tamu 3
Member
- Dec 11, 2024
- 88
- 216
MWANETU NENDA SHULENI
1.
Wazazi wako zamani, hatukuenda shuleni,
Hapo kale tuamini, likuwa chache nchini,
Tungelisoma jamani, mengi tungeyajueni,
Mwanetu nenda shuleni, unoe wako ubongo.
2.
Wazazi hatukupata, nafasi ya kwenda shule,
Ujuzi tuliopata, sio mwingi huko kale,
Kukosa shule twajuta, ni hasara ya milele,

3.
Wazazi wako zamani, hatukupata elimu,
Pindi mjarumani, haikupewa muhimu,
Ukishakua zamani, wayaanza majukumu,

4.
Siku hizi bila shule, mwanetu umepotea,
Hutojua mambo yale, kichwani utasumbua,
Na utaishi kikale, kipishana na dunia,

5.
Mwanetu nenda shuleni, ung'amue ya dunia,
Kiwa huko darasani, kusomeni zingatia,
Nidhamu weka mbeleni, mavuno kuyafikia,

6.
Siku hizi bila shule, utaishindwa dunia,
Hautajua mchele, ni wapi umetokea,
Utakuwa msukule, chochote usichojua,

7.
Si vyote utavipata, ukiwa huko shuleni,
Lakini acha kusita, kuingia darasani,
Jifunze kipimo mita, tatumia maishani,

8.
Elimu kwako muhimu, mfano wake ni njia,
Usafirishapo ndimu, humo ndimo tapitia,
Hili ni letu jukumu, mwanetu kukuusia,

9.
Kurusha ndege angani, lazima wende shuleni,
Ujifunze ya angani, huko nako kuna nini,
Ujue dira ya nini, uwendapo Marekani,

10.
Daktari maridadi, lazima ende shuleni,
Tena some kwa juhudi, kwa kufuata kanuni,
Uuache ukaidi, puuzo la darasani,

11.
Kwa mwanasheria nguli, hakwepi kwenda shuleni,
Mwanetu tambua hili, uliweke akilini,
Huko tapata akili, mambo kuyapembueni,

12.
Kiitwa kwenye semina, utoe lolote neno,
Utasema ya maana, yasoleta mgongano,
Hivyo shule kwa kijana, kama ulimi na meno,

13.
Mazingira ya kisasa, tofauti na zamani,
Mwanetu tunakuasa, sipuuze ya shuleni,
Mbeleni tapata pesa, ujuzi wako kichwani,

14.
Elimu ni ufunguo, mwanetu hili kariri,
Takupandisha upeo, cheo nguo na muhuri,
Elimu kikaangio, kupikia ni kizuri,

Denny Jeremias kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 1/4/2025