Mwanza: Chui ashambulia askari wanne, Wawili walazwa ICU

Mwanza: Chui ashambulia askari wanne, Wawili walazwa ICU

Asant kwa muongozo. Iko mjini au porini? maana Najua Wilaya ya Ilemela ni mjini kabisa
Nyamagana ndio town sana. Ilemela sio sana mkuu japo ipo town kiasi chake mkuu.

-Silasc-
 
Huu mwaka wao walah,
Arusha wanagongwa,Mwanza wanaliwa,kah
Kuna mkono wa watafuna Gomba hapa sio bure

thA God thA bubbs!!
 
Hakuna vya kupumua, wanaume wamemsaka kona zote wamepambana na chui kufa kupona hadi kulazwa, wa Dar angeingia uvunguni wiki nzima. wanashindwa kupiga tu game itakuwa chui mnyama!!! au wamefikiri ni ile bia?
Chui tu mpaka unalazwa wajameni? Halafu mko watatu!!!

Ungekuwa muhenga nikisema " LINDU AMWOKOA KAPILIMA" ungenielewa.
 
View attachment 579976
Askari wanne na raia mmoja wajeruhiwa vibaya kwa kushambuliwa na chui katika kijiji cha Kabangaja kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Majeruhi wawili akiwemo askari wa wanyamapori amelazwa katika kitengo cha uangalizi maalumu ICU katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure baada ya kupata majeraha makali kichwani.

Chanzo: ITV

Weka facts sawia kwanza: Sekou Toure ni Hospital ya Mkoa ama Ni Hospitali ya Rufaa?

Pili punguza mhemuko: Elezea tukio lilivyoanza, mambo yalivyofanyika na hitimisho sio uaandika generally! Waandishi wenyewe siku hizi hivyo tu!
 
Wanaopondea hawa jamaa ningependa kuona wanavolunteer kwenda kupambana na chui. Yule paka mnachekacheka mnadhani anafanya utani
 
Eti umesemaje??
image-jpeg.336646
Hamjui chui usimfananishe na fisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bugogwa kwa kuwa ni sehemu ya Ilemela tutaita ni mjini ila kiukweli bado ni kijijini kwenye mwambao wa ziwa Victoria kama unaenda Kayenze (kama ni mwenyeji wa Mwanza)..kuna uwezekano chui akawa anaisha kwenye miamba miamba yenye vichaka
Mkuu kwa mazingira ya kabangaja ni ngumu kuishi mnyama kama chui asionekane population ya watu ni Kubwa, na kama hivyo ametokea wapi? Kama ni chui wa watu sawa,
 
Kama ni askari acha washambuliwe mpka wafee mana wamezidi rushwa hizo ni malipo yao

Ni miMi CHalIIiiii Ya "R"
 
Hara mimi nimejiuliza hilo, Ilemela si mjini?
Mnyama chui ni hatari ,katoka wapi?
Ilemela hakuna mapori wala huwezi tembea mita 100 bila kuona nyumba ingawa bado kuna mashamba. Na wala huyo chui si wa kwanza hapa mjini, kuna mwingine alitokea mwaka 2000 mjini kabisa wilaya ya Nyamagana kwenye zile slums Tanesco mlimani mita 100 tu kutoka Bugando hospital, washashi na wajaruo ambao ndio wakazi wa eneo lile walimshambulia kwa silaha za jadi hasa mawe mpaka akafa japo baadhi yao walijeruhiwa kidogo sasa huyu chui wa leo amejitokeza kwa wanyonge wasukuma ambao huishi mbali mbali.

Asante kwa ufafanuzi ingawaje ni ajabu.

Ninakotoka hata nyoka ji adimu sembuse mnyama mkali wa miguu minne.

Inaelekea Mwanza mjini unaweza kujikuta unafukuzwa na nyara ya serikali!
 
Back
Top Bottom