Mwanza inarudi nyuma huku Arusha ikiendelea

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
29,097
Reaction score
35,478
Wana JF

Sina lengo la kupambanisha Mwanza Vs Arusha ila kiukweli nashindwa kuelewa nini kimeisibu Mwanza.

Mwaka 2002 Nikiwa shuleni Mwanza nilijiona kama nipo Dar ndogo. Mwanza ilikuwa moto. Mambo yalikwenda faster mji ulikua unakua kwa kasi sana

Nilikuwa nikiamini kufikia 2015 jiji la Mwanza litakuwa la mfano kwa ukuaji wake cha ajabu na kushangaza Arusha ndio inakuja faster huku Mwanza ikidorora kama mtoto mwenye utapiamlo, kulikoni?

Tatizo nini Mwanza? Kama kuongozwa imeongozwa na CDM muda mzuri tu kwanini haipai kwa kasi ilee!?

Nashindwa hata kulinganisha Mwanza VS Arusha maana Arusha kwa sasa ipo moto vibaya kama hali itaendelea kuwa hivi tutegemee Arusha kuwa ndio jiji la pili kwa ukubwa Mwanza inakuja kupitwa na Dodoma itanikera sana.
 
hizi mada zinagawa watu kikanda na kikabila, kuna mada nyingine ya moshi vs dodoma, Bukoba vs Moshi n.k, hizi mada zinaanzishwa na watu wa kanda ya ziwa na ni kwa ajili ya kusakama tu kaskazini...upuuzi mtupu
 
Sasa kama Mameya walikuwa Mabula na Matata , unategemea nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…