Mwanza mnajiaibisha, hamjielewi nini?

Mwanza mnajiaibisha, hamjielewi nini?

Mimi siamini mwanasiasa atakujakunisaidia mimi kwa maisha yangu mpaka nimsujudu na kulazimisha au kuwashawishi wengine wamfuate yeye kama mkombozi.

Waache wao wafuate imani zao na mapenzi yao na wewe ufuate msimamo wako pia.

Wewe unawashangaa na wao wanakushangaa.
 
Mmmh! ni kweli wamesahau kila kitu?? ni kweli hawajielewi??? mi naona kuna haja ya kututaka radhi!!! mtu kwao acha yapite ila nina imani hata angekuwa kapita lowasa hakika arusha nzima pangezizima! TUTAKE RADHI
 
Magufuli sio msukuma ni mzinza ila ni kabila Dogo sana sema kalelewa na baba wa kufikia msukuma.
 
Nenda kawazue wasiwe wanajitokeza, maana hapa sio wote wanakusikia
 
Nilikua Nairobi 2008 siku ambayo wamarekani walipiga kura kumpata raisi wao mpya, baada ya matokeo kutoka Kenya nzima ilizizima watu hawakwenda makazini kisa kushangilia ushindi wa Obama eti ni mkenya mwenzao na atawasaidia kuwaletea maendeleo na kuwatolea umaskini, leo hii Kenya ya 2008 wananchi wao wanaikumbuka nilikua huko mwezi ulopita hamna maendeleo wala nini zaidi ni kuishi kwa hofu kwa kuogopa alshabaab.

Nije kwenye point yangu ya msingi nashindwa kuwaelewa wasukuma Tangu Magufuli ateuliwe kuwa mgombea wa CCM basi wamesahau kila kitu pale Mwanza walishaapa kuwa hawaitaki CCM ila kisa tu msukuma kateuliwa basi wamefuta tabu zote walizozipata kwa miaka 10 kwa sababu ya mtu mmoja.
Ni wazi kwamba kama CCM wangemteua mtu yyte tofauti na msukuma basi leo hii kanda ya hizi kelele wanazopiga zisingekuwepo.

Hint point: Mna miaka mingine kumi ya kusota CCM kocha mpya wachezaji wale wale.

if you decide to tell a lie. At least tell an intelligent lie.
 
Mleta mada bila shaka kuna jambo kubwa limekubana moyoni ni bora usubiri wakati wake ndio ulitoe, ni lini watu wote wa Mwanza walitamuka kwamba hawaitaki CCM, una ushahidi gani kwamba wote wamefurahia kuteuliwa kwa Magufuli?, kama suala ni umati wa watu wanaojitokeza kwani umati huo ndio kwanza umejitokeza kwa Magufuli tu hapo Mwanza?
 
Sijaona ulichokiita point km kweli ni point iliyokusukuma kuiweka vichwana mwa maelfu ya wanajf,naamini ukichotaka kutuonyesha hapo ni kuwa ukisafiri kwenda kenya.soma vizuri,humu ndani kuna watu daily wanaenda china na kwingineko na hawajitangazi kwa namna yako.
 
Hivi ni mzinza au msubi!?

Ni Msukuma, full stop!!

Ni sehemu ya Wasukuma waliohamia Uzinza kwa ajili ya kufuata malisho miaka ya '50 na '60!! Ni Wasukuma waliotoka 'Bugwe' (yaani ng'ambo ya ziwa Viktoria ukiwa upande wa Sengerema). Watu wasipotoshe hapa!
 
Hozo ni hisia zako but kumbuka hakuna mwana siasa atakaye kusaidia maishani mwako zaidi ya kujisaidia mwenyewe na hata kama akija mpanzani kama hayuko makini bado mambo yatakuwa making. Mimi imani yangu kubwa naona Magufuli ataibadili nchi hii
 
Tatizo la watanzania walio wengi ni mfumo wa elimu na umaskini wa watawaliwa,

ukiletewa chumvi,kanga,tisheti na kofia, basi unachekelea mpaka unaanguka chini,

una sahau machungu ya miaka 10 na hili watawala wameshajua udhaifu wa watawaliwa,

ni umaskini wao watu maskini uwaga hawajitambui kabisa ukizingatia na kichwani wameshalishwa matango mwitu ya elimu yetu ya kuunga unga basi ni shiiiiida nyingine,
 
2005 Hakuna rais nilimuona wa maana kama kikwete nikampa kura yangu ila alichotufanyia sitokaa nisahau
 
Back
Top Bottom