Mwanza: Maduka mengi ya wahindi hayatumii EFD'S

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,248
2,000
Maduka mengi ya raia wa kitanzania wenye asili ya kihindi hayatumii mashine za EFD's, TRA mkoa wa Mwanza sijui wanafanya kazi gani maofisini? serikali inakosa mapato, wafanyabiashara wanapata faida kubwa sana kwa kuiibia serikali.

Mkoani mwanza, maduka yanayouza pikipiki, magodoro, TV, nk. hayatumii mashine hizi, mashine wanazo ila ukifika wanakuandikia resit za kawaida, ukiuliza mbona hunipi resit ya EFD wanasema, kama unataka EFD BEI NI TOFAUTI, sasa kwa watanzania hawa ninao wajua ukishawaambia hivyo wenyewe wanaondoka tu...!

Ki ukweli, TRA bado sana, tokeni maofisini mwende field, kwani hamna kikosi cha mashushushu? mnaweza mkawaagiza vijana wenu waende madukani, mnawapa fedha kabisa ili wajifanye kama wananunua bidhaa ili mthibitishe madai haya, msisubiri mwananchi aliyefanyiwa hivyo aje kwenu, wengine huo muda hawana.

Kamishna wa TRA toka ofisini nenda field.
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,730
2,000
Wahindi na wafanabiashara wengi wa Mwanza wapo juu sheria, au ndio utajiri wa Maafisa wa TRA wa hapa maana hata wale walioajiliwa majuzi tu tayari wameisahkuwa matajiri!
Nampongeza sana mmiliki wa QSS, studio ya kupiga na kusafisha picha, tangu enzi zile hadi leo pale hata sh. 1000 tu unapewa risiti halali ya EFD.
 

silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,355
2,000
Nadhani kunahaja ya waziri husika kufanya ukaguzi wa kushtukiza kutumia mashushu wake binafsi kisha awasokote hao wafanyakazi.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
38,045
2,000
Kuna watu wanajifanya wana uchungu sana na nchi hii
 

TEAM VIBAJAJI

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,864
2,000
Nchi hii sisi wanyonge ndio walipaji wakubwa wa kodi maana hatuna pakuikwepea lakini matajiri wao kodi kwao nikama hiyari tu mfano ndio kama huo naukweli nikwamba kunaviongozi huko kwenye mamlaka husika wanaokula nao
 

Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,338
2,000
mmmh jamani c uwaache kwani siku wakikamtwa utawasaidia kulipa faini
 

Mjomba Itufae

Senior Member
Dec 6, 2016
183
250
Yaani baada ya kusoma tu kichwa cha habari, naunga mkono hoja. Nilikua huko wiki mbili zilizopita na nilipita maduka mengi ya wahindi. Bidhaa inauzwa kwa mfano sh 150,000 na unatakiwa hapo upewe risti yako ya manunuzi. Wao wanakwambia sh 180,000 wanakupa na risit. Ukibagain wanakwambia wanakupa kwa sh 150,000 hiyo but hawatoi risiti. Kwa hiyo kuna ukwepaji mkubwa wa kodi. Na najua wahusika wanalijua hilo ila ndo mye mye myeeee

Itufae Shoe Shine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom