Mwanza: Basi la Mohammed Trans lapinduka, wawili wafariki

Mwanza: Basi la Mohammed Trans lapinduka, wawili wafariki

Ajali jamani Bunda napo leo pikipiki yavaa Bajaji eneo la Reza karibu na Posta ila Dereva TOYO sio bodaboda na ameumia na kukimbizwa hospitali ya DDH Bunda.
 
Picha ndio kitu cha msingi.
kweli kwenye habari ya kusikitisha kama hii picha ndio kitu cha msingi ?, sio kwamba huyo mtu badala ya kwanza kujitahidi kupiga picha kuhakikisha kwamba watu wamepata misaada ya kutosha au kutoa habari kwa watu ili wenye uwezo wa kutoa misaada watoe ?
 
Wakuu hayo mabasi ya mohamed hata ukisema nauli buku kutoka dar hadi mwanza sipandi, naomba serikali ifanye uchunguzi ni kwanini mabasi ya mohamed trans ndio yanaongoza kupata ajali? tumechoka kusikia ajali za mohamed trans, mimi naona kama wanatoa kafara watu.
 
Jamani Mohamed Trans ni juzi tu wamepata ajali musoma, leo tena ukiluguru!, mbona sumatra hawawagusi? Mie mohamed trans naogopa kuipanda kabisa.
Uzembe tu wa madereva na magari kutofanyiwa service ya kutosha hizo imani zenu kila saa mnawaza kafara kafara tu.
Mtazidi kufa
 
Uzembe tu wa madereva na magari kutofanyiwa service ya kutosha hizo imani zenu kila saa mnawaza kafara kafara tu.
Mtazidi kufa

Pamoja na imani kiongozi hiyo huwezi kuzuia kwani ni hulka ya mwanadamu lakini mohamed wamezidi, mfano halisi mdogo ukipanda bus toka mwanza hadi dsm huwezi kukosa bus la mohamed njiani limepaki kwa matengezezo tena makubwa! Mfano pale manyoni kuna bus lao wamelishusha machine, jiulize hao abiria shida waliopata hadi kupata usafiri mwingine!
 
ni mabovu sana, tatizo trafiki sijui wanafanya kazi gani?
 
AJALI TABORA: Watu 6 wafa, kadhaa wajeruhiwa leo baada ya basi la Mohamed toka Mwanza-Dar kupinduka eneo la Makomero mpakani mwa Sindida na Tabora.
 
AJALI TABORA: Watu 6 wafa, kadhaa wajeruhiwa leo baada ya basi la Mohamed toka Mwanza-Dar kupinduka eneo la Makomero mpakani mwa Sindida na Tabora.

sindida ndo wapi?
 
Last edited by a moderator:
Haya mabasi yafungiwe kwa muda angalau wapate muda wa kujipanga upya.
 
Basi hilo limepinduka majira ya saa nane mchana, ambapo maiti na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.
 
Back
Top Bottom