Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemhukumu Mwandishi wa habari Albert Sengo kulipa faini ya Shilingi Milioni tano au kifungo Cha Mwaka mmoja jela. Mwandishi Sengo amechagua kulipa faini na kuachiliwa huru.
Sengo aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya kutoa taarifa mtandaoni na kuendesha Kituo cha habari mtandaoni (GSENGO Online TV) bila kuwa na leseni kinyume na Sheria.