Mwanza: Kichanga cha wiki mbili chapotea hospitalini

Mwanza: Kichanga cha wiki mbili chapotea hospitalini

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,120
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linachunguza tukio la kupotea katika mazingira ya kutatanisha kichanga cha wiki mbili ndani ya wodi ya akina mama waliojifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Butimba ya wilaya ya Nyamagana mkoani humo.

Kichanga hicho chenye jinsi ya kike kinadaiwa kupotea baada ya mama yake mzazi, Irene Juma, mkazi wa Serengeti mkoani Mara kwenda maliwatoni na aliporejea hakumkuta mwanaye kitandani, hatua iliyomfanya apigwe butwaa.

Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Juma Mfanga, ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema limeipaka matope hospitali hiyo.

Aidha, kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne Muliro, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na juhudi za kumpata mtoto huyo zinaendelea.

CREDIT: ITV
 
Habari hii ina zaidi ya wiki ndio imeletwa JF leo?
 
Kichanga cha wk mbili unakiteka alafu unaenda kukapa nini kale? Kuna watu wana roho mbaya sana
 
Wanakalea.. .na hatakuja kujua kama wale si wazazi wake halisi..

Au ndio vile..utajiri...
Kichanga cha wk mbili unakiteka alafu unaenda kukapa nini kale? Kuna watu wana roho mbaya sana
 
Back
Top Bottom