Mwandishi wa MWANANCHI atimuliwa kampeni za John Magufuli

Mwanzo nilikuwa sijakuelewa ila sasa,namshukuru Mungu nimekuelewa

ProudMama
Endelea KUNIELEWA hata baada ya Oct 25 pale tutakapojua Mungu amepigana upande upi. Hakuna kitu kibaya Kama kiongozi wa dini au mtu anayesema ameokoka halafu anafanya yaliyo kinyume na neno la Mungu.

Baada ya Oct 25 tutajua Mungu yupo upande upi. Bora viongozi wa dini waliosisitiza maombi bila kuegemea upande wowote.

Queen Esther
 
Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI ndugu Peter Elias ametimuliwa kutoka msafara wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Magufuli, imethibitishwa.

Mwandishi huyo ametimuliwa kwa kosa la kuripoti tukio la mgombea huyo kuzomewa na wafuasi wa Chadema jijini Mbeya hivi karibuni kinyume cha
makubaliano.

Mwandishi huyo aliripoti katika gazeti hilo kwa kichwa cha habari "Magufuli akabiliana na UKAWA Mbeya" na kuweka picha ya mgombea huyo akionyeshwa alama ya vidole viwili.

Tulishindwa kusoma alama za nyakati
 
Back
Top Bottom