hali ya afya ya Prof. Haitii matumaini...anything ...its serious....though ilianza so simple...
Nlitiwa moyo sana na habari hii hapa chini wiki iliyopita, wacha niendelee kuiamini..., urudi salama Prof..
Prof. Mwandosya aendelea vyema baada ya operesheni
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 17th August 2011 @ 23:00
WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya amesema anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya mgongo nchini India.
"Nikilinganisha na hali ilivyokuwa wakati nikija (hospitali India) kwa sasa naendelea vizuri nilikuwa na maumivu makali sana," alisema.
Profesa Mwandosya alisema hayo alipozungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kutoka Hospitali ya Apollo nchini India.
Alisema madaktari walimfanyia operesheni kubwa ya mgongo na kumshauri kuendelea kupata matibabu hadi afya itakapokuwa nzuri ndiyo maana hadi sasa yupo hospitali.
Mwandosya ambaye aliondoka nchini takribani miezi miwili iliyopita, alisema baada ya operesheni hiyo kwa sasa madaktari wanamfanyisha mazoezi na wamemshauri aendelee kubaki kwa muda.
Alifafanua kuwa operesheni kama hiyo aliyofanyiwa inachukua mtu hadi miezi mitatu kuruhusiwa kutoka hospitali, hivyo anaamini ataruhusiwa kutoka madaktari watakapojiridhisha.
"Kwa sasa nasikiliza maelekezo ninayopewa na madaktari, wakiniruhusu nitaondoka wakati wowote," alisema Profesa Mwandosya na kuwashukuru watu kutoka kila pembe ya nchi ambao wanamtumia salamu za pole na kumtakia heri ili apone haraka.
Alisema salamu za pole zimekuwa nyingi sana, hivyo anawashukuru wananchi na kuwa hana maneno ya kusema kuhusu salamu hizo na upendo wanaouonyesha, zaidi ya asante.
"Nashukuru wananchi wanaonitakia heri, wapo ambao wangependa kuona narudi mapema…niwaambie tu, wasiwe na wasiwasi hali inaendelea vizuri," alisema Profesa Mwandosya.
Pia, aliwashukuru Watanzania waliopo India wakiwemo maofisa wa ubalozi ambao wamekuwa wakimtembelea mara kwa mara.
"Unapokuwa nje ya nchi, unatamani kurudi na mapenzi kwa nchi yako yanaongezeka maradufu," alisema Mwandosya, ambaye alikuwa akitoa vijembe na utani wa hapa na pale.
Kutokana na hali hiyo, Profesa Mwandosya hatakuwepo nchini wiki ijayo kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji anayoiongoza, hivyo jukumu hilo
atapewa waziri mwingine.
Kabla ya kuzungumza, chumba cha habari cha gazeti hili kilikuwa kikipokea taarifa tofauti kuhusu na afya ya mwanasiasa huyo