Mwanza: Afisa tabibu Joseph Chacha Marwa aliyedakwa na TAKUKURU, Afikishwa Mahakamani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986

AFISA TABIBU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA RUSHWA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imemfikisha Mahakamani Afisa tabibu (Clinical Officer) wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba) Bw. JOSEPH CHACHA MARWA (45) kwa kosa la kupokea Rushwa kinyume na Kif cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Inadaiwa kwamba, Afisa Tabibu huyo wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba) Bw. JOSEPH CHACHA MARWA (45) mnamo tarehe 14/04/2021 alipokea rushwa ya Sh. 400,000/= kutoka kwa ndugu wa mgonjwa (jina limehifadhiwa) ambaye ndugu yake huyo alifika hospitalini hapo kwa lengo la kupata matibabu na ndipo Afisa Tatibu huyo alipomuomba fedha mgonjwa kiasi cha Sh. 600,000/= ili aweze kumfanyia upasuaji.

Uchunguzi wa tuhuma hii umekamilika na Afisa huyo mnamo tarehe 8/06/2021, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kufunguliwa shauri la rushwa namba 60/2021 kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akisomewa mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Bi. Dorothea Kinyonto mbele ya Hakimu Mheshimiwa Lukumay, mtuhumiwa amekana mashtaka yanayomkabili. Aidha, Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena tarehe 01/07/2021.
  • WAKATI HUO HUO TAKUKURU Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza, imemfikisha Mahakamani Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwang’ombe Kata ya Hungumalwa, Wilaya ya Kwimba Bw. LEONARD ENOS HOLOMOL (45) kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na Kif cha 15 (1) (a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
  • Mwenyekiti huyo aliomba rushwa kwa wananchi zaidi ya 12 kwa kuwachangisha kila mmoja Sh. 2000/=, wananchi ambao walikuwa wanahitaji kupata vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA ili waweze kuwa na sifa ya kuwa wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.
  • Mwenyekiti huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa, ili waweze kupata vitambulisho, ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA wanahitaji fedha hivyo inabidi wachange kila mmoja Sh.2000/= azipeleke katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA ndipo watapata vitambulisho kitu ambacho uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini si utaratibu halali.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo tarehe 3/06/2021, na tarehe 04/06/2021 amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba na

kufunguliwa shauri la rushwa namba 3/2021 kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akisomewa mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wakili JOVIN MAJURA mbele ya Hakimu Mheshimiwa JOHN JAGADI mtuhumiwa amekana mashtaka yanayomkabili.

Aidha, Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena tarehe 15/07/2021.

WITO:

TAKUKURU Mkoa wa Mwanza inaendelea kuwahimiza watumishi mkoani humu kuzingatia miiko na maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kazi na pia watumishi wawaelimishe wananchi kuhusu huduma zinazotolewa kwenye maeneo yao ya kazi na utaratibu sahihi wa kufuata.

Aidha, tunawasihi wananchi wote wa mkoa wa Mwanza kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ili wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

PENDA NCHI YAKO, KATAA RUSHWA

“Kwa taarifa za vitendo vya rushwa fika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu nawe, tumia TAKUKURU APP, piga simu ya dharura namba 113 au tuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 113 au Piga *113# fuata maelekezo” Huduma hii ni ya BURE

IMETOLEWA NA:

...................................

FRANK MKILANYA – 0738 150 162

MKUU WA TAKUKURU (M) MWANZA
 
FRANK MKILANYA – 0738 150 162,karibu wilaya ya misungwi .ujionee Rushwa kwenye ofisi za halmashauri Rushwa kila Kona. Idara ya ardhi,elimu,fedha, maji.
 
Takukuru wasiache kuchunguza ubadhirifu ndani ya chadema ,

Waraka wa Chacha Wangwe upo wazi,

Kuna ufujaji wa fedha za Ruzuku.
 
Wale waliokwapua siku ya May mosi mbona kimya?
 
Yaani rushwa ya laki 6,inatakangazwa,mtuhumiwa anaonyeshwa kwenye vyombo vya habari,lakini wale mbwa wa hazina waliopiga millioni 400 kwa siku,hata majina yao hayatajwi,Tena unaweza Kuta,hakuna hata uchunguzi,wakubwa wote wameishapewa Chao,maisha yanaendelea,Mtu wa kutenguliwa ni Khasim Majaliwa,huyu hana mashiko kabisa,huwa anacheka cheka tu,
 
Afisa tabibu anafanya upusuaji ?????
Taarifa haiko sahihi labda km chanzo cha taarifa kilidanganya baadhi ya taarifa leseni ya afisa tabibu haimuruhusu kufanya upasuaji labda kama alikua anapasua jipu na kma ni jipu haiewezi kia iyo pesa ya 600000.
 
bado rushwa ipo mahospitalini, polisi na mahakamani, takukuru wanapaswa wapige kambi ili kutokomeza rushwa ktk maeneo hayo.
msiwaonee aibu wakamateni wala rushwa wote msiwaache wakiwasumbua wananchi
 
H
Afisa tabibu anafanya upusuaji ?????
Taarifa haiko sahihi labda km chanzo cha taarifa kilidanganya baadhi ya taarifa leseni ya afisa tabibu haimuruhusu kufanya upasuaji labda kama alikua anapasua jipu na kma ni jipu haiewezi kia iyo pesa ya 600000.
Hospitali nyingi za mikoani Cleanical Officers wanafanya upasuaji. Hasa Appendicitis
 
Back
Top Bottom