Ruta nina mashaka na analysis yako, imeifanyia utafiti wa kutosha? au una bifu na Prof Mwandosya? kahusika vipi na ufisadi wakati yeye kapokea mradi ukiwa umeshakwisha? hakuwa waziri wa maji kipindi mradi huu unajengwa, vile vile analysis yako in upotoshaji wa hali ya angalia hapa chini
part a) Mradi huu ulikuwa wa shs. 210 billion ambazo gharama zake zilipanda hadi shs. 225 Billion, sababu ya kuongeza gharama ni kuongeza maeneo ambayo hayakuwa kwenye mpango wa mradi, Jee kuongeza idadi ya wanufaika wa mradi ni ufisadi?? kwanza haya yalifanyika wakati wa Kawamba, Prof anahusika vipi? vile vile hilo ongezeko lilitumika kujenga uzio na kituo cha poliso, nyumba za operators kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya uhalifu maeneo ya mradi, jee hii nao ni ufisadi? isingekuwa busara kama serikali isingeweka ulinzi wa kutosha kwenye mradi huu wa mabillioi ya walipa kodi, jee huu nao ni ufisadi? angalia taarifa ya Kawambwa juu ya ongezeko hilo ambayo iliwekwa wazi kwa watanzania wote kupitia vyombo vya umma
part b) mradi huu unanufaisha zaidi ya hao wanavijiji 10,000 ( si kweli wakazi wa misungwi, kahama, shinyanga na sehemu zingine za mradi wakawa 10,000 tu haiiingii akili.. MISUNGWI na kahama pekee ni zaidi ya 10,000)
c) Mradi kujiendesha wenyewe unatokana na willingness to pay by users, kama users hawawezi kuka cover costs zote ni kazi ya state duniani kote ku subsides hasa kwenye sector ya maji.. kumbuka hata UN mwaka jana wametoa tamko kuwa 'access to safe and clean water is a human right' hivyo ni jukumu la state/dola kuhakikisha haki hii haivunjwi. Maji ni uhai (bahati mbaya TZ ni kati ya dola chache ambazo hazikuunga wala kupinga azimio hili
d) pesa hizi zingetumika kuchimba visima - Hii nayo ni upotoshaji, kwani si kila sehemu ina maji ya chini ya ardhi ambayo yanakidhi viwango vya kiafya, pia kweli karne hii ya 21 bado unashauri tuendelee na technolojia ya visima na pump za mkono? kama tuna maji ya ziwa why visima? acha watu wafaidi rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu amewawekea. Kuna chnagamoto nyingi sana katika kutumia visiwa hasa maeneo ambayo hayana umeme, maana wazo lako la visima linamaanisha kila mtu bado aende na ndoo kisimani na kuendelea kutumia zile pump za mdundiko (hand pump), I know kuna suala la solar lakini ngarama yake ni zaidi ya kuchimba kisima ili kupata solar ambayo itaendesha hiyo pump. Hivyo makadirio yako si sahihi maana umeangalia ngarama ya kuchimba kisima tu bila kungalia namna ya kutoka hayo maji toka chini mita 50 na ziadi ili yawafikie watumiaji mabao wengine wapo zaidi ya km 5 toka kilipo kisima.
e) Mradi huu sio hasara, angalia ni watanzani wangapi hadi leo wanapata haki yao ya msingi ya kupata huduma ya maji safi na salama? watoto wangapi hawatakufa kwa kuhara na magonjwa mengine yaletwayo na maji? ni mabinti wangapi sasa watapata fursa sawa ya kielimu kama watoto wengine wa kiume? kumbuka wanawake na mabinti ndo waliokuwa wakihangaika kwenda kutafuta maji mbali kabla ua mradi huu, ni ndoa ngapi zitapona sasa (yasemakana kuna wamama husingizika kwenda kwenye maji kumbe waenda ka mabwana wa nje.. a joke), shughuli za kiuchumi kwa wamama, watoto wa kike kusoma na n.k ni sehemu ya manufaa ya kuwa na maji karibu, usisahu hata rape cases zitapungua maana hakuna tena cha kufuata maji mbali na tena usiku.
f) soma comment ya NGOKO HAPO.