasa unataka waombe arusha wakati huko waombwaji nao ni waombaji??
 
Kwanza niseme kabisa, kulinganisha jiji la Mwanza na Arusha ni matumizi mabaya ya akili. Arusha ni kamji kadogo Sana kwa Mwanza, Arusha inaingia mara mbili kwa Mwanza.

Tatizo ni kwamba hawa ndugu zetu wenyeji wa Mwanza, tukiwaambia wasizae Sana kama nyumbu hawatuelewi, mwisho wake jiji zima limejaa omba omba kila mtaa.

Yaani inafikia hatua omba omba wanapita nyumba kwa nyumba, ofisi kwa ofisi kuomba msaada.

Omba omba hawa, walio wengi ni watoto wadogo, hii maana yake ni kwamba wametelekezwa na familia zao au wamezikimbia familia zao kutokana na hali ngumu ya maisha.

Zaeni kwa mpangilio, msifyatue hovyo hovyo, yaani mji mzima umejaa omba omba kila kona hadi mtu unaona kero, ata ukisema utoe msaada, utatoa kwa wangapi kwa siku?

Nawasihi tena wenyeji wa Mwanza, hacheni kufyatua hovyo hovyo na kutelekeza watoto wadogo.View attachment 2323537
Omba omba wengi wa Mwanza wametoka Arusha, Dodoma, Singida....Sie Wazazi wetu wanatufundisha kupiga Kazi haijalishi tumezaliwa mia au mia mbili lkn kila mtoto anakauwanja kake huyu kafuga huyu kalima.....Tunawalisha sana nyie watoto wa mikoani☺️
 
Back
Top Bottom