Mwandishi wa habari za kimtandao anahitajika

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises LTD, inayomiliki tovuti ya Global Publishers, Mitandao ya Kijamii, Global Radio na Global TV ina nafasi ya kazi ya Intern ya Mwandishi Mahiri wa Habari za Mtandaoni na Mwenye uwezo wa kuendesha mitandao ya kijamii, mwenye sifa zifuatazo:-

ELIMU: Anahitajika kijana wa kiume au wa kike mwenye Shahada ya Uandishi wa Habari (Degree) au Stashahada (Diploma) ya Mass Communication au Education au Degree ya IT au vyovyote.

SIFA
Aidha, mtarajiwa awe kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 24 anayeishi jijini Dar es Salaam, mwenye uwezo mkubwa wa kuandika kwa UFASAHA lugha ya Kiswahili na Kingereza, Mwenye uwezo wa kutafsiri habari za Kingereza kwenda Kiswahili anayejua VIZURI sana kutumia mitandao ya kijamii (Website, Facebook, Instagram, Twitter, WhatsApp, Telegram na mingineyo) awe mfuatiliaji pia wa habari za mastaa, burudani na matukio ya kisiasa, anayejua kanuni za kuandika TAGS, HASH TAGS, Descriptions na Keywords kwenye mitandao.

Anayejua kutumia Computer na Smartphone.
Unaweza usiwe na Degree wala cheti chochote lakini kama unaweza kufanya hayo yote yalioelezwa kwenye sifa, unaweza kufikiriwa pia.

MWISHO
Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tutumie barua yako ya maombi na CV yako pamoja na vivuli vya vyeti vyako kwa Email hii uwazi@hotmail.com
Mwisho wa kutuma maombi Septemba 25,
 
Kweli kuna binadamu wamezaliwa kuajiriwa, sasa mtu uwezo wote huo kuanzia kuandika makala, keywords, hashtags, social media campaign kwanini asianzishe site yake mwenyewe.

Au mmlipe kwa kila makala anayoandika.
Basi sawa mkuu.
 
Back
Top Bottom