Mwandishi wa habari Johnson Mbwambo yuko wapi?

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Kila nikikumbuka makala zako kwenye Gazeti la Raia Mwema za kumpigia kampeni "Mr just praise me " na kumponda kwa nguvu zako zote "Mr white hair ",huwa naishia kujisemea moyoni mwangu kuwa, "ama kweli hatujui kesho yetu, na kesho ni ya Mungu ".

Na pia ktk jambo lolote ni vyema mwanadamu ukawa na akiba ya maneno.
Wewe Baba yangu mzee Mbwambo hukuwahi hata kubakiza chembe ya akiba, uliamini ulichokiandika kwamba kilikuwa ni sahihi kabisa 100%.

Mimi niliumia Sana, hasa nikizingatia kuwa wewe ni msomi na intellectual mwenye weledi wa kuchambua mambo kwa kina huku ukiweka akiba pia ya baadaye.

Kinachoendelea leo sijui utasema nini, ila ninachokushari Kama una hofu ya Mungu, jitokeze utuombe msamaha wasomaji wako kwa jinsi ulivyokuwa unakera, nilifurahi mno Raia Mwema, ilipopelekwa kulazwa ICU, ila naiombea ipone haraka.
 
mimi ninacholumbuka mbwambo aliandika kwamba MAGUFULI alipaswa kuwa wazir mkuu ili awe na watu wa kumfunga gavana alitolea mfano baadhi ya matamshi na matendo yake kama lile la kupiga mbizi kwa wana wa kigamboni na lile la kuzuia magar yenye uzito mkubwa
 
mimi ninacholumbuka mbwambo aliandika kwamba MAGUFULI alipaswa kuwa wazir mkuu ili awe na watu wa kumfunga gavana alitolea mfano baadhi ya matamshi na matendo yake kama lile la kupiga mbizi kwa wana wa kigamboni na lile la kuzuia magar yenye uzito mkubwa
Baadae alibalika na kuanza kumtetea Mr Gongo na kumponda Mr silent
 
Watu wa aina ya Mzee Mbwambo ni wa nadra. Alikuwa anajua ukweli wa yatakayotokea baada ya Mr. White kuchukua
 
Kipindi ninasoma sana magazeti (kipindi kile kuna Uhuru wa kutoa maoni) kwenye serikali ya kidiplomasia iliyopita,nilikuwa ninafuatiloa sana makala za hawa mabwana...Sijui kama bado wanaandika
1.Ndimara Tegamwande

2.Jenerali Ulimwengu

3.M.M Mwanakijiji (sio huyu wa sasa)

4.Padri Privatus Karugendo

5.Saed Kubenea

6.Johnson Mbwambo

Na wengine waliokuwa conscious...Wanaandika hawa bado?
 
Sidhani kama Mbwambo alikuwa mkereketwa wa Magufuli, lakini alikuwa tu realistic! Hoja yake kuu ilikuwa Magufuli na Lowasa wote hawafai kuwa marais. Sababu Magufuli ni 'dikteta'; asiye muumini wa sheria huku Lowassa ni fisadi. Lakini sababu nchi ni lazima iwe na Rais, na wale ndio candidates, alitumia kanuni ya kuchagua 'shetani' mwenye nafuu na kwake alikua ni Magufuli.

Na alimuona walau anafaa sababu 'hakua' fisadi[ugonjwa mkubwa uliokuwepo wakati huo] na pili alikua ni dikteta mamboleo(benovelent Dictator), ambae kwa mazingira ya kisiasa wakati huo ilihitaji mtu wa aina yake. Na mengi kama matumizi ya mabavu aliyabashiri, yamekua kweli. Kimsingi mbwambo alikua na hoja sahihi kabisa.
 
Aisee ulivyokuwa unataja majina nikaona kama tuko mapacha vile, hapo umemsahau Jabir Idrissa na Mzee wa mikikimikiki(mabala)
 
Enzi hizo mada zinajadiliwa kwa tafakuri kweli kweli, siku hizi habari kuu ni manara na maulidi kitenge wapatana sijui ujinga gani..dah
 
Johnson Mbwambo - Mwandishi Mzuri sana na Alivuma sana na Msemo wake wa kumnukuu Pastor Martin Niemoller

First they came for the socialists, and I did not speak out—
Because I was not a socialist.


Then they came for the trade unionists, and I did not speak out—
Because I was not a trade unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.


Then they came for me—and there was no one left to speak for me.
 
Back
Top Bottom