Mwanza: Mwandishi wa habari Albert Sengo ahukumiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni tano au kifungo Cha Mwaka mmoja jela

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,759
4,307
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemhukumu Mwandishi wa habari Albert Sengo kulipa faini ya Shilingi Milioni tano au kifungo Cha Mwaka mmoja jela. Mwandishi Sengo amechagua kulipa faini na kuachiliwa huru.

Sengo aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya kutoa taarifa mtandaoni na kuendesha Kituo cha habari mtandaoni (GSENGO Online TV) bila kuwa na leseni kinyume na Sheria.

PIA SOMA:
= > Mwanza: Mwandishi wa Habari, Albert Sengo Kizimbani akishtakiwa kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni
 
Vijana wanaambiwa wajiajiri na wakifanya hivyo wanakutana na mambo kama hayo.
 
Waambie vijana wawe wanafata taratibu,unaendeshaje online TV bila leseni? Angefata taratibu na akahukumiwa tungemtetea kaonewa.
Unajua unaongelea mil 1 lakini?

Najua kwa fogo kama wewe unaiona hio pesa ni ndogo kwa kijana mwenye mtaji wa simu yake tu na bando.
 
Unaendesha kituo cha runinga mtandaoni huna leseni.Wakati TCRA inataka hata wenye channel YouTube wasajiliwe.
Sijui sasa mnatetea kitu gani hapo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom