chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 11,983
- 20,634
Rais Samia amefungulia mikutano ya hadhara, na katika majiji ambayo Chadema wanajiwinda kuyadhibiti ni Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam. Wanatafuta ajenda nzito za kutikisa na kuwashika wananchi.
Arusha walifanya tukio, Sasa hivi wote wananyea debe, angalau wanaarusha wanaelewa hatua zimechukuliwa.
Kwa Jiji la Mwanza, Mkurugenzi wa Jiji na maafisa ardhi nao hawajachelewa kuwapa wapinzani ajenda.
Kuna habari kwamba Jiji la mwanza limeuza nyumba zake katikati ya Jiji kwa bei ya kutupa, bila kufuata taratibu.
Maeneo hayo yameuzwa wakati machinga mjini hawana maeneo ya biashara, wameenda kutupwa igoma nyamongolo huko ambako hakuna wateja, na kiloleli, na bila kuzingatia maelekezo ya Rais ya ubia kati ya sekta binafsi na Serikali, kiasi kwamba wangeongea na taasisi yoyote ile au mtu binafsi, akawekeza, wakawa wanakula faida, na eneo likabali lao.
Ni kwamba, wanamwanza wameibiwa.
Stanslaus Mabula, wewe ndio mbunge wa Nyamagana, bila shaka unalijua Jimbo linakuwaga la moto, hasa ukizingatia "sponsor kafa".
Angelina Mabula, wewe ndio Waziri wa hiyo ardhi ya serikali iliyouzwa, na uhamishaji miliki usingefanyika bila kupitia Ofisi za ardhi. Na sijui kwa nini kama mamlaka ya serikali inapotaka kuuza ardhi isitakiwe kupata Kibali Cha Waziri wa Ardhi au Waziri Mkuu! Au Rais! Uwepo udhibiti.
Mna kazi moja tu, kuirudisha ardhi hiyo, hatutaki Rais aanze kupata shida kupata kura za Mwanza wakati alishanyoosha mapito yake kwa miradi mikubwa ya maendeleo.
Ni hapohapo mwanza machinga aliyekuwa anauza ndizi, Jiji lilimwaga ndizi zake na kumpiga, Leo Jiji Lina ardhi hapohapo katikati ya mji linaiuza!
Njia moja tu, kurejesha hizo nyumba, na Kila Afisa aliyehusika apelekwe mahakamani, wanamwanza wataridhika wakiwaona wahusika wanapanda kizimbani, na kupelekwa gereza la Butimba.