Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,986
Waandishi hao awali walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu na baada ya kukata rufaa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Ziwa iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya chini ya hakimu mwingine.
Mahakama kuu kanda ya Mwanza leo hii tarehe 20 Disemba 2019 imefuta kesi hii chini ya Kifungu cha 98 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambapo waandishi wa Habari Christopher Gamaina, Wilfred Makuna, Manga Msalaba na Zephania Mandia wapo huru kuanzia sasa.
Vilevile, ufutwaji wa kesi hii ni kufuatia serikali kuonesha kutokua na nia ya kuendelea na kesi hii.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
20 Disemba 2019
Pichani chini: Waandishi wawili Christopher Gamaina (kushoto) na Zephania Mandia (kulia) wakiwa wameshikana mikono na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza, Bw. Edwin Soko (katikati)
Zaidi, soma:
Sent using Jamii Forums mobile app

Mwandishi wa habari Christopher Gamaina afungwa miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu
Anaitwa Christopher Gamaina mwanza Waandishi Christopher Gamaina wa Raia Mwema na Zaphania Mandia wa Channel 10 leo tarehe 18 Aprili, 2019 wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa Gamaina na miaka 4 kwa Mandia. Waandishi hawa pamoja na watu wengine wawili walioshtakiwa kwa kosa la unyang'anyi wa...
www.jamiiforums.com
Sent using Jamii Forums mobile app