Mwandishi wa mapenzi China afungwa jela miaka 10 kwa kitabu cha mapenzi ya jinsia moja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja.

Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza "maudhui machafu".

Jina la kitabu hicho ni "Occupation", lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya "tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume...pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii."

Kwa mujibu wa shirika la habari la Beijing News, bi Liu - ambaye anafahamika zaidi mtandaoni kama kama Tian Yi - tayari amaeshakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Kutengeneza na kusambaza maudhui ya ngono ni kinyume cha sheria nchini Uchina.

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 31, lakini habari hiyo imeripotiwa na vyombo vya habari hivi karibuni.

Polisi waliarifiwa juu ya uwepo wa kitabu hicho baada ya kupata umaarufu mtandaoni.

Bi Liu inasemekana ameshauza nakala zaidi ya 7,000 ya kitabu hicho na vyengine vya ngono na kujipatia yuan 150,000 ambayo ni sawa na $21,604.

Hata hivyo kifungo hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.

"Miaka 10 jela kwa kitabu tu? Hiyo ni miaka mingi sana," ameandika mtumiaji mmoja wa mtandao wa Weibo.

Mtumiaji mwengine wa mtandao huo akalinganisha uzito wa adhabu hiyo na kesi ya mtumishi wa serikali aliyefungwa miaka nane kwa kumnajisi binti wa miaka minne.

"Wale wanaokutwa na hatia ya ubakaji wanafungwa chini ya miaka 10. Mwandishi anafungwa miaka 10."

BBC Swahili
 
Hutaskia kelele sijui wanaharakati hata kama angenyongwa sasa fanya ww wa dunia ya tatu!!
 
Ukiwa na hela weww ndio mtunga sheria..
Na mtunga sheria ndio anaamua lipi ni kosa na lipi sio kosa..
 
Back
Top Bottom